Je, ni upi mwitikio wa jamii ya kitanzania katika dawa mpya ya uzazi wa mpango kwa wanaume?

Je, ni upi mwitikio wa jamii ya kitanzania katika dawa mpya ya uzazi wa mpango kwa wanaume?

Shida ni pale mume wakp aende kwa mcheps afu apigwe massage yenye mpango amazing, mnatafuta watoto weeee mwshowe mnachoka kumbe mwafulani alipewa massage mpango....🧐🧐
😂😂😂😂Aise nacheka lakini umeongea kitu ya maana sana, hakika umewaza mbali🤝​
 
Ila wadau bwana, mbona mnakubali wake zenu kutumia hayo mauzazi ya mpango ilhali yana madhara kibao, mood swings, wengine wanapata mauvimbe, wengine cycle zao zimeathirika lakin hamuoni hilo, na mnajua kabisa ni hayo madude yanawaathiri, hapa umoja wenu wa mataifa unataka kuguswa mmekemea kwa nguvu zote, ina maana hamuwajali wake zenu, mnajijali nyinyi tu? Hamna huruma eti?
🤔🤔🤔Mmmh, una hoja nzito📌
 

Ndugu Wanajamvi,

Ninawaletea mjadala wenye uzito wa kielimu na kifikra kuhusu maendeleo mapya katika teknolojia ya uzazi wa mpango kwa wanaume. Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu mjadala unaoendelea kuhusu dawa mpya ya uzazi wa mpango kwa wanaume, ambayo inaonekana kupokelewa na pande mbili tofauti katika nchi yetu. Kuna wanaounga mkono na wanaopinga. Wanaounga mkono wanaona hii kama hatua muhimu katika kuleta usawa wa jinsia katika majukumu ya uzazi wa mpango. Wanaopinga wanahofia athari za kiafya na kisaikolojia, pamoja na changamoto za kiutamaduni.

Faida na Hasara: Dawa hii ina faida zake, kama vile kumpa mwanamke uhuru zaidi na kuepusha mimba zisizotarajiwa. Hata hivyo, kuna wasiwasi kuhusu athari za kiafya na kisaikolojia, hasa kuhusiana na nguvu za kiume na uzalishaji wa mbegu.

Dawa hii, ambayo inatumia homoni mbili za kiume, nestorone na testosterone, inategemea kuwa njia mbadala kwa wanaume kuchangia katika uzazi wa mpango kwa njia ambayo haijawahi kuonekana before.​

Hata hivyo, kuna masuala kadhaa ambayo yanahitaji kujadiliwa kwa kina ili kuhakikisha kuwa mapokeo ya dawa hii nchini Tanzania yatakuwa yenye tija na kuzingatia mila, desturi, na hali halisi ya kijamii.​
  1. Usalama na Ufanisi: Ni muhimu kujadili kwa kina kuhusu ufanisi wa dawa hii na usalama wake kwa matumizi ya muda mrefu.​
  2. Mabadiliko ya Kiutamaduni: Tunapaswa kuchambua kwa umakini jinsi gani dawa hii itakavyopokelewa katika jamii yetu, ambayo ina mila na desturi zake. Je, wanaume wa Kitanzania wako tayari kutumia njia hii mpya ya uzazi wa mpango?
  3. Athari za Kisaikolojia: Ni muhimu kujadili athari za kisaikolojia kwa wanaume wanaotumia dawa hii, hasa kuhusiana na masuala ya nguvu za kiume na uzalishaji wa mbegu. Je, kuna wasiwasi wowote wa kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa?
  4. Mbinu za Uzazi wa Mpango Zilizopo: Tunapaswa kulinganisha dawa hii mpya na mbinu zingine za uzazi wa mpango zinazotumika na wanaume kama vile kondomu na upasuaji wa mirija ya uzazi. Je, dawa hii itakuwa na faida zaidi ukilinganisha na mbinu zilizopo?
Ninawaalika wataalamu, wanazuoni, na wanajamii kuchangia mawazo yao kuhusu mada hii nyeti na ya kipekee. Tujadili kwa kina na tufungue ukurasa mpya katika historia ya uzazi wa mpango nchini Tanzania.​

Karibuni kwenye mjadala!
Huu ni upuuzi wa hali ya juu kabisa,kupoteza muda kwa kujadili ajenda ovu kama hii,na inadhihirisha uwezo mdogo wa kufikiri uliopo kwa mnaowaita wasomi na wataalam wetu.
Tunajua na kuona mpango na harakati mbalimbali za kupunguza idadi ya watu duniani mf.magonjwa,vita, ugaidi,uzazi wa mpango n.k.na bado hatufikirii athari zake kama zilivyoanza kwa wanawake [nyota ya kijani,uzazi wa mpango,vipandikizi,sindano n.k.]sasa tunashuhudia matokeo yake, magonjwa kibao ya mfumo wa uzazi, matokeo hasi kwa baadhi ya watoto wanaozaliwa n.k.,bado bila aibu/haya mnajadili kuwashawishi wanaume kutumia hizo dawa ,mwogopeni Mungu,aliyetuagiza tuzae tuijaze nchi.
Tunajiandaa kuwa na taifa la namna gani baadae,ikiwa kabla hatujamaliza la ushoga,mnaleta mpango wa uzazi kwa wanaume,hamuoni kuwa hawa wazungu wamekusudia kudhoofisha na kuyamaliza mataifa ya Africa?Mnasikitisha sana,Ni hasara sana kwa taifa kuwa na wasomi na wataalam wa aina yenu.
 
Huu ni upuuzi wa hali ya juu kabisa,kupoteza muda kwa kujadili ajenda ovu kama hii,na inadhihirisha uwezo mdogo wa kufikiri uliopo kwa mnaowaita wasomi na wataalam wetu.
I bet, hujasoma hii thread na kama umesoma basi hujaielewa. I have a reason to say so✍️.​
Tunajua na kuona mpango na harakati mbalimbali za kupunguza idadi ya watu duniani mf.magonjwa,vita, ugaidi,uzazi wa mpango n.k.na bado hatufikirii athari zake kama zilivyoanza kwa wanawake [nyota ya kijani,uzazi wa mpango,vipandikizi,sindano n.k.]sasa tunashuhudia matokeo yake, magonjwa kibao ya mfumo wa uzazi, matokeo hasi kwa baadhi ya watoto wanaozaliwa n.k.
Huu ni mtazamo mmoja wapo ambao hata katika thread hii umezungumzwa (angalia reply #21)​
bado bila aibu/haya mnajadili kuwashawishi wanaume kutumia hizo dawa
Nadhani hujausoma vizuri huu uzi na kuufatilia, hakuna sehemu yeyote ya uzi huu iliyo ashiria kumshawishi mtu yeyote kwa namna yeyote, bali kutoa fursa ya kujadili pamoja na kujua juu ya muitikio wa dawa hii Tanzania (yani, namna watu wanavyo ichukulia).​
hatujamaliza la ushoga,mnaleta mpango wa uzazi kwa wanaume,hamuoni kuwa hawa wazungu wamekusudia kudhoofisha na kuyamaliza mataifa ya Africa?
Kwanza kabisa sio kwamba tumeuleta mpango, ni mjadala wa kujadili juu ya vila watanzania wanawaza kuhusu mada husika. Lakini pia, hoja kama hii unayo rise tayari ilikua imesha tolewa katika reply #29, na ndiyo maana nasema haujausoma vizuri huu uzi ama haujauelewa na kufatilia.​
Mnasikitisha sana,Ni hasara sana kwa taifa kuwa na wasomi na wataalam wa aina yenu.
Naheshimu mawazo yako🤝.
 
Back
Top Bottom