Je, ni sahihi Mwamposa kuimba wimbo wa taifa kanisani kwake?

Je, ni sahihi Mwamposa kuimba wimbo wa taifa kanisani kwake?

Wimbo wa taifa kwa namna nyingine ni kama sala(maombi) kwa taifa, tena ilibidi uimbwe kila asubuhi na raia wote. Ndo maana kwa zamani mashuleni ilikuwa kila asubuhi unaimbwa, sijui kwa sasa
 
Wimbo wetu wa Taifa siyo TUNU ya Taifa. Hatuna hatimiliki yake. Wenye hati miliki nayo wenye wimbo wao Afrika ya Kusini. Hivyo, unaweza kuupiga hata Bar na kwenye Disco.
Thubuuuutu! We usiwahadae wenzako halafu leo-leo wakajikuta pabaya na pengine hiyo bar na mmiliki wake wakapigwa BAN.:BatChesting:
 
Tatizo wimbo wa taifa ni nembo ya taifa. Haupaswi kuimbwa kama singeli au bongofleva na una unaimbwa kwenye matukio mbalimbali sio kila mahali na kila wakati. Umeelewa mkuu?
Mkuu unajua nembo ta Taifa
 
Wimbo wa taifa unaimbika popote wakati wowote. Na huo ndiyo uzalendo. Kama anaimba kanisani kqbla yq lbada ni jambo jema mnoo. Utaifa kwanza.
 
Hata ww unaweza nyumbani kwako asubhi kabla ya kwenda job.

Hiyo ni kama sala tu yakuombea nchi nothing special
Mkuu, hiyo Ni special kama ilivyo kwa sala nyingine i.e. unamtanguliza Mungu katika shughuli zako. e.g. Shule za msingi nyingi hapa Tz, huianza siku kwa kuimba wimbo huo kila siku asubuhi kabla ya kuingia madarasani kuanza masomo.:COGGERS:
 
Leo nimemsikia kwa masikio yangu mawili mtume Mwamposa akiimna wimbo wa taifa kanisani kwake Kawe, jijini Dar es Salaam.

Tukumbuke wimbo wa taifa ni moja ya nembo na alama za taifa. Wimbo huu unaimbwa nyakati maalumu, kwa mfano kabla ya Rais kulihutubia taifa na wakati timu ya taifa inawakilisha nchi kwenye michuano ya kima
taifa.

Sasa Mwamposa yeye ni nani hadi adhalilishe wimbo wa taifa mbele ya waumini wake? Je, yeye ni Rais au anataka kumpindua Rais aichukue hii nchi?

Mficha ugonjwa kifo humuumbua. Kama tukiendelea kuacha nembo za taifa kuchezewa, ipo siku Mwamposa na misukule yake watachambia benders ya taifa. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwadhibiti wahuni wanaochezea nembo za taifa. Kama BoT imechukua batua kulinda udhalilishaji wa noti, serikali ya mama Samia inashindwa nini kiwadhibiti wahuni hawa wanaodharaulisha wimbo wa taifa?

MAONI YANGU
Rais anawakilisha nchi na timu ya taifa inawakilisha nchi. Mwamposa anawakilisha tumbo lake. Serikali inapaswa kumchukulia hatua huyu bwana kwa dharau aliyoionyesha kusigina wimbo wa taifa mbele ya misukule yake. Hakuna haja ya kuogopa kumuadhibu Mwamposa kwa kisingizio cha kuwakasirisha wapiga kura. Nafahamu kwamba misukule wa Mwamposa ndiyo wapiga kura wakubwa wa CCM Lakini lazima serikali ichukue hatua kukomesha uhuni huu. Ukimchekea mbwa, ipo siku atakufuata hadi msikitini.

Nawasilisha.
Sijui kama ipo sheria inayoelekeza matumizi ya wimbo wa taifa.
Mashule mengi wanafunzi wanaimba wimbo wa taifa kabla ya kuingia darasani.
 
Wewe ulikuwa unamsikiliza ukiwa kama nan!?
Hoja ya misukule iliingiaje!?
Ndio maana nimekwambia
Mbona tumeuimba sana tukiwa mashuleni huko??
Mkuu kuimba wimbo wa taifa ukiwa shuleni sio tatizo kwa kuwa ni mahali sahihi naunaimbwa kwa kufuata utaraibu uliowekwa. Mtu huwezi kwenda kuimba wimbo wa taifa kanisani kwenye mapambio kwani huu si wimbo wa singeli bali ni mojawapo ya nembo za taifa. Umenielewa?
 
Kwani wimbo huo unaimbwa ovyo ovyo na kila mtanzania? Unapaswa urudi shule ukasome vizuri somo la uraia.
Kwani kanisani kwa Mwamposa waliimba ovyo ovyo? Umetumia vigezo gani na kuona wameimba ovyo ovyo?
 
Leo nimemsikia kwa masikio yangu mawili mtume Mwamposa akiimna wimbo wa taifa kanisani kwake Kawe, jijini Dar es Salaam.

Tukumbuke wimbo wa taifa ni moja ya nembo na alama za taifa. Wimbo huu unaimbwa nyakati maalumu, kwa mfano kabla ya Rais kulihutubia taifa na wakati timu ya taifa inawakilisha nchi kwenye michuano ya kima
taifa.

Sasa Mwamposa yeye ni nani hadi adhalilishe wimbo wa taifa mbele ya waumini wake? Je, yeye ni Rais au anataka kumpindua Rais aichukue hii nchi?

Mficha ugonjwa kifo humuumbua. Kama tukiendelea kuacha nembo za taifa kuchezewa, ipo siku Mwamposa na misukule yake watachambia benders ya taifa. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwadhibiti wahuni wanaochezea nembo za taifa. Kama BoT imechukua batua kulinda udhalilishaji wa noti, serikali ya mama Samia inashindwa nini kiwadhibiti wahuni hawa wanaodharaulisha wimbo wa taifa?

MAONI YANGU
Rais anawakilisha nchi na timu ya taifa inawakilisha nchi. Mwamposa anawakilisha tumbo lake. Serikali inapaswa kumchukulia hatua huyu bwana kwa dharau aliyoionyesha kusigina wimbo wa taifa mbele ya misukule yake. Hakuna haja ya kuogopa kumuadhibu Mwamposa kwa kisingizio cha kuwakasirisha wapiga kura. Nafahamu kwamba misukule wa Mwamposa ndiyo wapiga kura wakubwa wa CCM Lakini lazima serikali ichukue hatua kukomesha uhuni huu. Ukimchekea mbwa, ipo siku atakufuata hadi msikitini.

Nawasilisha.
Mkuu TPaul inaonyesha umepata fursa ya kuyatoa machungu yaliyokujaa moyoni mwako dhidi ya mtumishi Mwamposa kupitia kuimba kwake wimbo wa taifa akiwa ibadani. Ndiyo! Wimbo wa taifa ni mojawapo ya nembo za taifa, lakini huweza kuimbwa kwa heshima mahali popote pale kuendana na mazingira ya wakati huo yanavyohitaji matumizi yake.

Sidhani wimbo huo uliimbwa tu kama nyimbo nyingine za kusifu na kuabudu akiwa ibadani, bali ni lazima yalitokea mazimgira fulani ambayo yalichochea ukaimbwa katika eneo hilo la ibada na kwa wakati huo. Na pia kama amekiuka sheria, basi ni vyema ukaainisha ni kifungu kipi cha sheria amekwenda kinyume chake ili haki yote iweze kutendeka dhidi yake.

"Mungu ibariki Tanzania , wabariki viongozi wake, uwabariki watu wake,...." Je! Hizi baraka huwa zinaombwa wapi na zipatikana katika maeneo yapi maalum kama siyo ndani ya nyumba za ibada!? Je! Waongoza ibada ni akina nani, Mwamposa si mmoja wao!? na pia Je! Hao uliowakashifu kwa kuwaita "misukule" si miongoni mwa kundi la waumini wake!?
 
Rais anawakilisha nchi na timu ya taifa inawakilisha nchi. Mwamposa anawakilisha tumbo lake. Serikali inapaswa kumchukulia hatua huyu bwana kwa dharau aliyoionyesha kusigina wimbo wa taifa mbele ya misukule yake.
Mkuu! umesema misukule yake? Na umeemdelea kuwa na amani moyoni mwako?

Halafu usikute anayekwenda hapo na ndugu zako ktk Imani ni wengi tu

Lakini siku zote mtu mwenye afya njema, mwenye kuweza kufanya lolote kwa sababu ya afya yake kwa maana ya Kiburi cha uzima hawa watu Huwa kama vipofu

Apatwe na lolote Sasa, hatauliza na hatasema ilikuwaje nikaenda kuombewa kwa mwamposa
 
Nyie mnaona ni sahihi mtume wenu kudhalilisha nembo ya taifa? Imba wimbo wa taifa hadharani kama hujakamatwa na kutiwa ndani.
Sio kweli. Tena ujue kwamba Wimbo wa Taifa sio nembo ya Taifa. wewe Huionagi nembo ya Taifa kwenye Barua au Nyaraka zote rasmi za Kiserikali?
1711892248460.png
 
Tatizo wimbo wa taifa ni nembo ya taifa. Haupaswi kuimbwa kama singeli au bongofleva na una unaimbwa kwenye matukio mbalimbali sio kila mahali na kila wakati. Umeelewa mkuu?
Acha mawazo mfu hayo,yaani hii police state umekutia woga mkubwa sana
 
Ndio maana nimekwambia

Mkuu kuimba wimbo wa taifa ukiwa shuleni sio tatizo kwa kuwa ni mahali sahihi naunaimbwa kwa kufuata utaraibu uliowekwa. Mtu huwezi kwenda kuimba wimbo wa taifa kanisani kwenye mapambio kwani huu si wimbo wa singeli bali ni mojawapo ya nembo za taifa. Umenielewa?
We bhana, si umeulizwa hapo juu kwamba je, unaifahamu nembo ya Taifa? Ww Ukapiga kimya.
 
Wimbo wa taifa, bendera, na nembo zingine zote za taifa inapaswa ziimbwe/kutumika mahali popote pale bila vikwazo. Ni ujinga kubania watu kutumia nembo zao za taifa ndo maana watu wanajaza bendera za USA na Israel kila Kona sababu wajinga wachache wanadhani nembo za taifa ni zao peke yako.
 
Back
Top Bottom