Je ni yupi anapaswa kulaumiwa nyoka au ibilisi?

Mr Antidote

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2015
Posts
953
Reaction score
1,304
Wakuu habari zenu, natumaini mko poa kabisa. Baada ya salaam hiyo fupi wacha nijikite moja kwa moja katika mada husika.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza kutaka kuhoji na kuuliza ni nani kati ya hivyo vitu viwili ambae tunapaswa kumlaumu kwa matokeo yote baada ya Adam na Eva (Hawa) kula tunda.

Ukisoma kitabu cha mwanzo sura ya pili kinaelezea uumbwaji wa viumbe hai vingine (except Adam) wanyama, ndege nk. Bila kumsahau Eva. Baada ya Mungu kuumba wanyama wote alimpa Adam awaite majina na kila jina alilowapa Adam ndio majina yao waliyovyoitwa. Hii inamaanisha simba, chura, kinyonga, nyoka nk wote hawa waliitwa hivi na Adam.

Ukisoma mwanzo sura ya tatu inavyoanza tu pale mstari wa kwanza tunaambiwa nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote. Ukiendelea mbele unaonA nyoka anatumia werevu wake kumshawishi Eva kula tunda na kisha Eva kumshawishi Adam. Kwa mujibu wa biblia hapa dhambi ndo inaingia ulimwenguni. Matokeo ya kitendo hicho ni kulaaniwa kwa nyoka na adhabu kali kwa mwanadamu.

Sasa swali ni kwamba...
Je tunasababu ipi ya kumlaumu Lucifer (shetani) kwa kosa ambalo lilitendwa na nyoka kutokana na werevu wake kama andiko linavyosema?

Au ni shetani alimwingia nyoka na kumuhadaa mwanadamu (lakini biblia haijasema, imesema tu nyoka alikua ni mwerevu)?

Na kama shetani alimwingia nyoka kwanini nyoka alaaniwe kwa kosa ambalo alilubuniwa na Lucifer ambaye alikua na uwezo mkubwa ambao aliwezA kugundua udhaifu wa huyo nyoka na kuutumia?

Au Lucifer na nyoka anayeongelewa ni kitu kimoja?

Natanguliza shukrani!!
 
Kilichotokea ni Lucifer kujigeuza kufanana na nyoka! Kumbuka Lucifer anauwezo wa jigeuza
Na kua kama malaika Wa nuru
 
nashukuru umesema uumbaji ulioandikwa katika Bibilia, hizo ni simulizi tu hazina ukweli wowote, Mungu si binadamu ahangaike kuchukua udongo atengeneze mwanadamu kwa masaa 24 akitokwa na jasho

kusema nyoka au shetani alimdanganya mwanadamu, hiyo ni janja ya mwanadamu mwenyewe kukwepa uwajibikaji, kifo mwanadamu alikikuta kipo (Asili), kilisababishwa na mabadiliko (evolution) fikiria km wanadamu tunavyozaana km tungelikuwa tuna kufa Je kungelikuwa na ardhi yeyote ya kutosha kuishi wanadamu walio kufa na walio hai sasa?

kila jamii ina simulizi zake za mwazo wa dunia na mwanzo wa binadamu, bibilia ni simulizi za uumbji za dunia ya wayahudi, kwa taarifa hawa wayahudi na waarabu, tangu mwanzo walikuwa na Mungu anayeitwa ENLY Mungu huyu alikuwa Mungu mtia mimba na kwa niaba ya miungu, alimtia mimba MADU ambaye hakuwa tayari kuupokea uzazi lkn kwa sababu ya miungu alikubali, wakati huo alikuwapo na mtu anayeitwa ADAM alikuwa na mkewe aliyeitwa LILITHI, LILITHI ni jini jike LILITHI huyu siku moja aliringa kujaamiiana na ADAMU akasikitika sana, ndipo Mungu akaja kumlaza usingizi akachukua ubavu akamtengenezea mke mwingine anaitwa HAWA,

Simulizi zsa uumbaji zilizoandikwa ktk misaafu ya kidini ni simulizi za Miungu zilizoboreshwa
 
Hapo hamna cha nyoka wala ibilisi kwa sababu havikujiumba vyenyewe viliumbwa.
 
Duuuuh,, nashangaa wajenzi huru wanaongezeka ....hatari hii 🙂🙂 mara hakuna uumbaji, hakuna ibilisi, hakuna adamu, aiseeee
 
Kila kitu alichokiumba Mungu kilo kwenye utaratibu wake,na Mungu hakosei,ukija kwenye anguko huwezi leo ukasema nyoka na shetani ni vitu tofauti,maana nyoka alikua a natembea kwa miguu kama kawaida ndio maana baada ya anguko la Hawa Mungu alimlaani Nyoka akamwambia tangu leo kwa tumbo utakwenda na mavumbi ndio kitakua chakula Chako. Na kulifahamu hili ni lazima uwe na ufunuo unaposoma maandiko bila msaada wa Mungu hutaweza kulifahamu hilo kamwe hata mwanasayansi,msomi yeyote hataelewa hili.i amuhitaji Roho mtakatifu kukifunua kwako.na unaposema ni historia nadhani unakosea kwasababu Hilo ni Neno la Mungu liloandikwa kwa ufunuo kupitia kwa MANABII, kwani Neno la Mungu Kwanza huja kwa Nabii ndipo ulipate wewe.
Sasa kumbuka Huwezi kumlaumu Adam kwani tayari shetani sikuzote huangalia mahali penye upenyo.na pia ujue Adam ni kiumbe cha Asilimia katika uumbaji wa Mungu,Adam hakua na kitovu kama tulivyo sisi ambao tunavyo kwakua tumenyonya tokea tumbo ni mwa mama zetu,Adam hakudanganywa bali hawa ndio alidanganywa na ndio maana aliweza kushiriki tendo hili.
 
wakulaumiwa ni mwanadamu (huyo Eva&Adam) kwa sababu walikosa unyenyekevu mbele za Mungu. Hakuna hata mmoja aliyeomba msamaha kwa kosa walilofanya. Huwa najaribu kufikiria kama wangemuomba mungu msamaha je asingewasamehe?
 
Kwenye Biblia hawakuomba Msamaha. Ila kwenye Quran waliomba Msamaha.
 
Wakuu habari zenu, natumaini mko poa kabisa. Baada ya salaam hiyo fupi wacha nijikite moja kwa moja katika mada husika.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza kutaka kuhoji na kuuliza ni nani kati ya hivyo vitu viwili ambae tunapaswa kumlaumu kwa matokeo yote baada ya Adam na Eva (Hawa) kula tunda.

Ukisoma kitabu cha mwanzo sura ya pili kinaelezea uumbwaji wa viumbe hai vingine (except Adam) wanyama, ndege nk. Bila kumsahau Eva. Baada ya Mungu kuumba wanyama wote alimpa Adam awaite majina na kila jina alilowapa Adam ndio majina yao waliyovyoitwa. Hii inamaanisha simba, chura, kinyonga, nyoka nk wote hawa waliitwa hivi na Adam.

Ukisoma mwanzo sura ya tatu inavyoanza tu pale mstari wa kwanza tunaambiwa nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote. Ukiendelea mbele unaonA nyoka anatumia werevu wake kumshawishi Eva kula tunda na kisha Eva kumshawishi Adam. Kwa mujibu wa biblia hapa dhambi ndo inaingia ulimwenguni. Matokeo ya kitendo hicho ni kulaaniwa kwa nyoka na adhabu kali kwa mwanadamu.

Sasa swali ni kwamba...
Je tunasababu ipi ya kumlaumu Lucifer (shetani) kwa kosa ambalo lilitendwa na nyoka kutokana na werevu wake kama andiko linavyosema?

Au ni shetani alimwingia nyoka na kumuhadaa mwanadamu (lakini biblia haijasema, imesema tu nyoka alikua ni mwerevu)?

Na kama shetani alimwingia nyoka kwanini nyoka alaaniwe kwa kosa ambalo alilubuniwa na Lucifer ambaye alikua na uwezo mkubwa ambao aliwezA kugundua udhaifu wa huyo nyoka na kuutumia?

Au Lucifer na nyoka anayeongelewa ni kitu kimoja?

Natanguliza shukrani!!
Je nani aliumba Nyoka na Ibilisi??Je nani aliyempa uwezo mkubwa zaidi ya mwanadamu mpendwa huyo Ibilisi???....Kwanini???
 
1 Kila alicho kiumba Mungu kiko sawa....
a. Alidhamiria kumuumba mwovu?
b. Alidhamiria Adam aanguke?

2 anguko la bustanini sio vitu halisi pale ni

2 anguko la bustanini sio vitu halisi pale ni lugha ya picha hapakuwa na nyoka halisi wala tunda halisi noooo. Jifunze hapo
3. Adam hakuweza kudanganyika mbona alikula tunda? Au alipewa usingizini?
 
Je nani aliumba Nyoka na Ibilisi??Je nani aliyempa uwezo mkubwa zaidi ya mwanadamu mpendwa huyo Ibilisi???....Kwanini???
Ibilisi alikuwa ni malaika na alitaka kuipindua Mungu Means alikuwa na nguvu karibu na Mungu na pia hakunyang'anywa zile nguvu alizokuwa nazo.
 
Wakuu habari zenu, natumaini mko poa kabisa. Baada ya salaam hiyo fupi wacha nijikite moja kwa moja katika mada husika.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza kutaka kuhoji na kuuliza ni nani kati ya hivyo vitu viwili ambae tunapaswa kumlaumu kwa matokeo yote baada ya Adam na Eva (Hawa) kula tunda.

Ukisoma kitabu cha mwanzo sura ya pili kinaelezea uumbwaji wa viumbe hai vingine (except Adam) wanyama, ndege nk. Bila kumsahau Eva. Baada ya Mungu kuumba wanyama wote alimpa Adam awaite majina na kila jina alilowapa Adam ndio majina yao waliyovyoitwa. Hii inamaanisha simba, chura, kinyonga, nyoka nk wote hawa waliitwa hivi na Adam.

Ukisoma mwanzo sura ya tatu inavyoanza tu pale mstari wa kwanza tunaambiwa nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote. Ukiendelea mbele unaonA nyoka anatumia werevu wake kumshawishi Eva kula tunda na kisha Eva kumshawishi Adam. Kwa mujibu wa biblia hapa dhambi ndo inaingia ulimwenguni. Matokeo ya kitendo hicho ni kulaaniwa kwa nyoka na adhabu kali kwa mwanadamu.

Sasa swali ni kwamba...
Je tunasababu ipi ya kumlaumu Lucifer (shetani) kwa kosa ambalo lilitendwa na nyoka kutokana na werevu wake kama andiko linavyosema?

Au ni shetani alimwingia nyoka na kumuhadaa mwanadamu (lakini biblia haijasema, imesema tu nyoka alikua ni mwerevu)?

Na kama shetani alimwingia nyoka kwanini nyoka alaaniwe kwa kosa ambalo alilubuniwa na Lucifer ambaye alikua na uwezo mkubwa ambao aliwezA kugundua udhaifu wa huyo nyoka na kuutumia?

Au Lucifer na nyoka anayeongelewa ni kitu kimoja?

Natanguliza shukrani!!
Habari ya nyoka... Tunda.. Bustani... Ni lugha ya picha.
Hebu jiulize haya.
1 wanyama walikuwa wanaongea?
2 kwann Mungu aweke mitego kiasi hicho angali anajua binadamu ni dhaifu?
3.......
4.....
 
wakulaumiwa ni mwanadamu (huyo Eva&Adam) kwa sababu walikosa unyenyekevu mbele za Mungu. Hakuna hata mmoja aliyeomba msamaha kwa kosa walilofanya. Huwa najaribu kufikiria kama wangemuomba mungu msamaha je asingewasamehe?
Msamaha ulikuwa sio wa hapo hapo...lazma utumike adhabu uonje ghadhabu ya Mungu. Kumbuka kipindi cha kina musa...
 
Kwa nn nyoka alipewa akili nyingi akawa mwerevu zaidi kuliko wanyama wote,,,? Ukinijibu utajua wa kulaumiwa ni nani?
 
Back
Top Bottom