Je, ni Salama kuzima friji kwa siku kadhaa kama halitumiki?

Je, ni Salama kuzima friji kwa siku kadhaa kama halitumiki?

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Wakuu habari

Nauliza je kama situmii friji ni salama kuzima? Mfano limeisha vitu au nasafiri nikalizimaa wiki au mbili

Maana kuna ambayo yanazimwa kisha baadaye yanakuwa yameharibika
 
Wakuu habari

Nauliza je kama situmii friji ni salama kuzima? Mfano limeisha vitu au nasafiri nikalizimaa wiki au mbili

Maana kuna ambayo yanazimwa kisha baadaye yanakuwa yameharibika
Inaonekana wewe ni mgeni wa matumizi ya friji kama mimi acha nikae mkao wa kujifunza.
 
Mtu atupe uzoefu wa mafriji ya mtumba pia , ubora wake na matumizi ya umeme yako salama wadau ?
 
Wakuu habari

Nauliza je kama situmii friji ni salama kuzima? Mfano limeisha vitu au nasafiri nikalizimaa wiki au mbili

Maana kuna ambayo yanazimwa kisha baadaye yanakuwa yameharibika

Kwani TV huwa unaiacha inawaka mda wote hata kama haupo?
 
Wakuu habari

Nauliza je kama situmii friji ni salama kuzima? Mfano limeisha vitu au nasafiri nikalizimaa wiki au mbili

Maana kuna ambayo yanazimwa kisha baadaye yanakuwa yameharibika
Watu wanaona friji limeharibika pale ukungu unapoota ndani kwani walizima friji bila kukausha vizuri ndani ya friji. Safisha na kukausha friji vizuri kabla ya kulizima.
 
Wataalamu wanashauri kulitumia jokofu na kulizima kwa week 1, 2 au miezi kadhaa na kuliwasha tena si salama. Na usalama unaoongelewa hapo ni wa kiafya, si wa kiufundi. Jokofu linapozimwa kwa muda mrefu ni rahisi kuota fangasi, bacteria au vijidudu vingine ambavyo ni hatari kwa binadamu. Hata harufu yake huwa ni mbaya (kwa wazungu lakini.......am kidding). Lakini hakuna tatizo la kiufundi. Mfumo wake wa kupooza utafanya kazi kama kawaida yake.
Nina jokofu moja ambalo lina function ya 'Holiday'. Hii function unatumia wakati umesafiri kwa week au miezi kadhaa. Unatoa kilakitu, unaweka 'Holiday', unafunga nyumba yako unaondoka. Jokofu inakuwa haipozi ila nadhani inaruhusu mzunguko wa hewa ili kutoruhusu vijidudu kuzaliana ndani ya jokofu na kuleta ile harufu.
 
Nilihamia kwangu kukiwa hamna Umeme. Friji cum Freezer likawa Off miezi Saba. Lipo poa sasa
 
Back
Top Bottom