Je, niliyestushwa na hii kauli 'tata' ya Naibu Katibu Mkuu CCM Mpogole ni peke yangu tu au tupo wengi? Mama kuwa makini sana!

Kwani uongo?

Huyo Ni rais wa kusimika tu sio wa kupitia sanduku la kura.

Halafu tuko kwenye awamu tano bado huyu kakaimu tu.
Mawazo ya mjinga mmoja asiye jua chochote kuhusu katiba inasema nini ila anajifanya kujua, poleni chuma chenu kimesha liwa na funza huko msitupigie kelele zenu
 
Apange safu yake tuu hata huyo mpogolo anajifariji tuu ikibidi fukuza vinginevyo watakusumbua but najua JK mzee wa mipango atamsaidia kuweka mambo sawa.
 
Mkuu naomba nitofautiane na wewe kidogo kuhusu hilo la pili. Ni kweli CCM ilianza kuyumba enzi za JK kwani aliondoa Baraza la ushauri na kupunguza nguvu ya Halmashauri Kuu ya chama ambayo ni chombo pekee kinachotunga sera zitakazotekelezwa na serikali ya CCM. Pili aliingiza kwenye Kamati Kuu ya CCM watu ambao hawakuwa na uzoefu katika uendeshaji wa chama ( party political organisation). Matokeo yake ndiyo hayo ya JK kuona CCM inakufa, akaitwa Kinana, Nape wakashirikiana na Mangula kuokoa jahazi.

Awamu ya Tano CCM ilizidi kudhoofika sana kwa sababu zifuatazo;
1. Halmashauri Kuu ikazidi kupungunzwa nguvu kwa kupunguza idadi kubwa ya wajumbe wake na vikao vyake vikawa ni vya siku moja au mbili tu.
2. Uingizaji wa wanachama kiholela bila kuwasaili kujua kama wanaijua na wanaikubali ITIKADI ya CCM. Mfano ni Polepole na Bashiru na wengine wengi kiasi cha kwamba CCM Maslahi ni wengi zaidi kuliko CCM Asilia.

Kwa kumalizia, CCM kama chama cha siasa kiko hoi bin taabani. Kimepoteza ule moyo wake wa kiitikadi. Ni wakati sahihi wa Mwenyekiti Mpya kuiangalia hali hii kwa makini aanze kukijenga upya chama aondoe mamluki na CCM maslahi wote, aunde Sekretariet mpya iogozwe na makada wazoefu, airudishie nguvu na heshima Halmashauri Kuu na Kuimarisha uongozi na uendeshaji wa chama kutoka ngazi ya Matawi hadi Taifa.
 
Hahahahah daah
 
Good
 
Mimba changa
 
Mawazo yako at face value.
 
Ndani ya CCM kuna shida.

Anaetakiwa kubaki ni huyu mzee Mangula wengine wote wakuondoa.

Chama kirudi kwa Nchimbi, Nape, January.

Kinyume na hivyo, Mh. Mama Samia ana kwenda kufanyiwa zengwe.
Ramli huwa hazijibu
 
Atakaposuka kikosi chake ataanzisha chuki nyingine ya wazi ambayo sasa kwake nayo itamsumbua kuliko wanaojificha na kusemea pembeni bila madhala kuluko kujitengenezea madhala yeye mwenyewe.
 
Hiyo ni tafsri yako tu

Hakuna kitu cha kushangaza hapo.
 
Umenistua aisee. Usiwe unataja taja huyo shetani
 
Woote mnaongea as if mama peke yake ana mvuto kwa wana CCM!

Hivi kati ya mama yenu na hao waandamizi ndani ya #CCM ni nani ana mvuto wa kukiweka chama mahali pake?

Hao kina Nchimbi,Kikwete,Nape,na vurugu zao zingine si ndio hao waliokuwa tayari wamekiuwa chama?

Kuna mambo ndani ya #CCM akiyapindisha sasa hivi itakigharimu chama hicho vibaya sana 2025.

Sio mnaongea tu,utadhani mnaoongelea CHADEMA.

#CCM ni kitu ingine..
 
 
JPM hakurudisha uhai wa CCM. Alichofanya ni kutumia vyombo vya dola kufanya siasa yeye peke yake na CCM na kuzuia vyama vingine kufanya siasa.

Alizuia vyama vya upinzani kufanya siasa na kuwafanyia viongozi na wanachama wa vyama hivyo kila aina ya hujuma inayoweza kufanywa duniani!
 
Unaropoka pumba tu!

Ficha chuki zako kwa mama. Yeye ndiye raisi wa JMT na mwenyekiti wa CCM. Watanzania tunampenda. WanaCCM tunampenda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…