Je ni sawa kuolewa na kaka yako wa kambo?

Je ni sawa kuolewa na kaka yako wa kambo?

Aliyeelewa anieleweshe.
Chukulia wewe umekutana na msichana ana mtoto kutoka kwa mwanaume mwingine ukamuoa. Ila na wewe pia ulikua tayari na mtoto kutoka kwa mwanamke mwingine kabla hamjaoana, so mkawachukua watoto wenu mliowapata nje ya ndoa mkaishi nao pamoja kama watoto wa kuwazaa. Hao watoto wamekua wakubwa, wamependana kimapenzi na sasa wanataka kuoana japo mliwalea kama kaka na dada.

Sasa wewe na mkeo hamtaki maana ni aibu na mtaonekanaje kijamii, wakati watu wote wanawajua hao kama watoto wenu wa familia.
 
Tusome maandiko yanasemaje kidogo wakuu

Walawi :18:9
Kamwe usilale na dada yako, awe ni dada yako halisi au dada yako wa kambo.

Walawi :18:11
Kamwe usilale na msichana aliyezaliwa na mama yako wa kambo aliyeolewa na baba yako; msichana huyo ni dada yako.
 
Hao watoto wamefanya maksud maana wanajua kwamba wao ni ndugu japo sio Kwa dam ila wazaz wametengeneza bond wao wakaona wafanye wanayojua wao wamefanya kusudi
 
Hawa watoto wasiochangia damu huwa wanakulana tangu wakiwa wadogo, hako ka mchezo kapo. Ila kama mmechangia mzazi mmojawapo baba au mama hapo ni ngumu kulana. Sema kuna heshima fulani inakuwepo kutokumla mtoto wa mke wa baba/mtoto wa mume wa mama
 
Nimeshirikishwa kwenye mgogoro wa kifamilia ambao wazazi waliooana wote wakiwa na watoto waliozaa kwenye mahusiano kabla ya ndoa.

Wakati wanaoana, mtoto wa kiume alikuja na mke / mama akiwa na miaka 9 na mtoto wa kike alitokea upande wa mume na alikua na miaka 4. Hawajachangia damu ila wote wamekulia kwenye nyumba moja wakilelewa kwa pamoja kama kaka na dada kwa zaidi ya miaka 20.

Wiki iliyopita wamewashtua wazazi wao kwa kuwajulisha kua wanataka kuoana na kwamba wamekua na mahusiano ya kimapenzi kwa zaidi ya miaka miwili.

Hii issue imeleta changamoto kubwa kwenye familia na wazazi hawaafiki kabisa hao watoto/vijana kuoana.
Je, ingekua wewe, ungewashauri nini both hao watoto na wazazi?
mila za kiarabu ni ruksa,sasa huku kwetu sijui
 
Kama hao wazazi hawakuzaa baada ya kuoana,I mean hao vijana hawana mdogo wao wa kuchangia ,hao wazazi watengane ili hao watoto waoane.
 
Mbona zamani hata kwenye Bible walikua wanaona.ndugu wa mbali?
 
Back
Top Bottom