Je, nikimuacha nitakuwa nakosea?

Je, nikimuacha nitakuwa nakosea?

Kama utapendelea pitia story za iddimakengo hopefully utajifunza kitu.
 
labda nkushauri mwenzang.....jarb kumkalisha chini mpange maisha yenu kwanz ukion unavyo jarb kumshauri kaelekei...hapo itabidi uchukue maamuzi mwenyew kama mwanamke...ila kama mama yake kuona amebadilika kwang mm naona sio mbaya since wew ndie mama yake kwa sas na unatakiwa umbadilishe positively
Asante kwa ushauri mpendwa
 
Habari wadau, ama kweli yakikufika huna namna utazungumza tu. Mwenzenu yamenifika shingoni na sijui kama nikichukua maamuzi ya kumuacha nitakua nakosea au lah!

Nikiri katika mahusiano yote niliyopitia sijawahi kuwa na mwanaume anayenifanya nijisikie furaha kama huyu kaka.Uhusiano wetu una mwaka sasa. Ni mkaka anayepambana sana, anajali, anahudumia pale anapoweza na kule 6*6 ndo usiseme. Hamna kitu ananificha. In short he is a man in every woman's dream mpaka nikawa naogopa kumpoteza bwana.

Mbembe ikaja baada ya kunitambulisha kwa mama yake mzazi (Eh Mungu). Mama alinipokea vizuri tu lakini siku ya kwanza tu akaniambia ukija niletee bia, mtoto wa kike nikapeleka. Baada ya hapo kila nikiona simu ya yule mama yeye ni kutaka hela tu kwangu. Nikajiuliza ni kisa kaniona na gari au ni nini?

On top of that mama yake hatak apange, kashikilia akae nyumbani eti asiharibu hela kwa kulipa kodi. Mshahara wake wote unatumika kwenye matumizi ya nyumbani, kama anabakiza ni kiasi kdg sana. Sasa kutokana na ukaribu huo kati yao naogopa hata kumshauri asije ona nawaingilia maisha yao.

Napata hofu kuwa ntakua adui kwa yule mama, maana akibadilika kimatumizi ataona mimi ndo kisababishi. Jamaa anapanga mipango ya ndoa lakini naogopa sana kuingia kwenye ile familia. Maana hata akiongea nae kwenye simu akiomba hela akimwambia hana anamwambia ahakikishe anaipata anampa na kijana anafanya hivyo.

Je nikimuacha huyu kijana mapema nitakuwa nakosea??????
Ukishamuacha naomba unitag....!!
 
Wew dili na mpenzi wako...nduguu, jamaa, marafiki wa huyo mwanaume sio consern yako cha msingi kuwa nao makini.
 
Habari wadau, ama kweli yakikufika huna namna utazungumza tu. Mwenzenu yamenifika shingoni na sijui kama nikichukua maamuzi ya kumuacha nitakua nakosea au lah.

Nikiri katika mahusiano yote niliyopitia sijawahi kuwa na mwanaume anayenifanya nijisikie furaha kama huyu kaka.Uhusiano wetu una mwaka sasa. Ni mkaka anayepambana sana, anajali, anahudumia pale anapoweza na kule 6*6 ndo usiseme. Hamna kitu ananificha. In short he is a man in every woman's dream mpaka nikawa naogopa kumpoteza bwana.

Mbembe ikaja baada ya kunitambulisha kwa mama yake mzazi (Eh Mungu). Mama alinipokea vizuri tu lakini siku ya kwanza tu akaniambia ukija niletee bia, mtoto wa kike nikapeleka. Baada ya hapo kila nikiona simu ya yule mama yeye ni kutaka hela tu kwangu. Nikajiuliza ni kisa kaniona na gari au ni nini?

On top of that mama yake hatak apange, kashikilia akae nyumbani eti asiharibu hela kwa kulipa kodi. Mshahara wake wote unatumika kwenye matumizi ya nyumbani, kama anabakiza ni kiasi kdg sana. Sasa kutokana na ukaribu huo kati yao naogopa hata kumshauri asije ona nawaingilia maisha yao.

Napata hofu kuwa ntakua adui kwa yule mama, maana akibadilika kimatumizi ataona mimi ndo kisababishi. Jamaa anapanga mipango ya ndoa lakini naogopa sana kuingia kwenye ile familia. Maana hata akiongea nae kwenye simu akiomba hela akimwambia hana anamwambia ahakikishe anaipata anampa na kijana anafanya hivyo.

Je, nikimuacha huyu kijana mapema nitakuwa nakosea?
My dear kwa unavyomjua huyo mwanaume wako anaweza kujisimamia? Maana kushauri mwanaume ambae hana msimamo ni wa kupelekeshwa na mama[emoji848] utajichosha bure. Anaweza kubali ushauri wako sababu hataki kuachana na wewe but Utekelezaji zero, na ukiolewa nae ndo utakinywea.

Nakwambia from my experience, nilipata mkwe mwenye tabia kama za huyo wako.... siku ya utambulisho ananisifia "Masha Allah mtoto mzuri, umeumbika shape kweli kweli hapa mwanangu kapata". Baada ya hapo akawa mtu wa kuagiza ninunulie hiki, ninunulie kile kwa ufupi simu za pesa pesa zikazidi haswaa (imagine mama wa mchumba anakwambia umnunulie kitu cost yake laki7[emoji849]) . Kumbe ashajua nafanya kazi gani so familia nzima wanaamini mtoto wao kanipendea hela[emoji30][emoji30]
Nikamkaushia tena vingine nikawa namjibu sina hela, baadae mwanae alivotaka tufunge ndoa akakataa eti asubiri afanye kwanza maendeleo nyumbani. Kijana akagoma keshaamua kuoa, tukafunga ndoa mkoa tuliopo (sio kwao) though mama mtu alikuja harusini kinafiki tena kwa kuchelewa...... from there hakuna mahusiano mazuri kati yetu na familia yake.
Na huu ni mwaka wa Sita wa ndoa ila hatuna mtoto.
So my dear tumia akili yako effectively, kama utaweza mikiki na mengine yasojulikana endelea na huyo mwanaume.
 
Dah love nmesoma mkasa wako umenisisimua hatari. Sema mi watoto wala sio muhimu nkipata haya nikkosa haya mana tayar mungu alishanjaalia. Ila nimeyachukua mawazo yako nina imani yataniongoza
 
Hongera, kumbe tayari mna watoto... basi olewa nae tu. Za kuambiwa changanya na zako pia, maana wewe ndio unamjua mtu wako
 
wewe tako huna mpaka unakuwa na wasiwasi wa kumuweka kikao njemba yako? unaogopa nini wakati wewe ndio mwenye mbususu? wanawake sometimes bwana mnajishusha wenyewe
 
Wewe elewa ya kwamba, 'mpenzi' wa kwanza wa mwanaume ni mama yake na 'mpenzi' wa kwanza wa mwanamke ni baba yake...

Wewe una sehemu kwa moyo wake na wazazi/mzazi wake hivyo hivyo...

Wewe kama wataka jiondoa, jiondoe kwa sababu zako tu na sio hizo unataja...

Sijui kwa nini watu huwa hawaelewi neno 'upendo'!!!!
 
Back
Top Bottom