Je, ni sawa kwa Wanajeshi kurekodi video kama hizi na kuzisambaza mtandaoni?

Huku ndiko tulikofikia mtu kurekodiwa anafanyishwa mazoezi ni kumdhalilisha ili akirekodiwa akikata mauno nusu uchi au vigodoro ni au akifanya ngono ni sifa
Mkuu hao wa nusu uchi huwa wanajirekodi wenyewe, au hata wakirekodiwa huwa ni kwa ridhaa yao, lazima ujue kutofautisha
 
Aaaah Mkuu, usiniambie hii ndiyo video ya kwanza ya mtindo kama huu kuiona mtandaoni, msema ukweli mpenzi wa Mungu
 
Aaaah Mkuu, usiniambie hii ndiyo video ya kwanza ya mtindo kama huu kuiona mtandaoni, msema ukweli mpenzi wa Mungu
Ni kweli sijaona video ya mtindo huu; lakini hilo halinizuii kuihoji Ukweli au Uhalali wake.
 
Tanzania uhuru umezidi ,Kisheria ni kosa kumchukua mtu video bila idhini yake
 
unashaangaa kupigwq picha jeshini watu wanapigwa hadi risasi kwa hizi fasi za kijeda unaleta masuala ya civil rights kwa makamanda
Una matatizo makubwa sana kichwani kwako.
Hivi mama yako mzazi angerekodiwa video wakati alipokuwa anajifungua ujauzito wako wewe huko hospitalini alikoenda kujifungua na Kisha video hiyo ingewekwa hadharani humu mitandaoni na kuonekana dunia nzima wewe ungejisikiaje??? Je, Ungefurahia kuiona video hiyo wakati huu ukiwa umekuwa mtu mzima??
 
apo tunaongelea mafunzoni jeshini kiongozi ni kipi usichokielewa kwamba sheria zako zote unazozijua hazi apply jeshini wao wana martial laws kama unataka kufurah ingia YouTube wana chanel yao uone makuruta wanavyolia mpaka wanatoa kamas we utakua mgeni sana hapa duniani
 
Maadili ya Kutunza Siri yapo kwenye taaluma zote, Sheria za kutunza Siri zipo na zina-apply kwa watu wote, uwe katika shughuli za kiraia au kwenye kazi za kijeshi
. Na kwa bahati mbaya zaidi, kwenye Majeshi kuna Sheria Kali zaidi za Kutunza Siri za Jeshi au Siri za Nchi, hili ni takwa la lazima kwa Majeshi yote hapa duniani. Na ndio maana Wanajeshi ni LAZIMA WAAPISHWE Viapo, ikiwamo na KIAPO CHA KUTUNZA SIRI.
 
Ipo siku tutaona wagonjwa wakipasuliwa thieta au kuzalishwa mtandaoni
 
Raia nawapenda sana , hapana kosa hapo acheni kukuza mambo jaribuni kusoma vifungu vya sheria za jeshi na za kiraia ila mathalani mjue kutofautisha neno muktadha na mazingira kwa minajiri ya jeshini au kikosini na uraiani bila kusahau , sheria ya mtandao hasa upande wa jeshini iko uchi kiasi chake hivyo ukija kichwa kichwa wewe raia hautaeleweka maana sheria zenu ni huko uraiani sio jeshini .

Sijaeleweka , jambo wakuu ?? Nisiulizwe chochote niko sawa .

Note : Shemeji yenu yuko hapa naomba mtu yeyote anijibu kwa staha na kwa logic kwenye komenti yangu ili asinione kilaza maana hatuna hata mwezi ni penzi jipya.
 
Kwa hiyo hata huyo mkeo uliyenaye akienda kujifungua kwenye hospitali ya Jeshi akirekodiwa video huko wakati anajifungua mbele ya Madaktari/Wakunga Wanajeshi Wanaojifunza kazi na kisha video yake ikiwekwa mitandaoni ni sawa tu eti kwa sababu yuko katika Hospitali ya Jeshi inayozingatia Sheria za Jeshi????? Au unamaanisha nini??
 
Huku ndiko tulikofikia mtu kurekodiwa anafanyishwa mazoezi ni kumdhalilisha ili akirekodiwa akikata mauno nusu uchi au vigodoro ni au akifanya ngono ni sifa
Ebu soma ulichoandika na ukitafakari , upo timamu kwel ?
 
Hakuna Kosa hapo..
Hakuna Mtu anayejua Lengo la mchukuaji Video zaidi ya mchukuaji mwenyewe..

HIsia za Muonaji Sio hisia za mchukuaji..
Kwahyo Hakuna kosa hata kidogo..

Kisheria Na wala Ethically labda kama una Mada nyingine
halaf ww ndo unakuja kuwa kiongoz baadae , hahaa waafrika mpk tustaraabike ndo tutapata viongoz bora , yaan kwa akili yako unahisi hatokuja kuwa na familia baadae ? je watoto wake watajisikiaje ? Je aliridhia kurekodiwa ? unajuwa kosa la kuharibu privacy ya mtu ? je kuna umuhimu gan kumrekodi kwanza ? pili kuna umuhimu gan kusambaza video ulizorekodi ? TUJIFUNZE KUWAHESHIMU WENGINE BILA KUJALI UMRI , CHEO , KABILA , DINI AU JINSIA AU ELIMU , MAANA UPANDE MWINGINE ANAEZA KUWA MTU ANAEHESHIMIKA SANA , UNAEZA UKAONA NI KITU KDG ILA KIKAMUATHIRI KISAIKOLOJIA MAISHA YAKE YOTE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…