Je, ni Salama kuzima friji kwa siku kadhaa kama halitumiki?

Je, ni Salama kuzima friji kwa siku kadhaa kama halitumiki?

Mi sijawahi zima, Ila nadhani halina shida ukizima unapotaka kulitumia tena lisafishwe vizuri vinega na bicarbonate of soda then likaushwe vizuri salama kwa matumizi.

Lakini pia si salama vyakula kuwepo ndani ya fridge na fridge likuwa limezimwa.
 
Wakuu habari

Nauliza je kama situmii friji ni salama kuzima? Mfano limeisha vitu au nasafiri nikalizimaa wiki au mbili

Maana kuna ambayo yanazimwa kisha baadaye yanakuwa yameharibika
Sasa unazima friji ambalo matumizi yake ni unit 276 per annum! Afu unahonga elfu 50!
 
Sisi tunaotumia mitungi tunaweka wapi comments zetu?
 
Wataalamu wanashauri kulitumia jokofu na kulizima kwa week 1, 2 au miezi kadhaa na kuliwasha tena si salama. Na usalama unaoongelewa hapo ni wa kiafya, si wa kiufundi. Jokofu linapozimwa kwa muda mrefu ni rahisi kuota fangasi, bacteria au vijidudu vingine ambavyo ni hatari kwa binadamu. Hata harufu yake huwa ni mbaya (kwa wazungu lakini.......am kidding). Lakini hakuna tatizo la kiufundi. Mfumo wake wa kupooza utafanya kazi kama kawaida yake.
Nina jokofu moja ambalo lina function ya 'Holiday'. Hii function unatumia wakati umesafiri kwa week au miezi kadhaa. Unatoa kilakitu, unaweka 'Holiday', unafunga nyumba yako unaondoka. Jokofu inakuwa haipozi ila nadhani inaruhusu mzunguko wa hewa ili kutoruhusu vijidudu kuzaliana ndani ya jokofu na kuleta ile harufu.
Naomba jina/model/brand ya hiyo friji.
 
Mimi huwa kwa masaa 24 naliwasha masaa 12 kila siku na ninalizima masaa 12.. huu mwaka wa 1.5 na liko poa tu
 
Unazima vizuri tu..haina shida

Anavyouliza utafikiri alilinunua dukani likiwa linawaka...

Ni ukizima mda mrefu friji huwa linatengeneza ka-harufu flani hivi endapo hukusafisha vizuri,,,,Otherwise hakuna tatizo lolote, Mleta uzi stori za vijiwe vya pweza zinamchanganya
 
Wakuu habari

Nauliza je kama situmii friji ni salama kuzima? Mfano limeisha vitu au nasafiri nikalizimaa wiki au mbili

Maana kuna ambayo yanazimwa kisha baadaye yanakuwa yameharibika
Wakati unalinunua huko dukani ulikuta limewashwa?
 
Niko Happ kusubiri majibu mnk juz nimewasha friji Tena jipya kbsa la hensens. Niliweka soda na maji kujaribu ufanisi na uwezo usku ilipotimia nililizima mm sijuu itakuwa nimearibu friji ya watu
 
Mimi Nina freezer langu nililizima kwa miezi 3 baada ya kurudi nimelikuta halina tatizo kabsa
 
Naomba jina/model/brand ya hiyo friji.
DSC_0349.JPG

Brand ni 'Haier'. Ni ya mtumba nilichukua K/koo. Nadhani hiyo sticker kushoto ina model number na taarifa nyingine.
 
Wakuu habari

Nauliza je kama situmii friji ni salama kuzima? Mfano limeisha vitu au nasafiri nikalizimaa wiki au mbili

Maana kuna ambayo yanazimwa kisha baadaye yanakuwa yameharibika
Huwa ni maneno ya kitaa tu kuwa fridge halizimwi.

Mimi ni mtumiaji wa majokofu miaka nenda rudi, sijawahi pata shida itokanayo na kulizima.

Nalizima na kuliwasha kutokana na mahitaji yangu bila kujali nakaa siku ngapi ama muda gani bila ya kuliwasha.

Isipokuwa likikaa siku nyingi bila kufanyakazi, siku ukiliwasha, linachukua muda mrefu kuanza kupoza.

Labda kama kuna sababu nyingine ya kiufundi ambayo siielewi, siwezi kuikataa.

Ni hivyo tu.
 
Kuzima usiku na kuwasha mchana...

Inasababisha kutu, barafu ikiyeyuka maji yake yanatoka nje,pale yanapotokea baadae inaanza kutu.. mwisho viraka... ..
 
Back
Top Bottom