Je, ni sahihi vijana kutumia simu na kompyuta kujisomea kuliko kutumia vitabu?

Je, ni sahihi vijana kutumia simu na kompyuta kujisomea kuliko kutumia vitabu?

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
2,268
Reaction score
7,119
Vijana wa siku hizi hawasomi vitabu kabisa.

Unakuta kijana iwe chuoni au sekondari anatumia simu kutafuta material na anaona sawa.

Vijana wengi wananiambia wanajisomea nyumbani kwa kutumia simu. Wanagugo ili kupata material wanayotaka.

Je, simu na kompyuta zinadumaza akili?
 
Siku hizi vyuo serious utakuta vitabu vya library vipo katika electronic form ili watoto wavipate katika simu zao za mkononi
 
Kama mimi hapa, karibia kila kitu najisomea kwenye laptop. Iwe ni notes au past papers
Pia ni rahisi kutafuta video za ma lecturer wa Kihindi wakiwa wanasolve maswali ya Mechanical pale, ubongo wangu unajaa haswaa
Plus material niliyofundishwa venue, uunganishe na notes, uunganishe na malecturer wa YouTube naona mambo yanakuwa mepesi. Sio kama Advance bila kitabu husomi, mimi ni mvivu wa kufunua karatasi. Bora nisome hivihivi kwenye laptop
 
Vitabu labda kama ni hobby tu na upo karibu na library ya vitabu..

Ila kama uko mbali na library ni vyema kuea na kindle ambayo ni kama tablet ya usomaji.

Mimi nikiwa karibu na library huea nakusanya hata vitabu vinne nasoma kama nascroll instagram yaani naangalia heading inayonivutia naisoma na isiyonivutia naachana nayo..

So kama mtu yuko karibu na vitabu bora asomee vitabu, kama yuko mbali na vitabu ni vyema akatumia electronic device kusomea cha muhimu maarifa yapatikane
 
Siku hizi vyuo serious utakuta vitabu vya library vipo katika electronic form ili watoto wavipate katika simu zao za mkononi
Tofautisha kitabu soft copy na kutumia mtadao kupata material
 
Vitabu labda kama ni hobby tu na upo karibu na library ya vitabu..

Ila kama uko mbali na library ni vyema kuea na kindle ambayo ni kama tablet ya usomaji.

Mimi nikiwa karibu na library huea nakusanya hata vitabu vinne nasoma kama nascroll instagram yaani naangalia heading inayonivutia naisoma na isiyonivutia naachana nayo..

So kama mtu yuko karibu na vitabu bora asomee vitabu, kama yuko mbali na vitabu ni vyema akatumia electronic device kusomea cha muhimu maarifa yapatikane
Umenipata vizuri.? Mfano mwanafunzi anaulizwa nini maana ya ekolojia? Haendi kutafuta kitabu kinachohusu ekolojia. Anaigia google anatafuta jibu? Ni sahihi?
 
Mbona unaongea as if kuna ubaya watu kupata material mtandaoni Heri yao wanatumia mtandao kwa manufaa, sio kulike picha za makalio 24/7
Kuna hoja zinaibuka kuwa mitandao inadumaza akili. Vitabu ni bora kuliko mitandao. Swali langu lipo hapo
 
Kuna hoja zinaibuka kuwa mitandao inadumaza akili. Vitabu ni bora kuliko mitandao. Swali langu lipo hapo
Anhaa hapo sasa nimekuelewa
Watu wanaposema mitandao inadumaza akili ni kwa sababu watu wengi wanatumia mitandao kuangalia picha za makalio, kuscroll vichekesho muda wote, kufuatilia umbea nk. Sio vibaya lakini ukizidisha haya mambo ni kweli yanadumaza akili
Lakini wanaotumia mitandao kutafuta materials kwa lengo la kupata maarifa, hawadumazi akili

Wanaodumaza akili ni wale wanaotegemea AI kufanya assignment zao kwa 100%
 
Karibu kila kitabu ulichosoma chuo miaka hiyo uliyosoma kipo mtandaoni kwa muundo wa soft copy.
Kitabu siyo lazima kuwa ktk muundo wa hardcopy, au printback.
Vile ambavyo publishing company haija zakisha soft copy ku a watu wake scan au wameoiga picha kurasa zote na kuweka mitandaoni.
University nyingi hata Tanzania waalimu/wahahii wanatengeneza soft copy ya notice za tutorials zao. Kisha wanapakia mtandaoni au wanasambaza kwa wanafunzi ambao huzitunza kwenye simu au kwenye computer, au online ktk cloud storage mfano Google drive.
 
Umenipata vizuri.? Mfano mwanafunzi anaulizwa nini maana ya ekolojia? Haendi kutafuta kitabu kinachohusu ekolojia. Anaigia google anatafuta jibu? Ni sahihi?
Kwa mtu ambaye hana interest na kusoma na kujua vitu kwa undani nadhani usomaji huo sio sahihi..

Kama mtu ambaye ana interest ya kujus vitu kea undani basi ni vyema akatafuta vitsbu husika ili apate ile deep knowledge inayoweza kumsaidia kwenye mambo mengine pia.

Usomaji wa aina hiyo uliyouliza ndio unaweza kuwatofautisha watu kutoka kwenye ukawaida na watu smbao tunaweza kusema ni genious.

Ukijua vitu kwa undani unaweza kuconnect dots mbalimbali na ukaja na kitu chako kipya watu wakaona jamaa niaje huyu mchawi nini, kumbe ni kuconnect dots tu.

Swali kwako..

Je kama elimu ya vitabuni wanaweza kuipata kwenye electronics kama ilivyo unaonaje hapo?
 
Kiafya probably not unless unatumia ebook reader; Kiu-halisia imesaidia unadhani wangapi wangekuwa na uwezo wa kupata materials au vitabu version za karibuni...

Kuna watu wamejikuta wanasomea vitabu vya version ya kwanza badala ya recent (edition hata ya 20); Nakumbuka likitabu la University Physics huko shule sijui walipewa msaada na watu gani likitabu hata lilikuwa hata halina metric system bado ni mwendo wa ft, ounces na pounds
 
Kusoma kwenye simu au computer ni Bora zaidi kuliko kwenye kitabu Kwa sababu utaona na video ambazo zinafafanua zaidi unachosoma na kukifahamu kiundani
 
Back
Top Bottom