Je, ni sahihi Mwamposa kuimba wimbo wa taifa kanisani kwake?

Mkuu nimekuuliza maswali hapo juu ujanijibu wimbo wa Taifa ni nini na tunu za Taifa ni nini
Wimbo wa taifa ni moja ya nembo na tunu za taifa. Haupaswi kufanyiwa dhihaka wala kubezwa na mtu yeyote yule. Ndio maana wimbo ukiwa unaimbwa mtu unapaswa kuwa mtulivu. Sasa kitendo cha Mwamposa kudhihaki wimbk wa taifa wewe unaona sawa tu?
 
Leo nimemsikia kwa masikio yangu mawili mtume Mwamposa akiimba wimbo wa taifa kanisani kwake Kawe, jijini Dar es Salaam.

Tukumbuke wimbo wa taifa ni moja ya nembo na alama za taifa. Wimbo huu unaimbwa nyakati maalumu, kwa mfano kabla ya Rais kulihutubia taifa na wakati timu ya taifa inawakilisha nchi kwenye michuano ya kima
taifa.

Sasa Mwamposa yeye ni nani hadi adhalilishe wimbo wa taifa mbele ya waumini wake? Je, yeye ni Rais au anataka kumpindua Rais aichukue hii nchi?

Mficha ugonjwa kifo humuumbua. Kama tukiendelea kuacha nembo za taifa kuchezewa, ipo siku Mwamposa na misukule yake watachambia benders ya taifa. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwadhibiti wahuni wanaochezea nembo za taifa. Kama BoT imechukua batua kulinda udhalilishaji wa noti, serikali ya mama Samia inashindwa nini kiwadhibiti wahuni hawa wanaodharaulisha wimbo wa taifa?

MAONI YANGU
Rais anawakilisha nchi na timu ya taifa inawakilisha nchi. Mwamposa anawakilisha tumbo lake. Serikali inapaswa kumchukulia hatua huyu bwana kwa dharau aliyoionyesha kusigina wimbo wa taifa mbele ya misukule yake. Hakuna haja ya kuogopa kumuadhibu Mwamposa kwa kisingizio cha kuwakasirisha wapiga kura. Nafahamu kwamba misukule wa Mwamposa ndiyo wapiga kura wakubwa wa CCM Lakini lazima serikali ichukue hatua kukomesha uhuni huu. Ukimchekea mbwa, ipo siku atakufuata hadi msikitini.

Nawasilisha.​
Umeandika kwa chuki na lugha chafu ,na ww nenda ukaimbe na magaidi wenzio
 
Mkuu ugaidi wangu uko wapi? Wewe unafurahia wimbo wa taifa kutumiwa kama pambio kanisani? Kuwa na adabu na tunu za taifa mkuu.
 
Umeandika kwa chuki na lugha chafu ,na ww nenda ukaimbe na magaidi wenzio
Yaani watu wanaimba wimbo wa taifa huku wakicheza kanisani wewe unaona sawa tu? Yakhe huna khaya?
 
Kwa hiyo wimbo wa taifa kutumiwa kama pambio kanisani wewe unaona sawa tu? Acha dharau mkuu.
shida ni kwamba unaweka hisia binafsi na namna dini/dhehebu lako inafanya
mimi siamini kwenye Mungu
ila naamini kwenye kumfanyia mwenzako vile wewe ungependa kufanyiwa

yeye kaimba kanisani kwake,walioimba hajawalazimisha ni free will sasa mkuu ni nini hapo kinachokukwaza kama si personal feelings?
 
Leo nimemsikia kwa masikio yangu mawili mtume Mwamposa akiimba wimbo wa taifa kanisani kwake Kawe, jijini Dar es Salaam.

Tukumbuke wimbo wa taifa ni moja ya nembo na alama za taifa. Wimbo huu unaimbwa nyakati maalumu, kwa mfano kabla ya Rais kulihutubia taifa na wakati timu ya taifa inawakilisha nchi kwenye michuano ya kima
taifa.

Sasa Mwamposa yeye ni nani hadi adhalilishe wimbo wa taifa mbele ya waumini wake? Je, yeye ni Rais au anataka kumpindua Rais aichukue hii nchi?

Mficha ugonjwa kifo humuumbua. Kama tukiendelea kuacha nembo za taifa kuchezewa, ipo siku Mwamposa na misukule yake watachambia benders ya taifa. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwadhibiti wahuni wanaochezea nembo za taifa. Kama BoT imechukua batua kulinda udhalilishaji wa noti, serikali ya mama Samia inashindwa nini kiwadhibiti wahuni hawa wanaodharaulisha wimbo wa taifa?

MAONI YANGU
Rais anawakilisha nchi na timu ya taifa inawakilisha nchi. Mwamposa anawakilisha tumbo lake. Serikali inapaswa kumchukulia hatua huyu bwana kwa dharau aliyoionyesha kusigina wimbo wa taifa mbele ya misukule yake. Hakuna haja ya kuogopa kumuadhibu Mwamposa kwa kisingizio cha kuwakasirisha wapiga kura. Nafahamu kwamba misukule wa Mwamposa ndiyo wapiga kura wakubwa wa CCM Lakini lazima serikali ichukue hatua kukomesha uhuni huu. Ukimchekea mbwa, ipo siku atakufuata hadi msikitini.

Nawasilisha.​

1. NI RAIA WA NCHI GANI?
2. ANAIMBA WIMBO WA TAIFA GANI?
3.WIMBO UNA MANENO GANI?

Maana vijana wengi siku hizi hamna akili huwa mnakurupuka tu kama mabwabwa.
 
Wimbo wa Taifa unaimbwa hadi na vikundi vya wezi na wauaji... Mwacheni Mtume
 
1. NI RAIA WA NCHI GANI?
2. ANAIMBA WIMBO WA TAIFA GANI?
3.WIMBO UNA MANENO GANI?

Maana vijana wengi siku hizi hamna akili huwa mnakurupuka tu kama mabwabwa.
Wimbo wa taifa unaimbwa mahali gani na unaimbwaje mkuu?
 
Acheni chuki za kidini kuku nyinyi wimbo wa taifa ni baraka zaidi kuuimba kanisani kuliko hata huko mnakotaka uimbwe
 
Leo nimemsikia kwa masikio yangu mawili mtume Mwamposa akiimba wimbo wa taifa kanisani kwake Kawe, jijini Dar es Salaam.

Tukumbuke wimbo wa taifa ni moja ya nembo na alama za taifa. Wimbo huu unaimbwa nyakati maalumu, kwa mfano kabla ya Rais kulihutubia taifa na wakati timu ya taifa inawakilisha nchi kwenye michuano ya kima
taifa.

Sasa Mwamposa yeye ni nani hadi adhalilishe wimbo wa taifa mbele ya waumini wake? Je, yeye ni Rais au anataka kumpindua Rais aichukue hii nchi?

Mficha ugonjwa kifo humuumbua. Kama tukiendelea kuacha nembo za taifa kuchezewa, ipo siku Mwamposa na misukule yake watachambia benders ya taifa. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwadhibiti wahuni wanaochezea nembo za taifa. Kama BoT imechukua batua kulinda udhalilishaji wa noti, serikali ya mama Samia inashindwa nini kiwadhibiti wahuni hawa wanaodharaulisha wimbo wa taifa?

MAONI YANGU
Rais anawakilisha nchi na timu ya taifa inawakilisha nchi. Mwamposa anawakilisha tumbo lake. Serikali inapaswa kumchukulia hatua huyu bwana kwa dharau aliyoionyesha kusigina wimbo wa taifa mbele ya misukule yake. Hakuna haja ya kuogopa kumuadhibu Mwamposa kwa kisingizio cha kuwakasirisha wapiga kura. Nafahamu kwamba misukule wa Mwamposa ndiyo wapiga kura wakubwa wa CCM Lakini lazima serikali ichukue hatua kukomesha uhuni huu. Ukimchekea mbwa, ipo siku atakufuata hadi msikitini.

Nawasilisha.​
Majini yako yana hasira na Mwamposa, unafananishaje kuimba wimbo wa taifa na kuchambia bendera ya taifa? Kati ya Mwamposa na wewe nani anadhalilisha tunu za Taifa?
Shuleni unaimbwa kila siku na hawajachambia bendera ya taifa hadi leo.
Acha chuki wewe kakobe kwa vile waumini wako wamehamia kawe.
 
Naomba nijifunze bro, lengo la kuimba Wimbo wa Taifa Makanisani ni nini?

Kwa miaka yangu yote ya kuwepo Duniani na kutumika kwangu Kanisani kama mwandani(Inner Circle) sijawahi kuona tukiimba "Wimbo wa Taifa"
Huwa mnaimba bila kujua.
Huwa mnaliombea Taifa, mnaombea na viongozi. Sasa imba wimbo wa Taifa unambie Kuna tofauti gani na hayo maombi.
 
Wimbo wa taifa ni moja ya nembo na tunu za taifa. Haupaswi kufanyiwa dhihaka wala kubezwa na mtu yeyote yule. Ndio maana wimbo ukiwa unaimbwa mtu unapaswa kuwa mtulivu. Sasa kitendo cha Mwamposa kudhihaki wimbk wa taifa wewe unaona sawa tu?
Acha kuwa na ufinyu wa kufikiri, Mwamposa anawaambia waumini simameni tuimbe wimbo wa Taifa, Sasa dhihaka iko wapi?
Baada ya wimbo ànaliombea taifa na viongozi na hulalamiki kwamba anawadhihaki viongozi na taifa.
 
shida ni kwamba unaweka hisia binafsi na namna dini/dhehebu lako inafanya
mimi siamini kwenye Mungu
ila naamini kwenye kumfanyia mwenzako vile wewe ungependa kufanyiwa

yeye kaimba kanisani kwake,walioimba hajawalazimisha ni free will sasa mkuu ni nini hapo kinachokukwaza kama si personal feelings?
Wimbo wa taifa umeimbwa kama PAMBIO kanisani. Hilo ni sawa?
 
Back
Top Bottom