Je, ni sahihi Mwamposa kuimba wimbo wa taifa kanisani kwake?

Je, ni sahihi Mwamposa kuimba wimbo wa taifa kanisani kwake?

Leo nimemsikia kwa masikio yangu mawili mtume Mwamposa akiimna wimbo wa taifa kanisani kwake Kawe, jijini zdar es Salaam.

Tukumbuke wimbo wa taifa ni moja ya nembo na alama za taifa. Wimbo huu unaimbwa nyakati maalumu, kwa mfano kabla ya Rais kulihutubia taifa na wakati timu ya taifa inawakilisha nchi kwenye michuano ya kima
taifa.

Sasa Mwamposa yeye ni nani hadi adhalilishe wimbo wa taifa mbele ya waumini wake? Je, yeye ni Rais au anataka kumpindua Rais aichukue hii nchi?

Mficha ugonjwa kifo humuumbua. Kama tukiendelea kuacha nembo za taifa kuchezewa, ipo siku Mwamposa na misukule yake watachambia benders ya taifa. Serikali inapaswa kuchukua hatua kuwadhibiti wahuni wanaochezea nembo za taifa. Kama BoT imechukua batua kulinda udhalilishaji wa noti, serikali ya mama Samia inashindwa nini kiwadhibiti wahuni hawa wanaodharaulisha wimbo wa taifa?

MAONI YANGU
Rais anawakilisha nchi na timu ya taifa inawakilisha nchi. Mwamposa anawakilisha tumbo lake. Serikali inapaswa kumchukulia hatua huyu bwana kwa dharau aliyoionyesha kusigina wimbo wa taifa mbele ya misukule yake. Hakuna haja ya kuogopa kumuadhibu Mwamposa kwa kisingizio cha kuwakasirisha wapiga kura. Nafahamu kwamba misukule wa Mwamposa ndiyo wapiga kura wakubwa wa CCM Lakini lazima serikali ichukue hatua kukomesha uhuni huu. Ukimchekea mbwa, ipo siku atakufuata hadi msikitini.

Nawasilisha.
Unaweza imbwa kokote kule muhimu ni kufuata taratibu hasa kutulia wakati unaimbwa,
 
Hapa n wimbo tu kaimba unatokwa povu mkuu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],akichambia hyo benderaaa SI utatokwa damuu[emoji23][emoji23][emoji23]

Mwache mtume aendele kuwaburuza watu wake usimwaribie ulaji wakee bhanaa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapa n wimbo tu kaimba unatokwa povu mkuu [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],akichambia hyo benderaaa SI utatokwa damuu[emoji23][emoji23][emoji23]

Mwache mtume aendele kuwaburuza watu wake usimwaribie ulaji wakee bhanaa [emoji23][emoji23][emoji23]
Sijamzuia kuwakanua misukule wake lakini akome kuchezea wimbo wa taifa
 
🤣🤣🤣labda mtumeeh wenu anakaribia kupewa uenezi,manake Jimbo liko wazi,anapractice protocal
 
Uko sahihi wimbo wa taifa unaimbwa ktk matukio muhimu tu ya kiserikal pia ktk taasisi kama shule chuo na kadhalika
 
Bongo zozo ulishawahi kumuona anapeperusha bendera ya taifa akiwa nyumbn kwake tu bali huwa anafanya hivyo kama kuna tukio la kitaifa kama vile timu ya taifa inacheza
 
🤣🤣🤣labda mtumeeh wenu anakaribia kupewa uenezi,manake Jimbo liko wazi,anapractice protocal
Yawezekana kabisa; sio kwa utetezi huo wanaomtetea. Yaani mtu anachezea alama ya taifa badala akemewe, misukule yake inakuja hapa kumpa bichwa? Inaudhi sana.
 
Back
Top Bottom