Je, ni sahihi Watoto wadogo (under 18) kusoma Biblia bila uangalizi wa Mwalimu wa dini?

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Salaam Wakuu,

Watu wazima miaka 60 biblia bado hawaielewi, vipi watoto wadogo?

Je, Biblia inaweza kuwwjenga watoto au kuwabomoa?

Watoto wadogo wasome mambo Ufunuo, Walawi, Waamuzi, Ruth Samweli, Wimbo ulio bora nk.

Kwa upande wangu naona si sahihi watoto kuachiwa Biblia wajisomee bila Msimamizi.

Hata sisi Kanisani hatujisomei, tunapangiwa somo la kusoma kila jumapili na mtu wa kutuelezea maana yya somo hilo. Na bado tunattoka kapa

Vipi kwa watoto wadogo?

Nahisi ni njama za Wazungu kupandikiza umasikini kwa Mwafrika
 
Ni kuwaharibia akili mapema. Mnawazidisha uzwazwa wa kukariri visa na ngano za wengine tena wasio wahusu. Sijui nani alituroga Waafrika.
 
Sasa bible inashida gani!! . Na lini under 18 ni matajiri hapa Africa ?? 😀😀😀
Hakuna niliposema ina shida. Nimeuliza kama ni sahihi mtoto mdogo kujisomea Biblia bila Uangalizi?

Mfano mtoto wako anaweza kuelewa huu mstari?

na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na likiwapo neno lo lote linginelo lisilopatana na mafundisho yenye uzima; kama vile ilivyonenwa katika Habari Njema ya utukufu wa Mungu ahimidiwaye, niliyowekewa amana.
 
watoto wa kizazi hichi unawachukuliaje mkuu,mbona wana uelewa kushinda hata wewe mtu mzima
 
Muache asome ili ajue, kuhusu mambo mabaya na mazuri... Unataka ajifunze wapi kuhusu mambo mabaya yaliyopo duniani.??
 
unaposema watoto kusoma Biblia bila msimamizi ni kama kitabu kitakatifu hakiwafai watoto kina mambo ya kikubwa ,sema hivi wanasoma biblia bila kuongozwa.

sasa si unaweza anza wewe kuwasaidia watoto wako mimi nafanya hivyo kuna siku ya biblia lazima wasikie story za kwenye Biblia wanapenda wenyewe lakin wanajifunza maadili
 
unaposema watoto kusoma Biblia bila msimamizi ni kama kitabu kitakatifu hakiwafai watoto kina mambo ya kikubwa ,sema hivi wanasoma biblia bila kuongozwa.

sasa si unaweza anza wewe kuwasaidia watoto wako mimi nafanya hivyo kuna siku ya biblia lazima wasikie story za kwenye Biblia wanapenda wenyewe lakin wanajifunza maadili
 
kwanini unahisihisi tu mara ni njama za wazungu kututfanya tuwe masikini,

wewe kama wewe umeamini aslimia 100 kuwa ni mpango wa sisi kuwa masikini?
 
Lengo la dini Africa ni kuzuia mageuzi na ukuaji wa Technology and science
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…