Je, niolewe naye? Baba yake alizaa na Mama yangu

Je, niolewe naye? Baba yake alizaa na Mama yangu

Sasa huyo dadako na mumeo wataitanaje? Shemeji au kaka na dada? Mie sikushauri uolewe nae manake ni kakako pia.
 
Mimi nafikiri kwa kuwa mama yako alishawahi kuzaa na baba yake huyo jamaa,hapo mnakuwa mmeunganishwa kama ndugu,kwani mdogo/dada yako aliyezaliwa toka kwa baba yake na huyo jamaa ni ndugu yake/half blood na yule jamaa na wewe pia una 1/2 blood na ndugu yako so ki-maadili si busara wewe kuoana na huyo jamaa labda kama mngekuwa hamjuani.
 
Yaani naona unataka kuolewa kwenye familia isiyo familia kamili.

Sasa wewe na yeye wote familia zenu zimejaa drama sana kwanini usitafute mwanaume anayetokea katika familia iliyotulia ili watoto wako nao wakue kitofauti nawe.

Duh embu achana nae huyo maana mtaishia kama wazazi wenu
 
Wakuu wa Jukwaa,

Heri ya Mwaka Mpya 2012.

Kuna Mwanaume ambaye ametokea kunipenda sana, nami nampenda sana ingawa hatujafikia hatua ya mahusiano ya kimwili. Napenda kumwita A.

Kinachonitatiza ni kuwa enzi za ujana wao, Baba yake A (Namwita B) na Mama yangu walizaa binti ambaye tumpe jina C. Sasa mimi na C tunashare Mama lakini Baba zetu tofauti. C ni dada yangu, yeye ni mkubwa mimi ni mdogo. Wazazi wangu wote walifariki. A na C hawajawahi kufahahamiana hadi walipokutana hivi karibuni na kutambulishwa na baba yake yaani B katika harusi ya Binti mwingine wa baba yake A (yaani baba B) ambaye alizaa na Mwanamke mwingine tena.

Kwa upande wa A, yaani Mwanaume tunayependana amelelewa na familia nyingine toka utotoni ambayo mama yake Mzazi na A aliolewa na Baba mwingine. A ana ndugu zake huko waliolelewa pamoja. Hii ndiyo familia yake ya sasa.

Sasa swali langu kwenu wana MMU, je mimi naweza kuolewa na Mwanaume huyu yaani A?

Naomba kuwakilisha.

Hapo kwenye red, baba B ni nani? umenichanganya! inakuwa kama vile baba B ni babu yao A na C! ndio hivyo au vipi?
 
Sasa huyo dadako na mumeo wataitanaje? Shemeji au kaka na dada? Mie sikushauri uolewe nae manake ni kakako pia.

Familia yangu na yake hazijuani kabisa na zina majina na malezi na historia tofauti. Kama nilivyoeleza A na C wamekutana hivi karibuni ukubwani tu.
 
Mimi nafikiri kwa kuwa mama yako alishawahi kuzaa na baba yake huyo jamaa,hapo mnakuwa mmeunganishwa kama ndugu,kwani mdogo/dada yako aliyezaliwa toka kwa baba yake na huyo jamaa ni ndugu yake/half blood na yule jamaa na wewe pia una 1/2 blood na ndugu yako so ki-maadili si busara wewe kuoana na huyo jamaa labda kama mngekuwa hamjuani.

Unaweza kunifafanulia Kimaadili ya namna gani?
 
Yaani naona unataka kuolewa kwenye familia isiyo familia kamili.

Sasa wewe na yeye wote familia zenu zimejaa drama sana kwanini usitafute mwanaume anayetokea katika familia iliyotulia ili watoto wako nao wakue kitofauti nawe.

Duh embu achana nae huyo maana mtaishia kama wazazi wenu

Sasa jamani ni Drama zipi hizo tena? Kwani familia nyingine zilizotulia zikoje?

Kuhusu kutafuta, naamini ndoa inapangwa na Mungu. Nitatafutia wapi huyo Mwanaume na vipi?
 
Babu na wewe, una tabu kweli wewe . . . . lol

Iko hivi Babu DC Washington . . . Nimepeleleza na nimegundua yafuatayo:

Baba yake A yaani (B), kwa sasa japo ni mtu mzima sana, kamwoa Binamu yake, binti mbichi kabisa huko kijijini.

Baba Mlezi wa A ambaye ndo wa familia yake wa sasa, ni Muislamu na yeye anasema kama mimi na yeye A hatuko katika shina la ndugu walionyonya ziwa moja, then haina tabu na anasema Binamu ni Rukswa kumuoa kidini na Kimila. Bado nahitaji maelezo hapo maana sijaelewa kivileeee

Dada yangu yaani C, naona hana Kipingamizi, ila na yeye hajui ndugu wengine watasemaje hasa hawa watoto Liluki wa baba yake A yaani (Mzee B).

Hili la Kibiblia ndo napenda sana nilifahamu kwa Kina maana nami napenda kwenda Mbinguni, lakini sijaweza kulielewa kama kuna makatazo au hapana.

Dada na Kaka zake A katika familia yake hawana kizuizi na wanasema wako poa.

Kwa upande wa ndugu zangu ukiacha dada yangu C. Hakuna ambaye nimeongea naye. Ngoma nzito bado kuliko maelezo.

Una visa wewe dada......!!

Hivi kwa maelezo hayo...ngoma bado nzito katika suala lipi tena??

Halafu hebu nisaidie...hivi moyo wako unapodunda unakueleza nini????....Yes, Yes, Yes ...au No, No, No.....????

Babu DC!!
 
Moyo unadunda YES mara kisha NO mara moja.

Babu kama hoja zinavyokingana hapa jamvini na mimi ndivyo ninavyochanganyikiwa.

Lakini nampenda sana Brother. Ni "Bonge la Bwana" haaaa haaaa
 
Moyo unadunda YES mara kisha NO mara moja.

Babu kama hoja zinavyokingana hapa jamvini na mimi ndivyo ninavyochanganyikiwa.

Lakini nampenda sana Brother. Ni "Bonge la Bwana" haaaa haaaa

Ngonja nikusaidie kidogo kuweka hitimisho.....

Lakini nampenda sana Brother. Ni "Bonge la Bwana" haaaa haaaa[

Kilichobaki muulize huyo bwana naye anasemaje...!!
 
Wakuu wa Jukwaa,

Heri ya Mwaka Mpya 2012.

Kuna Mwanaume ambaye ametokea kunipenda sana, nami nampenda sana ingawa hatujafikia hatua ya mahusiano ya kimwili. Napenda kumwita A.

Kinachonitatiza ni kuwa enzi za ujana wao, Baba yake A (Namwita B) na Mama yangu walizaa binti ambaye tumpe jina C. Sasa mimi na C tunashare Mama lakini Baba zetu tofauti. C ni dada yangu, yeye ni mkubwa mimi ni mdogo. Wazazi wangu wote walifariki. A na C hawajawahi kufahahamiana hadi walipokutana hivi karibuni na kutambulishwa na baba yake yaani B katika harusi ya Binti mwingine wa baba yake A (yaani baba B) ambaye alizaa na Mwanamke mwingine tena.

Kwa upande wa A, yaani Mwanaume tunayependana amelelewa na familia nyingine toka utotoni ambayo mama yake Mzazi na A aliolewa na Baba mwingine. A ana ndugu zake huko waliolelewa pamoja. Hii ndiyo familia yake ya sasa.

Sasa swali langu kwenu wana MMU, je mimi naweza kuolewa na Mwanaume huyu yaani A?

Naomba kuwakilisha.

OK. We have A, B, C, and let call u D, your mom E

so. B and E make C
A and C come from B
C and D come from E

So what is relation btn D, A, B
D, A, E

D = only to E
A = only to B

so: A is not equal to D

A and D are not equal Genetically
There is no any biological, social, culture or belief conflict if they marry

for christian read Genesis 28:2 you can read all story to chapter 30.
 
Dada kupenda ni ugonjwa ambao hauponi mpaka umetimia ni sawa na kuwa njuka, huponi mpaka umekuwa form two, chamsingi hapo washirikishe watu wazima kwani kwenye wakubwa hakuharibiki kitu, lkn NENO LA MUNUG lipewe nafasi kubwa sana kwani siku za usoni yakitokea mabaya utalaumiwa lkn kama humkosei Mungu wa kweli na Yesu kristo mwana wa mungu basi Rhuksa, kula kasa japo inaua wakati mwingine.
 
Akati mnaanza kupigana sound kwanini hamkujiuliza hayo maswali kwanza?
Acha unafiki we binti.
Ningekua nakujua ningekucharaza mboko kwanza!
 
Back
Top Bottom