JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Je, unaridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Mamlaka katika kushughulikia Matukio na Taarifa za Rushwa na Ubadhirifu nchini?
Unaweza kutoa maoni yako na kupendekeza njia Bora za kupambana na Rushwa kupitia Mjadala utakaoendeshwa na JamiiForums Alhamisi Mei 30, 2024 Saa 12:00 Jioni hadi 2:00 Usiku kupitia XSpaces.
Ili kushiriki mjadala bofya kiungo hiki JF Spaces Link x.com
Pia unaweza kuweka maoni yako kwenye uzi huu na yatasomwa siku ya mjadala.
=======
Ili kufanikisha mapambano dhidi ya Rushwa, TAKUKURU inasisitiza mambo kadhaa:
Kuongeza au kuujengea Umma uelewa kuhusu mapambano dhidi ya Rushwa, Kubadili mitazamo ya walengwa wa Elimu inayotolewa au kuwajengea walengwa hao hisia ya kuichukia Rushwa na kuamsha ari yao ya kukabili rushwa.
Kushirikisha na kuhamasisha Wadau kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya Rushwa (mmoja mmoja au katika kikundi ama Taasisi), kuhamasisha na kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa, kubadilishana taarifa za msingi kuhusu vitendo vya Rushwa.
Kuhamasisha na kutoa ushahidi wa vitendo vya Rushwa, kuchukua hatua stahili na stahiki dhidi ya wanaojihusisha na Rushwa (uchunguzi na mashtaka) au kuhamasisha kuacha kushiriki vitendo vya Rushwa.
Mdau, unaridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Mamlaka kushughulikia Matukio na Taarifa za Rushwa na Ubadhirifu nchini? Shiriki kutoa maono katika Mjadala utakaoendeshwa na JamiiForums, Alhamisi Mei 30, 2024 Saa 12:00 Jioni hadi 2:00 Usiku kupitia XSpaces
---
DKT. BARUANI MSHALE (Mkurugenzi wa Mafunzo na Mikakati Twaweza):
Kuna Mazingira ambayo yametufanya tuikubali Rushwa kuwa sehemu ya Maisha yetu
Mfano, Dereva wa Gari akikamatwa au akisimamishwa na Askari wa Usalama Barabarani, anachofanya ni kuandaa kitu kidogo kwa ajili ya kumalizana na Afisa huyo bila kujali ana kosa au la
AHOBOKILE MWAITENDA (Mshauri wa Fedha na Kodi):
Tafiti nyingi Duniani zinaonesha kwenye Nchi nyingi ambazo kiwango cha Umasikini ni kikubwa, kiwango cha Rushwa nacho pia ni kikubwa
Kuna mazingira mapya ya #Rushwa yanatengenezwa kitaalam tunaiita hali hiyo “fraud”. Mfano tenda inapotolewa anayehusika anaichelewesha makusudi ili gharama za mradi zipande kisha malipo yakitolewa kuna Watu wanafaidika
JACKSON MMARI (Meneja wa Fedha na Utawala WAJIBU Institute):
Rushwa ina viwango na ina vitu vinavyoambatana au kuingiliana
Baadhi ni utakatishaji Fedha, Ufadhili wa Ugaidi, Usafirishaji haramu wa Watu, Usafirishaji wa Fedha
Rushwa zipo ndogondogo mfano za Huduma, zipo Rushwa zinazohusisha Taasisi na zipo Rushwa kubwa, mfano zinazohusisha tenda zenye thamani ya bilioni, trilioni
Kuna Rushwa kwenye Siasa, baadhi ya Watu wanaamini Mgombea anapotoa Fedha ili apate Madaraka ndio Rushwa pekee lakini kuna Rushwa nyingine za ndani ambazo zinatokana na masuala kama Utendaji wa ndani kwa jumla
Serikali imekuwa ikipambana na Rushwa Nchini, pamoja na yote kuna changamoto ya kukosekana kwa mikakati Madhubuti ya kumshirikisha Mwananchi wa kawaida katika mapambano hayo ya Rushwa
Utafiti wangu niliofanya nimebaini tatizo la Rushwa linaanza na muono wa Mwananchi mwenyewe, Mazingira yanaonesha anakuwa hatarini kutoa Rushwa kutokana na Mazingira na tabia yake. Huku Mitaani kuna tabia nyingi ambazo zinafanyika Mtu anakuwa anajitengenezea Mazingira ya kutoa Rushwa bila mwenyewe kujua
Kuna tabia ya kushuruku kupita kiasi, mfano Mtumishi wa Serikali anaweza kutimiza wajibu wake lakini wewe mhusika unamshukuru kiasi kwamba anaona alichofanya siyo wajibu wake bali ametoa msaada kwako.
Kuna Rushwa ya Kisiasa, Wananchi wanatakiwa kuliangalia hili eneo zaidi kwa kuwa wengi hawana ufahamu mzuri kuhusu kinachokuwa kinaendelea.

Rushwa inaweza kutokea kwa mtu yeyote na kumhusisha yeyote, inaweza kubadilibadilika, hivyo inaweza kuwa ngumu kupambana nayo kwa kuwa inatokea kwa kificho.
Rushwa ina gharama nyingi, mtu au watu wanaweza kutumia kukandamiza wengine, Imani ya Wananchi kwa Serikali inaweza kupungua, inaweza kuathiri Uchumi kwa kuwapendela watu wachache na wengi wakakosa.
ADO SHAIBU (Katibu Mkuu ACT Wazalendo):
Tunatakiwa kuangalia vyama vyetu ya Siasa vina maslahi gani dhidi ya Rushwa, mfano huko nyuma Rais wa Awamu ya Tano aliwahi kutaka kurasimisha Rushwa inayoombwa na Askari wa Barabarani ni halali
Uchunguzi ukifanywa kwenye vyama vya Siasa utaonesha bado hatujawa na msukumo mkubwa wa kupambana na Rushwa
Huko nyuma Vyombo vya Habari vilikuwa vikiripoti sana kuhusu Rushwa, magazeti yaliandika na kuripoti matukio ya Rushwa ndogo na kubwa, hivyo bila kuwa na Vyombo vya Habari vyenye Uhuru itakuwa ngumu kupambana dhidi ya Rushwa
Tunatakiwa kuangalia hali ya Mahakama zetu, tukiziboresha zitasaidia Wananchi kupata haki na kuwa na imani na Mahakama, pia tunatakiwa kuangalia taasisi zetu za Kirasia, ni muhimu ziwe huru katika kufanya kazi zao
Nini kifanyike kudhibiti Rushwa? Hali ya Umma wenyewe inatakiwa kuangaliwa, inatakiwa kutambua jukuu hilo la kupambana na Rushwa ni lao pia isionekane ni jukumu la Watu fulani.
JACKSON MMARI (Taasisi ya WAJIBU):
Kuondoa mazingira ya Rushwa kwenye Jamii, Wananchi wanatakiwa kujitambua na kuwa tayari kushiriki katika mapambano dhidi ya Rushwa
Wananchi tunawakilishwa na wawakilishi wetu kwenye masuala ya kiutawala, hivyo basi Wananchi wanatakiwa kuwa tayari kuwalinda watu wanaowawakilisha, mfano kama ni Mbunge au Diwani au Bunge, wawe tayari kusimama ya kile wanachokitaka hawa wawakilishi wao, hilo litasaidia kupambana na Rushwa
ZOBOGO (Mdau): Naona kuna ufu wa dhamira kwa Watanzania wengi, watu wengi hawashiriki katika mapambano kwa kuwa hawana nafasi na hawana dhamira
Tunatakiwa kubadili mitaala yetu kuanzia ngazi ya shule, Watoto wanatakiwa kuambiwa Rushwa sio kitu kizuri kuanzia ngazi ya chini.
Mtu anayechukua Rushwa hafikirii kizazi kichacho, anaifikiria familia yake au yeye mwenyewe binafsi.
Wananchi wanatoa kodi lakini matumizi ya kodi hiyo hayatumiki vizuri, baadhi ya Nchi za wenzetu Wananchi wanaona kodi zao zinavyotumika tofauti na huku kwetu
Huku kwetu (Tanzania) ukishakuwa kiongozi mhusika anaona amemaliza matatizo yake yote, pamoja na hivyo sisi wenyewe tuanze unafiki, hatujapata hizo nafasi ndio maana tunasema hapa, tukipata nafasi tutafanya kama wanavyofanya hao tunaowasema
Mfano mtu akiajiriwa TRA, ikapita mwaka mmoja bila kuwa na maendeleo yake kuonekana wazi Jamii itaanza kuhoji anafanyaje kazi TRA kisha hana maendeleo? Hiyo inamaanisha au inaonesha Rushwa ipo kwenye vichwa vyetu na kama tumeiridhia
VALENCY (Mdau):
Wanaopatikana na Rushwa wanawajibika vipi, mfumo wetu unaonesha wanaopatikana na hatia ya kuiba kuku adhabu yao ni kubwa kuliko wanaoiba fedha nyingi, wanaishia kushushwa cheo au kuhamishwa kituo cha kazi
MAGODE75 (Mdau)6: Mazingira ya Rushwa hayajatupa uwoga, mfano kijana wako akiwa na ajira ya mshahara mdogo, akijenga nyumba ya mamilioni ya fedha ndani ya muda mfupi huwezi kuhoji badala yake utafurahia.
BA’JOHNIE (Mdau):
Tunashuhudia Rushwa za waziwazi barabarani, mfano mkiwa kwenye Daladala mkasimamishwa na Askari wa Barabarani, Kondakta Anashuka anaenda kumpa Tsh. 2,000 na abiria wanaona na hakuna kinachofanyika. Ikitokea Askari anataka kuandika faini, utasikia abiria wanamlalamikia Kondakta kuwa ampe Tsh. 2,000 ili safari iendelee.
Tunatakiwa kuiondia Rushwa kwenye taswira za fikra zetu, hata kama watafunga kamera kama wanavyosema, wahusika watatafuta njia nyingine za kutoa na kupokea rushwa, tunatakiwa kuiondoa kwenye jamii kuanzia chini.
ISIHAKA MCHINJITA (Waziri Mkuu Kivuli ACT Wazalendo):
Hakuna kinachotokea kwa wala Rushwa, hilo linafanya Mwananchi ajue kuwa hata akiripoti hakuna kitakachofanyika
Miradi mikubwa ipo mingi imebebwa katika mazingira ya Rushwa kama ilivyo kwa tenda kubwa pia zimebebwa katika hali hiyo.
Katika Nchi hii, tunavyokwenda kila mtu anajua Rushwa ni sehemu ya Maisha yetu, ni kama tumeikubali na tunaishi nayo.
TAKUKURU inapambana na Rushwa lakini yenyewe sio sehemu ya Jamii ndio maana Mwananchi anaona hakuna umuhimu wa kushiriki kutoa taarifa ya Rushwa kwao
Naamini ili mafanikio yapatikane ni hadi pale ambapo Wananchi wataona kuna maamuzi yanafanyika na Uwajibikaji unakuwepo