Je, nikweli kwamba Rais Samia amemtuma mkurugenzi wa halmashauri ya Morogoro kuwaadhibu walimu watakaoshindwa kutoa hela ya mwenge?

Je, nikweli kwamba Rais Samia amemtuma mkurugenzi wa halmashauri ya Morogoro kuwaadhibu walimu watakaoshindwa kutoa hela ya mwenge?

kuchangia mwenge huwa ni kwa watumishi wote walioko kwenye halmashauri husika, tasisi binafsi na wafanyabisahara.
 
Mkurugenzi wa halmashauri ya Morogoro ndugu Jeshi Lipembe amesema kwamba ameagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwaadhibu walimu na watumishi wa sekta ya afya watakaoshindwa kutoa mchango wa mwenge (10,000/=)

Aidha ameagiza walimu wakuu, wakuu wa shule, na viongozi katika idara ya afya kuorodhesha na kumtumia majina ya watumishi watakaoshindwa kutoa kiasi hicho cha fedha.

Amesema wakuu wote wa shule watakaoshindwa watavuliwa nyadhifa zao na walimu watanyimwa fursa ya kusimamia mitihani huku akiahidi kuwashughulikia watumishi katika kada ya afya ambao hawata toa.

Je, nikweli ameagizwa na Mh Rais au anafanya tu kwa utashi wake? Kwanini anatumia jina la Rais?
Haya maujinga yapo kila mwana kwa wafanyakazi wa halmashauri ambao wapo chini ya mkurugenzi sijawahi toa pesa yoyote wala kushona vitenge vyao..
Na hamna walilowahi nifanya
 
ili swala waliweke kwenye mkataba wa kazi sasa ...mm nmewahi kuhoji kwann nitoe mchango wa mwenge simu zikaanza
 
Back
Top Bottom