Je, ni sawa kwa Wanajeshi kurekodi video kama hizi na kuzisambaza mtandaoni?

Je, ni sawa kwa Wanajeshi kurekodi video kama hizi na kuzisambaza mtandaoni?

Ila naona huyo Kuruta alikuwa bado anahitaji mafunzo zaidi, maana hayo mambo ya kwata ni sehemu ndogo sana ya mafunzo ya Jeshi
Athari za utandawazi hayo, mambo ya sirini yanawekwa wazi na ya wazi yanafanywa Siri 🙌
 
Wakuu kwema?

Nimekutana na video hii mtandaoni, ambako huyu 'kuruta' (kama sijakosea) anapewa amri ya kugeuka kulia na kushoto, kijana huyo anafata maagizo aliyopewa huku anayetoa maagizo na wengine wakisikika wakicheka.

Nini dhumuni la kurekodi video hizi mpaka kufikia hatua ya kuzirusha mtandaoni? Anayerekodiwa ameridhia? Na hii sio mara ya kwanza kukutana na video kama hizi mtandaoni, za hawa wanafunzi wanaokwenda jeshi kwa mujibu wa sheria kurekodiwa katika matukio mbalimbali.

Huu ni udhalilishaji wa utu wake, tayari watu washaanza kutoa maoni mbalimbali juu ya muonekano wake, maumbile na kadhalika, kwa hali tu ya kawaida hakuna mtu angependa kurekodiwa katika hali hiyo na video hiyo irushwe kwa kila mtu kuona.

Hii sio sawa, kwanza ukipewa amri hapo lazima ufate, usipofata ni kukaidi na udhabu unapewa. Kwanini tunahalalisha udhalilishaji huu uendelee kutokea na kuonekana na kawaida? Wanajeshi wapo juu ya Sheria? Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wao haiwahusu?

Aliyechukua video hii awajibishwe, Jeshi kama chombo cha ulinzi wanatakiwa kuwa mfano kwenye kufata sheria na sio kuwa wa kwanza kwenda kinyume na kudhalilisha utu wa watu.

Kutoka kwenye comments za video hiyo anayesikika akitoa amri ni Afande Sese, JKT Oljoro.

Sheria iwe msumeno, sio ikate kwetu tu halafu kwao kuwe butu.

Hakuna Mwanajeshi hapo

Mleta mada

Huoni kuwa ni raia huyo
 
Unaona huo ugeukaji wake

Ila naona huyo Kuruta alikuwa bado anahitaji mafunzo zaidi, maana hayo mambo ya kwata ni sehemu ndogo sana ya mafunzo ya Jeshi
Athari za utandawazi hayo, mambo ya sirini yanawekwa wazi na ya wazi yanafanywa Siri 🙌
Huyo ni raia mkuu na hata sio kuruta
 
Kasome vizuri nilichondika, sijasema namjua, nimesema kwa mujibu wa comments kutoka kwenye video hiyo mtandaoni. Mkuu, mpaka unatafuta visababu vyote hivyo kutetea hili naamini umeona kabisa kosa hili. Ingekuwa igizo tungeona kwenye official page zao, wakitaja tukio pamoja na taarifa nyingine. Kama upo kwenye kada hiyo saidia kuelimisha wenzako kuliko kutetea ujinga
Mkuu mbona umeandika hivi:
"Nimekutana na video hii mtandaoni, ambako huyu 'kuruta' (kama sijakosea) anapewa amri ya kugeuka kulia na kushoto, kijana huyo anafata maagizo aliyopewa huku anayetoa maagizo na wengine wakisikika wakicheka.

Nini dhumuni la kurekodi video hizi mpaka kufikia hatua ya kuzirusha mtandaoni?.........."

Kwa maana hiyo wewe umeamini hicho kitu ni kweli na ukachangia kukisambaza kutoka huko ulikokiona hadi ukakileta hapa kwa maGT - Jf.
Nimekuwekea visababu hivyo ili kukurudisha kwenye ukweli usiendelee kuhadaiwa.
Hapo hakuna kosa lolote kwani maigizo hufanywa na yeyote anayejisikia kufanya hivyo ( bure au kwa malipo)na wala sio lazima awe na official page.
Siwezi kusaidia jambo hewa. Wewe mwenyewe unajua jinsi ilivyo vigumu kuchukua picha ndani ya eneo la Jeshi lakini bado unaamini jambo hilo limerekodiwa Oljoro JKT.
Ni hayo tu.
 
emotional and sensitive people wanaua sana vibe kwa huu ulimwengu kila kitu wanachukulia personal
kuruta mwenyewe anaonekana ana enjoy na afande member wa internet society ana catch feelings
 
Back
Top Bottom