Je, ni sawa kisheria kwa mwanamuziki kumtaja mtu au brand kwenye nyimbo yake bila ridhaa yake?

Je, ni sawa kisheria kwa mwanamuziki kumtaja mtu au brand kwenye nyimbo yake bila ridhaa yake?

Forest Hill

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2018
Posts
2,873
Reaction score
6,821
Habari zenu ndugu zangu, hii thread sio kwaajili ya kejeli au kusutana, nauliza nataka kujua kwa wenye ujuzi wa Mambo haya, je ni sawa mwanamuziki kumtaja mtu au brand fulani kwenye nyimbo yake bila ridhaa ya mtu huyo au kampuni husika?

Vipi kuhusu kuipa nyimbo jina la mtu au brand fulani? Nyimbo nyingi nazijua zimetaja au Zina "title" ya jina la mtu au kampuni fulani baadhi ya nyimbo ninazokumbuka kwa haraka ni

Rick Ross. (Elvis Presley) Elvis alikua mwanamuziki maarufu duniani, pia ndio King wa mtindo wa Rock and roll

Gosby. (Wema Sepetu)anhaa wema wengi tunamjua,

Cassper nyovest. (Tito Mboweni) wakati Cass anatoa Tito Mboweni,wakati huo bwana Tito Mboweni alikua waziri wa fedha na uchumi wa South Africa

G nako (Juma Ikangaa)Juma ikangaa ni mtanzania, mwanariadha nguli, bingwa wa mashindano ya olimpiki mwaka 1989, nakumbuka mstari wa da Hustler"ikangaaa nawakimbiza kwenye hii marathon"

Mex Cortez (Luanda Magere) Luanda Magere alikua mpiganaji na shujaa wa kabila la waluo huko Kenya.

Harmonize (Bakhressa) Bakhressa ni mfanyabiashara mkubwa Tanzania, kijana kaiita nyimbo yake Bakhressa.

Hii ipoje wadau? kutajana majina, wadhifa, cheo, utajiri, maisha binafsi kwenye nyimbo?
 
Ni sawa labda kama angelitumia kibiashara ingekuwa tatizo ila kama sifa naona ni sawa.
 
Ni sawa labda kama angelitumia kibiashara kama sifa naona ni sawa.
Hawezi kupata faida yeyote kwenye biashara zake kwa kujiita hivyo??kuongeza attention kwa mashabiki sio faida hiyo kibiashara??
 
Ni sawa tu..hata Mimi ningekua star ningewaambia wanamuziki hata was singeli wanitaje kila wimbo..😎
 
Hahaha hapo sawa shemeji,ukiwa na shida ndogo ndogo usiache kuniambia,sawa shem lake???
Hahaha kumbe ulikuwa unapima kina cha maji?
Wewe ndio ukiwa na shida ndogo ndogo na kubwa usisite kusema
 
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
emoji1787.png
hata mimi nimecheka, sio kwa utabiri huo

Hahaha kumbe ulikuwa unapima kina cha maji?
Wewe ndio ukiwa na shida ndogo ndogo na kubwa usisite kusema
Mnunulie dada yako iPhone, itel yake camera ya uwongo...
 
Back
Top Bottom