Je, ni sawa kwa Rais Samia kuiunga mkono Somalia kiusalama?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2023
Posts
6,683
Reaction score
14,060
“Kama mnavyojua hali ya wenzetu [Somalia] haiko vizuri sana, kwahiyo tumewahakikishia kuwaunga mkono kwenye kujenga uwezo wa wao kama nchi kujilinda wenyewe.” – Rais Samia Suluhu

Sasa nchi yetu tumekwisha iendeleza na kuilinda vya kutosha sasa tuna vuka kwenda kuwajenga na kuwaendeleza wengine.

Ombi langu ni hili ni kuwa hiki sio kipindi cha utawala wa Nyerere na harakati za ukombozi wa Afrika.

Hii kauli sioni kama ilikuwa sahihi kutolewa na kiongozi wa ngazi ya juu ya serikali.

Kudhibiti tu wahamiaji haramu wanaouvaa uraia wa Tanzania tumeshindwa CDF kathibitisha hilo tena wengine na madaraka makubwa nchini tunawapa.

Wasomali tunao hapa nchini na wanazidi ingia kwa njia wanazo jua wenyewe, sehemu tunayotaka kukanyaga sio sahihi hata kidogo labda kama tupo tayari kwa matokeo yoyote yatakayo tupata.
 
Tunapaswa kujizatiti katika kujenga nchi yetu kuliko kujiingiza katika migogoro ya ajabu ajabu.
 
Huyo bibi hakitakiwa kuongea hi o mbele ya rais wa Somalia.
Inashangaza kiongozi anasema chochote kile kufurahisha mgeni wake pasipo kuangalia madhara ya matamshi yake.
 
Nionavyo awe anasoma tu hotuba Rasmi,

Kila akipata wasaa kuongea yake Huwa anatoa Boko!!
 
Hao ni makomandoo,,,,migambo sijui wana hali gani
 
Supporting regional peace and stability is a major tenet of Tanzania's foreign policy.

By the way, Capacity Building is a broad term with infinite possibilities. Could be military training, intelligence sharing and diplomatic support, not necessarily active military intervention, like the Kenyan debacle.​
 
Angeiunga mkono kimya kimya lakini sio kwa kutangaza kama alivyofanya
 
Kama mnavyojua hali ya wenzetu [Somalia] haiko vizuri sana, kwahiyo tumewahakikishia kuwaunga mkono kwenye kujenga uwezo wa wao kama nchi kujilinda
Hivi sa100 anaujua vizuri mziki wa mahasimu wa serikali ya Somalia, yaani al-shabaab?
Wakianza kujilipua mfululizo ndani ya Tanzania atawamudu?
 
Reactions: rr4
Taifa haliwezi fanya maamuzi y kipumbavu sababu ya person ambitions.Ifike hatua huyu mama awe muangalizi wa kauli zake.
 
Huo mkataba wa kuwa Saidia ipoje , mpaka malalamike.
 
Mambo ya Somalia bora tuachane nayo tu, Somalia hata haina umuhimu wowote wa kimkakati kwa Tanzania
 
Reactions: rr4
Taifa haliwezi fanya maamuzi y kipumbavu sababu ya person ambitions.Ifike hatua huyu mama awe muangalizi wa kauli zake.
Watu mna mihemuko ya kijinga kwamba moral support inashida gani, mbona hilo ni kauli ya kiutawala, haja saini makubaliono yoyote, acheni chuki dhidi ya Raisi wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…