je nikaze roho nimkubali huyu kaka???

korino

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Posts
1,004
Reaction score
666
Habari zenu wanajf! naombeni ushauri wenu juu ya hili! mimi ni mschana nilikuwa na rafki angu mpendwa wa kike ambae amefariki dunia mwaka sasa unafika! huyo marehem rafk angu alikuwa na boyfrend wake hapohapo chuoni! yule rafk angu alinipenda sana na mara nyingi alikuwa akinisifia sana kwa boyfrend wake km mm ni msichna bora n.k!

Mpaka ikafkia wakati yule boyfrend wake akawa ananiita mimi mke mdogo! ilikuwa ni kama utani tena mbele ya rafki yangu! tuliheshimiana sana sote watatu!baada ya kufariki kwa shost angu huyu kaka sasa ananitongoza na anasema anataka anioe! ni mda mrefu sasa ananisumbua sana!

Nashindwa kumkubalia kutokana na najskia vibaya sana mda mwingine nahisi km nkimkubali basi ni kama namsaliti marehemu shost angu! na je ulimwengu utanichukuliaje mimi?

Wengine wanaweza wakafkiria huenda nilikuwa namsaliti rafki angu kabla hajafa! mbaya zaidi nimetokea kumpenda sana sana huyu kaka! nishaurini jamani nikaze roho nimkubali ama nimshit!!?? Niokoeni ktk janga hili ndugu zangu
 
kwani, kama angefariki mshikaji wake mwingine ambaye humfahamu, angekutokea je ungemkubalia?

kama ndiyo bac fanya hivyo
 
Huyo shoti wako alifariki na ugonjwa gani? Ina maana kipindi chote huyo shosti wako alipokuwa hai hukuwa na mtu mpaka akafa na saizi bado huna mtu?

Uhusiano wa marehemu ulifikia wapi kwa maana ya kujulikana?
 
nlikuwa na mahusiano na rafk ake huyo kaka ambae ananitaka sasa! lkn huyo rafk ake alinisaliti kwa mda mfupi sana! nliamua kuachana nae! tulikaa pamoja kwa mda usiozid miezi 2 nlipogundua ananicheat nkamuacha na sikuingia kwenye uhusiano hadi hii sasa! tulikuwa km marafiki wa kawaida ckuwah hata kukiss nae! rafiki angu aligongwa na gari
 

Haya mambo siyo mepesi hivyo. Mtaoana ndiyo, mapenzi ya kudanganyana ya mwanzo yakiisha, anaanza kuwaza-kama alimsaliti shost yake, nami kesho si atanisaliti? sisi tulio kwenye ndoa mika zaidi ya 20 tunayajua hayo. Amini kuna siku atajiuliza swali hilo kitambaa cha mapenzi kilichowafunika nyuso zenu kikitoka. Just imagine, kuna mwanamke alikuwa anamkacha mume wake anafanya mapenzi na mwanamume. Exactly kama ilivyotokea kwenu, yule mume wa mwanamke akafa, basi wakapata nafasi ya kuoana. Believe it, yule mwanamume alikuja kuniambia kuwa mwanamke alivyokuwa anamkacha mume wake atanikacha na mimi. Ndoa haikudumu!!!!!!!
 
sawa lkn mm ckuwa na mahusiano nae huyu kaka na wala ckuwahkufkiria hicho kitu! na ameanza kunitongoza baada ya kifo cha rafk angu! thx kwa ushauri wako
 
  • :decision:

Kipenda roho hula nyama mbichi, jibu la swali unalo mwenyewe so fuata moyo wako.
 

Achana nae huyo hakufai kwa sababu:

1.0 Ulishatembea na rafiki yake na kuachana, kama bado ni marafiki inaweza kuleta shida kwa hao marafiki hasa mumeo ambaye atakosa amani kila amuonapo rafiki yake na maneno ya hapa na pale ambayo yanaweza kuwafitinisha.

2.0 Still you have the chance to others, labda purposely uwe ulikuwa umefunga mlango.

3.0 Hujanijuza bado kuhusu mahusuano na huyo jamaa anayekutaka yalifikia wapi?
 
piper mimi moyo wangu hautaki kumkubali lkn nampenda kweli! hicho kitoto chako ckipendi hapo kinanicheka
 
Huyo shoti wako alifariki na ugonjwa gani? Ina maana kipindi chote huyo shosti wako alipokuwa hai hukuwa na mtu mpaka akafa na saizi bado huna mtu?

Uhusiano wa marehemu ulifikia wapi kwa maana ya kujulikana?

Kweli, vizuri kutuambia kwanza rafiki yako alifariki katika mazingira gani?
 
piper mimi moyo wangu hautaki kumkubali lkn nampenda kweli! hicho kitoto chako ckipendi hapo kinanicheka

The is no logic moyo ukatae lakini unampenda, mapenzi yanakaa moyoni bana.

Mashaka yangu kwako ni jinsi ya kuanza na huyo jamaa ndicho kimachokusumbua na si kumkubalia. Huelewi uanzie wapi na unajaribu kupata mapokeo ya jamii yatakwaje?
 
Ni muda gani tangia afariki rafiki yako?
Jamii iliokuzunguka inakuchukuliaje wewe na marehem rafiki yako?
Wewe binafsi ukoje? hauyumbishwi na maneno ya walimwengu?
Je mnapendana na huyo jamaa?
Nafsi yako haikusuti kusonga mbele?

Majibu ya masuala haya ndio msingi wa jibu lako.

Good luck
 
naona mahusiano yako yamegubikwa na utata mkubwa, kama kuna uwezekano ni bora uachane na hayo mawazo ili jinamizi la marehemu shosti wako lisikutafune. :hand:
 
Mkubalie tu ale tunda..ila what goes around comes around..!
 

subiri wa kwako!Itaonekana kama ulikuwa na uhusiano nae kabla rafiki yako hajafa!
 

Nadhani si mbaya, kama mwapendana sioni tatizo. Itakuwa ni nafasi nzuri kumuenzi marehemu rafiki yako. Pole kwa yote!
 

inakaribia mwaka sasa tangu afariki, tulikuwa marafiki sna na shost angu, nayumbishwa sana na maneno ya watu ikitokea nkimkubali na wakajua km nipo nae!, tunapenda sana na huyo kaka, japo cjamkubali lkn tunapendana! niko ktk wakati mgumu kaka nisaiedieni
 
kama unampenda na ni furaha yako,mkubali bana........waswahili wanasema kufa kufaana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…