Hakuna kitu cha maana ambacho tumeisaidia dunia. Kiufupi tupo tupo tu, Tunasubiria watu wa mashariki ya mbali waje watusaidie.
Tumejiandaa vipi majanga ya asili kama tsunami, tetemeko etc yakitotea?
Je, Kuna siku Waafrika tutakuja kuwa na akili za kuweza kutatua changamoto zetu? Au ndo tuseme bongo za Wanadamu zinatofautiana, Au ni kweli kuna namna ya kuchaji ubongo kwa kutumia binaural beats na baadhi formula ambazo zinajulikana kwa baadhi ya watu wachache tuu.
Maswali ni mengi ya kujiuliza, Mzungu aliwezaje kuunda ndege, Mzungu aliwezaje kuunda bunduki, Mzungu aliwezaje kuunda nyuklia bomb, Mzungu aliwezaje kuunda simu, Mzungu aliwezaje kuunda magari bila kusahau silaha za kibayolojia. Au ndo tuseme Wagunduzi hawakuwa watu wa kawaida (!!!) Mambo ni mengi ya kufikirisha.
Hakuna kitu Mzungu hajafanya, Lakini sisi Waafrika tunajivunia nini? Au kuna siku nasi tutafanya makubwa? Kichwa kinawaza sana..
Au ile sayansi ya alchemy ina matokeo katika technology? Mbona maswali ni mengi.
Tafadhalini njooni tujadili hili jambo la watu kuzidiana akili.
Kuna mambo mawili:
1: Kuwa na uwezo mdogo wa kutumia akili.
2: Kuwa na akili kidogo(hapa kuna shida ya afya ya akili).
Yote 1 na 2 hapo juu unaweza kuyapata kwa kuzaliwa nayo au kuyatengenezea mazingira baada ya kuzaliwa. Hivyo, tunachokiona kwa mtu ni matokeo kuzaliwa nacho na kuendelea kutengenezewa mazingira au kuondolewa mazingira ya maendeleo.
Kwa mantiki hiyo haya mambo huweza kupatikana kwa sababu moja kuleta mojawapo ya hali husika au kuleta jingine au kuleta yote kwa pamoja.
Ili uweze kuelewa juu ya haya ni vyema kufahamu kuwa uwezo wa akili na kiasi cha akili huweza kusababishwa na:
1: Kiasi cha akili na uwezo wa wazazi(mtoto kurithi).
2: Afya ya mzazi/mama wakati wa ujauzito/lishe.
3: Mazingira ya afya ya akili ya mama wakati wa ujauzito.
4: Mahusiano ya mama na mazingira wakati wa ujauzito.
5: Lishe ya mtoto wakati akiwa mchanga.
6: Lishe ya mtoto wakati anapokua.
7: Uhusiano wa mtoto na wanajamii kama jirani, ndugu na mwalimu nk.
8: Nafasi ya mtoto kujifunza na ku-challenge anayokutana nayo maishani.
9: Mazingira anayokulia mtoto na kumpatia challenge mbalimbali za kidunia.
10: Uwepo wa na utayari wa kumsadia mtoto anapopata challenge zenye kumpatia msukosuko kwake kijumla.
11: Uwepo wa mazingira wezeshi ya mtu kuibuka na kutenda kwa kadri ya uwezo wa akili.
12: Nk.
A: Hivyo, wenye kuwa na uwezo mdogo wa akili wapo pia kwenye mataifa ya wenzetu huko mbele na wasioweza kutumia uwezo wao pia wapo. Ila mazingira yao yamewapa nafasi wanaoweza kutumia akili kujitanabaisha vyema. Sisi hata kama una uwezo mzuri unaweza kujikuta mazingira hayakuruhusu kujipambanua na yale uliyonayo. Tunafuata yaliyopo kuliko kutafuta mapya.
B: Kulingana na maelezo kule juu, unaweza kumchukua mtu ambae anaonekana wa kawaida huku kwetu, akaenda kuwa Genius huko mbele kwa wenzetu kwa mazingira yaliyopo.