Je, nini kifanyike kuboresha mipango miji ya Manzese? Napendekeza walipwe fidia na watimuliwe wote

Hatujafikia hiyo hatua. Tuweke mikakati ya kunufaika na rasilimali asilia kwanza, mapato yake ndio yatafanya hiyo kazi ya kuwajengea wananchi.
 
Naunga mkono hoja..

Kuna maeneo Dar es salaam yalitakiwa kuvunjwa na watu wahamishwe na miji ijengwe upya kulingana na hali halisi, sijui hili linatushinda wapi.. Kama ni nyumba, zijengwe upya kwa ramani za kisasa na mipangilio mizuri then watu wakopeshwe kwa masharti nafuu...
 
Wakat wanajenga hizo ghorofa wakazi wataishi wapi?
 
Kuibuka Manzese nyingine haizuiliki kwa Tanzania hii.
 
Kwanza wajenge majengo ambayo yatatumika kwa muda na hizo familia za hao wakazi.....baada ya kukamilika kwa ujenzi warudishwe kwenye makazi yao mapya yaliyopangwa....
 
Napendekeza nyumba zote za Manzese zifanyiwe tathmini na wamiliki wake walipwe fidia ili kupisha uboreshaji wa mandhari ya jiji, ile takataka inayoitwa Manzese haivumiliki, no way!
View attachment 1320572
Au zitumie stringent development control codes. With a certification system.

1) Yatengwe maene ya familia single family (kwa ajili ya familia moja na waruhusiwe kujenga tu 35pc ya kiwanja(plot coverage) Ukitaka more space iwe g+1

2) Maeneo ya Biashara yatengwe na warudhusiwe kujenga na kujaza viwanja kwa asilimia 100..lazima waincorporate a
maeneo ya kuegesha magari.

3) yatengwe maeneo ya biashara ndogo ndogo (Forodhani style bazaar) kwa ajili ya wamachinga... Preferably pembezoni mwa Soko kuu pande zote mbili za barabara ya mwendo kasi.

4) Bajaji ziwe ndio main and only mode of public transportation kwa njia zote za ndani kwa maana ya kuunganisa Morogoro road na Morogoro Connect. Na Mburahati na mabibo kwa upande wa pili.

5) Boresha BRT na Ua Daladala Morogoro Rd. Zipite njia zozOte parallel na Morogoro rd. Ie Morogoro Connect na Mabibo ba Mburahati.

#patapendeza na huenda pakawa posh kuliko tunavyopadhania. Itakuwa organic layout.. lakini itakuwa Bora.. imagine the new kind of Stone town in the making.
 
Mawazo mazuri sana. Inahitajika ujasiri na political will kufanya maamuzi haya na utekelezaji wake
 
Suala la mipango miji kwa nchi yetu ni changamoto sana, japo wataalamu wapo ila sijui tunakwama wapi.
 
Mawazo mazuri sana. Inahitajika ujasiri na political will kufanya maamuzi haya na utekelezaji wake
Utekelezaji wake unaanzia shule kabisa
Lazima tuwe na.mfumo wa elimu kwa umma na massive campaign ya kubadilisha fikra. Tatizo la mipango miji holela chimbuko lake ni mindset.

Watu wanaishi Miji kwa taratibu za kijijini. Kijijini Ukipata mazao mengi ghafla hata kuwa umepanga kujenga ..Basi unaenda kwa baba unaomba kujenga as if yeye ndio Village Council.. anakusontea pahali unaanza kujenga.

Sasa na mjini mtu akipata hela ya ghafla tu mbio kununua eneo ili ajenge. Na unabaki unashangaa mbona watu wamesoma lakini wanakaa squatter areas!? Ni vile vile ni wasomi wenye mindset za kijijini. Inabidi uondoe ukijiji Kwanza katika akili zao ndio unaweza kuwa na miji Bora.

Kingine Makazi ya asili haimaanishi watu kwenda kila sehemu kuvamia na kujikatia maeneo Kisha yanaqualify Kama maeneo ya asili. Maeneo ya asili ni yale tu yalitambulika au kuwepo kabla ya sheria kutungwa. We una miaka 28-40 msukuma unakutwa Kibindu, Handeni unasema hapo ulipokutwa ni makazi yenu ya asili!?

Kwa kifupi baada ya Sheria iliyotambua makazi ya asili na customary ownership wote waliokwenda kuacqure land bila kupewa na kijiji kwa kutuata utaratibu wanapaswa wao.kuwajibishwa au Halmashauri za kijiji zote nchini kuwajibishwa kisheria kwa kuvuruga nchi.

Nasema hayo maana vijiji ndio footprint ya mji. Ni vijiji ambavyo baadae vitakua na kuwa miji. Ukiweka msingi mbovu utapata.miji mibovu au itakuwa gharama kubwa Sana kuiboresha.
 
Kweli kama inawezekana baadhi ya nyumba zivunjwe ili kupisha barabara maana haiwezekani watu waishi kama wako kwenye makambi ya wakimbizi
 
Bonge moja la idea...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…