je nikaze roho nimkubali huyu kaka???

subiri wa kwako!Itaonekana kama ulikuwa na uhusiano nae kabla rafiki yako hajafa!

watu wanaolewa na waume wa dada zao sembuse rafiki! Suala ni kuangalia kama uwezekano wa kudumu nae na kama kuna upendo wa kweli.
 
mimi naona hapo hamna tatizo,we mkubali mshikaji akuweke ndani kwani rafiki yako aliishafariki na usiishi kwa kuangalia watu wanasema nini
 

Vipi kama huyo jamaa naye ni member wa JF? Huoni kuwa anaweza kutumia fursa hii kukushauri ukubaliane naye bila wewe kujua kama ni yeye ndiye anatoa ushauri? Just thinking aloud!!!!
 
Dada kama moyo wako unasita acha na heshimu sana moyo wako.Ushauri wote unao ndani ya moyo wako.Respect ya instincts.Kila la heri.
 
well Said mkuu, kama aliweza kumsaliti mumewe akamfuata mshikaji, kwani itashindikana vipi kumsaliti mshikaji na kwenda kwa mshikaji mwingine, uaminifu kwa mwanamke uko rehani, asili haipotei.
 

Nimesoma mara mbili mbili uzi huu na nimeelewa kuwa hapo kuna penzi la dhati tena penzi lenye malengo mema kwa maana hiyo basi usiache moyo wako uteseke kwa kitu ulichokipenda. Kijana anamalengo mazuri na wewe na kama shost wako alikuwa anakubaliana nae pale alipokuwa akikuona wewe kama mke wake mdogo basi hata huko aliko atakubali tu. Kuna watu walikutana makabulini mwanaume alikuwa anajenga kabuli la mke wake na mwanamke alikuwa anajenga kabuli la mume wake bahati mbaya zaidi marehem hao walikufa siku moja. Kutokana na mshangao huo basi hawa wapendwa waliobaki duniani waliamua kuanzisha uhusiano ambao ulileta ndoa yenye balaka. Mshukulu mungu kwa kuwa huyo kijana amekuona wewe na wewe ndo unafaa kuwa mke wake. Kila la kheri mdada
 
Sioni kama kuna shida hapo.

Ila unatakiwa uwe mtu wa msimamo katika maamuzi yako. Jiandae walimwengu tutakusema sana tu, tena tunaweza hadi sema siku anagongwa gari alichanganyikiwa baada ya kuwafumania live.
Be prepared for the worst maneno.
 
ahsanteni sana kwa ushauri wenu nyote ndugu zangu na nitafanyia kazi
 

safi sana chukua chansi kama kumlindia mzigo rafikiyo vipi tena bibie mboni unachelewa aisee..
 
umsaliti marehemu ki vp? m2 akifa kafa 2,
 
kama unampenda na una uhakika na yeye anakupenda olewa bwana,
sion kipingamiz chochote hapo,
ila jifunze kupuuza maneno sbb watu watakusema sana sbb wengi watadhan mlianzana tokea enzi rafiki yako yupo.
Ila nakushauri usitembee na huyo kaka hadi muoane ili hata ukisemwa una uhakika uko ndani ya ndoa yako.
 
shoga yako si ashatangulia no problem.........we mpe tu jamaa mzigo ,aliyepita na lake halipo.........achana na habari za watu wao ni kusema tuuuu
 
-Chunguza rafiki yako kafa na ugonjwa gani
-Marehemu hana sababu, fanay kitu ile roho inapenda
 
kusema tumeumbiwa binadam,so usiogope maneno,watu wapo hai na wanasalitiana itakuwa hyo ameshatangulia,km moyo wako umependa bac sioni tatizo fuata moyo wako mpendwa,labda mungu ndo amekuchaguria hyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…