Je, ni tabia yako ipi hutamani watoto wako wairithi na ipi unatamani wairithi?

Je, ni tabia yako ipi hutamani watoto wako wairithi na ipi unatamani wairithi?

Agresive

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2018
Posts
891
Reaction score
1,237
Nawasalimu katika jina la JMT.

Kazi iendelee.

Moja kwa moja kwenye mada.

Katika maisha tunayoishi tunafanya mambo mengi na kupitia vitu kadhaa.

Baadhi matendo ni mazuri mengine si mazuri. Pia baadhi ya Tabia ni njema lakini nyingine si njema.

Pia kuna baadhi ya tabia si mbaya wala hazikuvunjii heshima lakini kuna muda unatamani kuacha lakini inakuwa ngumu sana kuiacha maana imeshakuwa sehemu ya maisha yako.

Sasa je ni tabia au mwenendo upi unamuomba Mungu muweza wa yote asaidie wanao wasiirithi.

Na tabia ipi au mwenendo pia unatamani wanao warithi.

Binafsi kwangu tabia ya kuchepuka Mungu asaidie wasirithi hii. Maana hata mie siipendi ingawa kuwa kuacha pia imekuwa ngumu.

Pia tabia ya kuamini watu kwa suala la pesa unamkopesha baadaye kukulipa ugomvi na moyo wa huruma sana hii pia wasirithi maana nimepoteza pesa kwa kuamini watu.
 
Natamani wanangu warithi tabia yangu ya kutokuwa mnafiki kama Magufuli.

Tabia ambayo sipendi hata kidogo waniige ni ku-kerisha watu. Endapo wakiwa wahadhiri wawe na huruma wasiwe kama baba yao Neb. Waulizeni wanafunzi wangu wa UDSM wananijua dadeki...
 
Watu wakiker sana huwa mnajisikiaje
Natamani wanangu warithi tabia yangu ya kutokuwa mnafiki kama Magufuli.

Tabia ambayo sipendi hata kidogo waniige ni ku-kerisha watu. Endapo wakiwa wahadhiri wawe na huruma wasiwe kama baba yao Neb. Waulizeni wanafunzi wangu wa UDSM wananijua dadeki...
 
Watakoma hukohuko wenyewe wachukue tu yoyote watapambana nazo mi mwenyewe nilizikuta..🙃
 
Back
Top Bottom