Haya mambo siyo mepesi hivyo. Mtaoana ndiyo, mapenzi ya kudanganyana ya mwanzo yakiisha, anaanza kuwaza-kama alimsaliti shost yake, nami kesho si atanisaliti? sisi tulio kwenye ndoa mika zaidi ya 20 tunayajua hayo. Amini kuna siku atajiuliza swali hilo kitambaa cha mapenzi kilichowafunika nyuso zenu kikitoka. Just imagine, kuna mwanamke alikuwa anamkacha mume wake anafanya mapenzi na mwanamume. Exactly kama ilivyotokea kwenu, yule mume wa mwanamke akafa, basi wakapata nafasi ya kuoana. Believe it, yule mwanamume alikuja kuniambia kuwa mwanamke alivyokuwa anamkacha mume wake atanikacha na mimi. Ndoa haikudumu!!!!!!!