Je, nikimuacha nitakuwa nakosea?

Je, nikimuacha nitakuwa nakosea?

Habari wadau, ama kweli yakikufika huna namna utazungumza tu. Mwenzenu yamenifika shingoni na sijui kama nikichukua maamuzi ya kumuacha nitakua nakosea au lah.

Nikiri katika mahusiano yote niliyopitia sijawahi kuwa na mwanaume anayenifanya nijisikie furaha kama huyu kaka.Uhusiano wetu una mwaka sasa. Ni mkaka anayepambana sana, anajali, anahudumia pale anapoweza na kule 6*6 ndo usiseme. Hamna kitu ananificha. In short he is a man in every woman's dream mpaka nikawa naogopa kumpoteza bwana.

Mbembe ikaja baada ya kunitambulisha kwa mama yake mzazi (Eh Mungu). Mama alinipokea vizuri tu lakini siku ya kwanza tu akaniambia ukija niletee bia, mtoto wa kike nikapeleka. Baada ya hapo kila nikiona simu ya yule mama yeye ni kutaka hela tu kwangu. Nikajiuliza ni kisa kaniona na gari au ni nini?

On top of that mama yake hatak apange, kashikilia akae nyumbani eti asiharibu hela kwa kulipa kodi. Mshahara wake wote unatumika kwenye matumizi ya nyumbani, kama anabakiza ni kiasi kdg sana. Sasa kutokana na ukaribu huo kati yao naogopa hata kumshauri asije ona nawaingilia maisha yao.

Napata hofu kuwa ntakua adui kwa yule mama, maana akibadilika kimatumizi ataona mimi ndo kisababishi. Jamaa anapanga mipango ya ndoa lakini naogopa sana kuingia kwenye ile familia. Maana hata akiongea nae kwenye simu akiomba hela akimwambia hana anamwambia ahakikishe anaipata anampa na kijana anafanya hivyo.

Je, nikimuacha huyu kijana mapema nitakuwa nakosea?
Humu watu watakushauri kwa kadri watakavyoona inafaa ila mwisho wa siku mwamuzi wa mwisho ni wewe.

Kuna changamoto nyingine ni za kibinadamu tu, kaa na huyo mume wako mtarajiwa mjadiri kuhusu yeye kupanga mana hakuna changamoto kubwa kama kuishi ukweni.

Kuhusu suala la huyo mama kukuomba hela mara kwa mara embu jaribu kumshirikisha mwenzi wako na wakati unamshirikisha fanya kama utani ili umuone ata react vp then majibu utayapata kutokana na reaction yake

Kuwa makini kabla hujaingia kwenye matatizo makubwa huko mbeleni.
 
Jinsi mama yangu alivyohangaika kunifikisha hapa nilipo leo aniombe hela nisimpe kisa kuna msukumo wa mwanamke niliyekutana naye ukubwani hilo haliwezi kutokea. Na kwa niaba ya uyo jamaa yako ni bora ujikatae tu madam.
Eh kama mamako anatumia kila thumni yako unashindwa kufanya maisha yako endelea kuwa mamas boy
 
Alafu umwambie ukweli , usimwache dailema.

Mpaka sasa ni ushamuacha bado kumwambia tu.

Nawaza tu: mwamba akigundua kapigwa chini na mtu aliyekuwa anampenda/aliyekuwa na mipango ya kumueka ndani kabisa , kisa tu Bi mkubwa[emoji848]

Alafu we Dada ,Mimi kama mimi nshakuchukia tayari.[emoji41]

Wacha niendelee kulewa Mimi[emoji482][emoji481][emoji481][emoji481]
Nichukie tu mwanang sikupunguzii hata ladha ya bia mimi
 
Nadhani huyo kijana anashaurika l, mshauri na hiki ndio kiunzi chako cha kwanza madame, hakuna mteremko tu katika mapenzi, ukiona mwanaume wako hana tatizo kabisa basi ndugu watakua na matatizo and vice versa.
 
new gal Usimwache huyo mwanaume esp kwa sababu umesema he is good,na ujue siku hizi good men are hard to find and golden chances never comes twice,we mwenyewe ushasema hujawahi date mkaka wa aina hiyo,sasa unatakaje?

Ni hivi endelea naye huku ukiendelea kusoma mazingira yote na kutafuta namna ya kuifanya influence ya mama kwenu iwe positive badala ya negative,hata ukikosa nyie endeleeni na mipango ya ndoa ila ujitahidi usijkubali muishi pale nyumbani kwao esp baada ya ndoa

Mara nyingi ndoa ni vile mnavyopanga na mkisha kua na ndoa baadhi ya mambo huwa yanakuja na kujiondoa automatikali

Wewe hupaswi kumshauri huyo mwanaume wako aache kuprovide kwao lakini mnaweza kukaa mezani na kupanga financial plans zenu za mkiwa ndani ya ndoa namna ambavyo mtazisupport famiia zenu zote financially na namna ambavyo mtaisustain familia yenu mpya financially ili muweze kubalance mambo vizuri,hakikisheni mna mawasiliano mazuri ya wazi wazi na msifichane chochote,inaweza kusaidia

All the best girl
 
Nadhani huyo kijana anashaurika l, mshauri na hiki ndio kiunzi chako cha kwanza madame, hakuna mteremko tu katika mapenzi, ukiona mwanaume wako hana tatizo kabisa basi ndugu watakua na matatizo and vice versa.
Sawa mkuu
 
new gal usimwache huyo mwanaume esp kwa sababu umesema he is good,na ujue siku hizi good men are hard to find and golden chances never comes twice,we mwenyewe ushasema hujawahi date mkaka wa aina hiyo,sasa unatakaje?

ni hivi endelea naye huku ukiendelea kusoma mazingira yote na kutafuta namna ya kuifanya influence ya mama kwenu iwe positive badala ya negative,hata ukikosa nyie endeleeni na mipango ya ndoa ila ujitahidi usijkubali muishi pale nyumbani kwao esp baada ya ndoa

mara nyingi ndoa ni vile mnavyopanga na mkisha kua na ndoa baadhi ya mambo huwa yanakuja na kujiondoa automatikali

wewe hupaswi kumshauri huyo mwanaume wako aache kuprovide kwao lakini mnaweza kukaa mezani na kupanga financial plans zenu za mkiwa ndani ya ndoa namna ambavyo mtazisupport famiia zenu zote financially na namna ambavyo mtaisustain familia yenu mpya financially ili muweze kubalance mambo vizuri,hakikisheni mna mawasiliano mazuri ya wazi wazi na msifichane chochote,inaweza kusaidia

all the best girl
Thank you love
 
Uyo mama ana itikadi kama za mama diamond ....usimwache uyo mwanaume kisa uyo mama ila ukishaolewa jitahidi mmfungulie biashara awe bize ili asiwasumbue nyie maana kuna wa mama wengine wanatreat watoto wao wa kiume kama waume zao vile na wamama wa hivyo hufanya ndoa kua ngumu
 
Kweli kabisa mamy, ushauri wako nimeupokea
 
Habari wadau, ama kweli yakikufika huna namna utazungumza tu. Mwenzenu yamenifika shingoni na sijui kama nikichukua maamuzi ya kumuacha nitakua nakosea au lah.

Nikiri katika mahusiano yote niliyopitia sijawahi kuwa na mwanaume anayenifanya nijisikie furaha kama huyu kaka.Uhusiano wetu una mwaka sasa. Ni mkaka anayepambana sana, anajali, anahudumia pale anapoweza na kule 6*6 ndo usiseme. Hamna kitu ananificha. In short he is a man in every woman's dream mpaka nikawa naogopa kumpoteza bwana.

Mbembe ikaja baada ya kunitambulisha kwa mama yake mzazi (Eh Mungu). Mama alinipokea vizuri tu lakini siku ya kwanza tu akaniambia ukija niletee bia, mtoto wa kike nikapeleka. Baada ya hapo kila nikiona simu ya yule mama yeye ni kutaka hela tu kwangu. Nikajiuliza ni kisa kaniona na gari au ni nini?

On top of that mama yake hatak apange, kashikilia akae nyumbani eti asiharibu hela kwa kulipa kodi. Mshahara wake wote unatumika kwenye matumizi ya nyumbani, kama anabakiza ni kiasi kdg sana. Sasa kutokana na ukaribu huo kati yao naogopa hata kumshauri asije ona nawaingilia maisha yao.

Napata hofu kuwa ntakua adui kwa yule mama, maana akibadilika kimatumizi ataona mimi ndo kisababishi. Jamaa anapanga mipango ya ndoa lakini naogopa sana kuingia kwenye ile familia. Maana hata akiongea nae kwenye simu akiomba hela akimwambia hana anamwambia ahakikishe anaipata anampa na kijana anafanya hivyo.

Je, nikimuacha huyu kijana mapema nitakuwa nakosea?
Sasa unamuacha kisa anamhumia mama yake na familia?maana sijaona mahali umeandika ana kasoro yeye kama yeye..acha roho mbaya muache amuhudumie mama yake na familia..wewe umekutana naye akiwa mkubwa huyo mama yake na ndg zake wengine ndo wamemfikisha hapo...cha msingi kama unaona kuhudumia familia yake kutadhuru familia mtakayoanzisha mpe mawazo ya kuongeza kitega uchumi ile isiwe shida kuhudumia mama yake...
Halafu wanawake sijui mkoje,sijaoa ila naona kabisa mna roho mbaya na mama zetu...hivi vihela vya bia hizi za buku jero jero vinakupa tabu?mtumie mama ale gambe bana kakuletea mtu anakuliza kunako sita kwa sita😀😀
 
Baba sio lazima nimwage mchele wote. Ukihitaj kujua kwa details follow my lead
 
Pole mkuu,ila wazo la kumuacha mtu ambaye mnaelewana kwenye kila kitu isipokuwa watu wa nje ndo shida sikushauri sana...mimi ni mhanga wa kumpoteza mtu tuliyeivana sana kisa baba yake kagomea dini yangu tukakwama kuoana,mpaka leo sijapata replacement na yeye hajapata na hatuna namna tunaweza kuoana tena..

Unajua kupata penzi siku hizi ni rahisi sana kuliko kumpata mtu mnayeendana katika maisha mengine ya kila siku..usimpoteze huyo jamaa ila mtengeneze indirectly kwa namna unavyotaka pasipo kumforce yaani unampeleka taratibu mpaka anakuwa vile unataka,utanishukuru baadaye...siku ya harusi usinisahau😀
 
Utakuwa unakosea kama hutojaribu kumshauri uone muitikio wake, nini tofauti ya yeye kuwa single na kuwa nawewe kama hata kushauri kama mwanamke shujaa unashindwa? Mshauri kwanza akigoma hapo sasa waweza chukua maamuzi.

Jamaa ni mtoto wa mama kwanza amshauri akapange akishindwa atoke nduki sana
 
Habari wadau, ama kweli yakikufika huna namna utazungumza tu. Mwenzenu yamenifika shingoni na sijui kama nikichukua maamuzi ya kumuacha nitakua nakosea au lah.

Nikiri katika mahusiano yote niliyopitia sijawahi kuwa na mwanaume anayenifanya nijisikie furaha kama huyu kaka.Uhusiano wetu una mwaka sasa. Ni mkaka anayepambana sana, anajali, anahudumia pale anapoweza na kule 6*6 ndo usiseme. Hamna kitu ananificha. In short he is a man in every woman's dream mpaka nikawa naogopa kumpoteza bwana.

Mbembe ikaja baada ya kunitambulisha kwa mama yake mzazi (Eh Mungu). Mama alinipokea vizuri tu lakini siku ya kwanza tu akaniambia ukija niletee bia, mtoto wa kike nikapeleka. Baada ya hapo kila nikiona simu ya yule mama yeye ni kutaka hela tu kwangu. Nikajiuliza ni kisa kaniona na gari au ni nini?

On top of that mama yake hatak apange, kashikilia akae nyumbani eti asiharibu hela kwa kulipa kodi. Mshahara wake wote unatumika kwenye matumizi ya nyumbani, kama anabakiza ni kiasi kdg sana. Sasa kutokana na ukaribu huo kati yao naogopa hata kumshauri asije ona nawaingilia maisha yao.

Napata hofu kuwa ntakua adui kwa yule mama, maana akibadilika kimatumizi ataona mimi ndo kisababishi. Jamaa anapanga mipango ya ndoa lakini naogopa sana kuingia kwenye ile familia. Maana hata akiongea nae kwenye simu akiomba hela akimwambia hana anamwambia ahakikishe anaipata anampa na kijana anafanya hivyo.

Je, nikimuacha huyu kijana mapema nitakuwa nakosea?
Usisahau kuwa kwa sasa wanaume waoaji ni wachache sana
 
Pole sana kwa changamoto hiyo. Lakin siku zote binadamu tunapaswa kusimamia maamuzi yenye kutufanya tuwe na furaha na amani kwani ndo kila kitu kwenye maisha.

Unaweza ukatenga muda wa kuongea nae lakin akakuahidi atabadilika labda mkishaona. Swali je mmeshaoana na asibadilike what's next?

Kuna watu au watoto wanadhani kufanya hivyo au kujitoa kupitiliza ni kumfanya mzazi afurahi lakin kumbe sio hivyo.
Tunapaswa kujitoa kwa vitu vya msingi. Wazazi ni Mungu wetu wa pili tunapaswa kuwajibika kwao lakn si kwa utaratibu huo.

Nitakupa mfano nina rafiki angu mmoja alikuwa na mahusiano na jamaa yake. Yule bwana alikuwa haambiwi kitu kuhusu familia yake. Hata kama hana hela bora alale njaa lkn familia yake ile that's good hata rafiki angu aliapreciate hilo.Yule bwana alikuwa na dada ake alifariki akaacha watoto 2 wadogo yeye akabeba jukumu la kusomesha wakati huo kaka yake mkubwa alikuwa ameoa mwanamke aliyekuwa na watoto 3 kabla.

Yule bwana akawa anashauriwa sasa na best angu watoto walee kulingana na uwezo wako. Akawa anajibu ni kweli ili wajifunze. Aliwapeleka boarding wa kike alikuwa yuko darasa la saba .Watoto walienda shule wananunuliwa maji ya katoni Mazagazaga wakati bwana uwezo hana anaunga unga.Na alipokuja anakwama basi best angu kumfurahisha akawa anajitoa kukusupport jamaaa. Bado yule kaka ake mkubwa akikwama jamaa yake atoe support. Basi best angu akawa anamshauri kwa mwendo huu hutakuja kufanikiwa sababu hujifikirii hata wewe halafu pia unajitoa hata kwa vitu ambavyo sio vya msingi.

Kwani hiyo hela yenyewe ya kuwapeleka bording anakopa wakati hana uhakika wa kipato,,akamshauri hiyo bora uweke kwenye biashara japo kwa mwaka mmoja ukishapata uhakika ndo watoto uwapeleke bording jamaa akagoma. Basi bwana maisha Yao yakaenda binti kufika kidato Cha tatu kaacha shule kaenda kuishi kwa mwanaume.

Baada ya kila kitu kuharibika ndo akamwambia best asieee najua ningesikiliza ushauri wako. Best angu kuona mwanaume ambaye hashauriki aliamua kufanya maamuzi magumu .

Ushauri wangu; Simamia msimamo utaoona kwako unafaa kamwe usiishi kwa kumfurahisha mtu. Kama Leo anamsikiliza mama yake hivyo basi hata mkiingia kwenye ndoa bado ataendelea kufanya hivyo.

Japokuwa sheria haisemi kuwa mtoto anawajibu wa kumelea mzazi ila kutokana na tamaduni ni wajibu wetu kuwasaidia ila kwa mambo ya msingi.Hata kama ni bia basi isiwe kuendekeza.
 
Back
Top Bottom