Mr Antidote
JF-Expert Member
- Jan 11, 2015
- 953
- 1,304
Wakuu habari zenu, natumaini mko poa kabisa. Baada ya salaam hiyo fupi wacha nijikite moja kwa moja katika mada husika.
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza kutaka kuhoji na kuuliza ni nani kati ya hivyo vitu viwili ambae tunapaswa kumlaumu kwa matokeo yote baada ya Adam na Eva (Hawa) kula tunda.
Ukisoma kitabu cha mwanzo sura ya pili kinaelezea uumbwaji wa viumbe hai vingine (except Adam) wanyama, ndege nk. Bila kumsahau Eva. Baada ya Mungu kuumba wanyama wote alimpa Adam awaite majina na kila jina alilowapa Adam ndio majina yao waliyovyoitwa. Hii inamaanisha simba, chura, kinyonga, nyoka nk wote hawa waliitwa hivi na Adam.
Ukisoma mwanzo sura ya tatu inavyoanza tu pale mstari wa kwanza tunaambiwa nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote. Ukiendelea mbele unaonA nyoka anatumia werevu wake kumshawishi Eva kula tunda na kisha Eva kumshawishi Adam. Kwa mujibu wa biblia hapa dhambi ndo inaingia ulimwenguni. Matokeo ya kitendo hicho ni kulaaniwa kwa nyoka na adhabu kali kwa mwanadamu.
Sasa swali ni kwamba...
Je tunasababu ipi ya kumlaumu Lucifer (shetani) kwa kosa ambalo lilitendwa na nyoka kutokana na werevu wake kama andiko linavyosema?
Au ni shetani alimwingia nyoka na kumuhadaa mwanadamu (lakini biblia haijasema, imesema tu nyoka alikua ni mwerevu)?
Na kama shetani alimwingia nyoka kwanini nyoka alaaniwe kwa kosa ambalo alilubuniwa na Lucifer ambaye alikua na uwezo mkubwa ambao aliwezA kugundua udhaifu wa huyo nyoka na kuutumia?
Au Lucifer na nyoka anayeongelewa ni kitu kimoja?
Natanguliza shukrani!!