Ndugu zangu Watanzania, kumekuwa na matatizo kadhaa yanayotukabili katika Taifa letu.
Kwa ufupi naomba tutathmini ikiwa njia tunazotumia kutatua tatizo ni sahihi kulingana na tatizo lenyewe au la?
Kwa kawaida ukitumia njia sahihi kutatua tatizo ulilo nalo, bila shaka tatizo hilo litakwisha na ukitumia njia zisizo sahihi hilo tatizo halitakwisha na huenda likaongezeka zaidi.
Mfano, mimi nimekukata kidole kimoja cha mkono kwa uonevu tu, na wewe ukashindwa kunikabili kwa kiwango kinacholingana au cha juu zaidi kuliko nilivyokutenda wewe, pengine ukaishia kulalamika tu. Bila shaka, kesho nikija nitakuwa na uwezo wa kukukata hata zaidi ya vitatu. Nikiona hujachukua bali unalalamika tu, kesho naweza kukukata hata mikono yote miwili kwa sababu nitakuwa nimekusoma kwamba huwezi kunichukulia hatua kali.
Lakini kama nitakukata kidole kimoja na wewe ukalipiza kwa kunikata kidole kimoja au zaidi, bila shaka sitaweza tena kukufanyia ujinga mwingine kwa sababu nitaogopa kupata maumivu zaidi ya niliyokupatia wewe na hapo utakuwa umetatua tatizo la kuonewa.
Kutokana na mfano huo tujifunze, Je, matatizo makubwa ya kuonewa tuliyo nayo sasa tunatumia njia sahihi zinazoweza kukomesha kabisa uonevu au tunaishia tu kulalamika ndo maana tunaendelea kuonewa?
Nawasilisha. Karibu kwa maoni yako.