Je ni sawa kuolewa na kaka yako wa kambo?

Je ni sawa kuolewa na kaka yako wa kambo?

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
1,345
Reaction score
3,503
Nimeshirikishwa kwenye mgogoro wa kifamilia ambao wazazi waliooana wote wakiwa na watoto waliozaa kwenye mahusiano kabla ya ndoa.

Wakati wanaoana, mtoto wa kiume alikuja na mke / mama akiwa na miaka 9 na mtoto wa kike alitokea upande wa mume na alikua na miaka 4. Hawajachangia damu ila wote wamekulia kwenye nyumba moja wakilelewa kwa pamoja kama kaka na dada kwa zaidi ya miaka 20.

Wiki iliyopita wamewashtua wazazi wao kwa kuwajulisha kua wanataka kuoana na kwamba wamekua na mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya miaka miwili.

Hii issue imeleta changamoto kubwa kwenye familia na wazazi hawaafiki kabisa hao watoto/vijana kuoana.
Je, ingekua wewe, ungewashauri nini both hao watoto na wazazi?
 
Hapana, isingefaa kuoana.. lakini wameshazini,na wameweka hadharani mahusiano yao..hakuna uaminifu tena kati yao..
 
Nimeshirikishwa kwenye mgogoro wa kifamilia ambao wazazi waliooana wote wakiwa na watoto waliozaa kwenye mahusiano kabla ya ndoa.

Wakati wanaoana, mtoto wa kiume alikuja na mke / mama akiwa na miaka 9 na mtoto wa kike alitokea upande wa mume na alikua na miaka 4. Hawajachangia damu ila wote wamelelewa kwenye nyumba moja kama kaka na dada kwa zaidi ya miaka 20.

Wiki iliyopita wamewashtua wazazi wao kwa kuwajulisha kua wanataka kuoana na kwamba wamekua na mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya miaka miwili.

Hii issue imeleta changamoto kubwa kwenye familia na wazazi hawaafiki kabisa hao watoto/vijana kuoana.
Je, ingekua wewe, ungewashauri nini both hao watoto na wazazi?
Matoto ya geti kali hayo!
 
Kibaiolojia wapo sahihi kwasababu hawana undugu wa damu ni undugu wa kijamii. Ila kijamii na kimila sio sahihi sababu wazazi wao tayari wamekuwa mke na mume hivyo wao wanalazimika kuwa ni ndugu awali ya yote.
 
Wacha waoane tu.
Watu wameshadinyana hadi Kei ina Sugu sioni cha ajabu hapo.
 
Incest ni kosa kisheria lakini Incest ni pale ndugu wa damu wanapokuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Kwa case ya hao wawili hawana undugu wa damu (they are not biologically related). Ralationship yao ipo more on the sociocultural side.

So hapo inabaki tu kuwa socioculturally (kijamii na kiutamaduni) je ni sahihi na inakubalika?

Mimi naona waowane tu kuliko kuwanyima wanachotaka ikiwa hawajavunja sheria ya nchi.
 
Back
Top Bottom