Mkuu Zurri, hii kauli yako siyo sahihi pale unaposema "Nijuavyo mimi kuwa kile kilicholetwa na mwanadamu hakikosi kasoro na "sayansi ikiwemo".
kwanza ni lazima tufahamu kuwa sayansi ni elimu ambayo mwanadamu huipata popote katika njia mbalimbali ili aweze kuyatumia mazingira yake kikamilifu kwa ajili ya maendeleo yake kwa muktadha huo sayansi inatoka kwa Mungu na hata ukisoma maelezo ya baadhi ya wanasayansi maarufu utakuta walikuwa katika hali fulani wakimsifu/kumtaja Mungu kuonyesha uthamini wao Kwake, kifupi ni kwamba elimu yoyote yenye manufaa kwa watu imetoka kwa mungu lakini inawezekana kutokana na mapungufu ya kibinadamu tukashindwa kutumia ipasavyo au tukaitumia kinyume elimu ya sayansi hata hivyo bado elimu hiyo itabaki kuwa ni kutoka kwa Mungu.
Halikadhalika,Mungu hutoa kidogo kidogo elimu ya sayansi kwa watu pale anapotaka, hebu chukua mfano tofauti iliyokuwepo leo na miaka iliyopita katika maendeleo ya sayansi- leo sayansi ipo juu mno katika kila nyanja na bado Mungu akipenda itakwenda juu zaidi ya hapa kama tusipokufuru na kuifanya sayansi na teknolojia kuwa Miungu badala ya Mungu wa kweli mkuu, aliyejuu na mwenye sifa zote njema.