Je, ni wizara gani kubwa inayotengewa hela nyingi?

chamaclotus

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2019
Posts
1,079
Reaction score
2,273
Salaam wakuu,

Nimekuwa nikijiuliza hili swali kwamba je ni wizara gani ni kubwa kati ya hizi wizara tulizo nazo na ambayo imekuwa ikitengewa pesa nyingi ukilinganisha na zingine?

Naomba wajuzi wa mambo mnifahamishe.
 
Kutengewa na kupewa ni vitu viwili tofauti.

Unaweza kutengewa pesa ndefu lakini mwishowe ukaambulia nusu ya pesa yote uliyotengewa

Je, hujawahi kusikia mawaziri wanalalamika kuwa wametengewa e.g. 10bn lakini hadi mwaka wa serikali unaisha wao wamepewa 40% tu ya pesa waliyotengewa?
 
duh hivi anayewapa ni nani hasa
 
Ninavyojua mimi TAMISEMI inabeba asilimia zaidi ya hamsini ya bajeti kwa maana ya matumizi ya kawaida (mishahara, nk) na matumizi ya maendeleo (maji, umeme, elimu, afya, barabara, nk).
nadhani ila nmeona wizara ya fedha nayo ni hatari ukiweka na mambo ya kulupa madeni ya nchi za nje
 
Back
Top Bottom