Je, nyama ya nguruwe inafaa kwa supu?

Je, nyama ya nguruwe inafaa kwa supu?

Za asubuhi wakuu,

No offense to my muslim folks, naomba kuuliza kama kuna mtu ameshawahi kukuta sehemu wanauza supu ya mdudu.

Kiukweli Mimi kuzunguka kwangu kote nlibahatisha sehemu kuna supu ya KONGORO la mdudu Ila sio Ile pure nyama kabisa.

Napenda kuuliza, je nyama yake haifai Kwa supu au kuna madhara yatokanayo na kuinywa supu yake?

inawezekana sehemu zipo,mimi sikuwahi kusikia mtu kala maini ya Nguluwe ila kuna siku nimeenda sehemu yangu fulani dada muuzaji akanambia yapo maini ya nguluwe nikakaangiwa yakalostiwa
siku nyingine kuna dada nilimpa hela afate nyama ya nguluwe akaleta ulimi ila ulikuwa mtamu,hivo basi nguluwe ana mambo mengi kwa kuna uwezekano supu yake inapigwa ila kongolo za miguu sidhani
 
Thumbs up mkuu ntajaribu na kukuletea mrejesho. Samahani kidogo, nyama unaichemsha Kwanza ndio unaitenga pembeni?
Itategemea na aina ya ndizi.
Kuna zile ndizi kubwa laini wanaita ndizi bukoba itabidi upike kwanza nyama iive ive then ndo uweke ndizi maana hizi ndizi zinawahi sana kuiva.
Kuna zile ndizi ngumu nyembamba wanaita ndizi mshale,unaweza chanyanya nyama na ndizi kwa wakati mmoja
 
Kwa nyama HAPANA na ataekwambia inawezekana huyo mtu mchukie

kwasababu atakua haitakii mema afya yako,hao ndio kula kula ilimradi (sio sumu)

Haifai kwasababu ile nyama ina mafuta sana sana ndio mana hata kwenye kukaanga

ni nyama pekee inayojikaanga yenyewe kwa mafuta yake,mdudu hakaangwi na Korie wala sunflower

hivyo kwenye supu wanachemsha kongoro tu kwa sababu ndiyo sehemu isiyo na mafuta mengi mtu unaweza

kunywa na ukashiba bila kusikia kukereketwa,ila supu ya nyama ya mdudu tu ukiinywa kesho yake utaendesha gari bila leseni.
Labda kama unaweka nyama vipande vichache saana.

Pia mkuu naona watu wengi wanakosea kukaanga hii nyama.

Hii nyama inabidi ichemshwe, ikimalizika unaikaanya na mafuta yake, na inakuwa nzuri mno.

Huenda wakawa wanakaanga na mafuta yake ili kuepusha muda.
 
Kuna siku nilikuwa nakula kitimoto mahali nikaitwa kafiri
Kwa mujibu wa Biblia Takatifu,kafiri maana Yake ni hii
IMG_20201104_211101_9.jpg
 
Labda kama unaweka nyama vipande vichache saana.

Pia mkuu naona watu wengi wanakosea kukaanga hii nyama.

Hii nyama inabidi ichemshwe, ikimalizika unaikaanya na mafuta yake, na inakuwa nzuri mno.

Huenda wakawa wanakaanga na mafuta yake ili kuepusha muda.
Mkuu hii nyama ukiichemsha halafu uikaange hupati taste ya mdudu OG

ndio mana point za mdudu nyingi hawachemshi,ukiona wanachemsha basi

ujue anakaaangia mafuta ya korie,sunflower,nk maana mafuta hayo yanawahi

ivisha nyama na kuikausha haraka tofauti na anaekaanga nyama kwa mafuta halisi

ya mdudu mwenyewe,mafuta ya mdudu sio makali,hayababui nyama yanakaanga nyama

taratiiibuuuu hadi inaiva,na wengi wanaokaanga kwa mafuta haya huwa hawachemshi nyama

wanaidumbukiza mbichi hvyo hvyo,ila ukitumia mafuta ya dukani nyama muhimu kuchemsha la sivyo

utakula nyama ngumu isiyo na real taste na usi enjoy utamu halisi wa mnyama aliethibitishwa na TBS.
 
inawezekana sehemu zipo,mimi sikuwahi kusikia mtu kala maini ya Nguluwe ila kuna siku nimeenda sehemu yangu fulani dada muuzaji akanambia yapo maini ya nguluwe nikakaangiwa yakalostiwa
siku nyingine kuna dada nilimpa hela afate nyama ya nguluwe akaleta ulimi ila ulikuwa mtamu,hivo basi nguluwe ana mambo mengi kwa kuna uwezekano supu yake inapigwa ila kongolo za miguu sidhani
Uko sahihi,labda culture zetu zinafanya kitojua vitu vingi. Mara ya kwanza kula mayai ya bata/kanga nilihisi kichefuchefu kutokana na background yangu sikuwahi kuona jamii yangu ikila.
 
Uko sahihi,labda culture zetu zinafanya kitojua vitu vingi. Mara ya kwanza kula mayai ya bata/kanga nilihisi kichefuchefu kutokana na background yangu sikuwahi kuona jamii yangu ikila.

ndio mkuu yani vitu vingi sana vinaliwa ila hatujui tu au hatuvifuatilii kwa mfano hapa jirani yangu kuna kanga ila nawaza nimuombe nifuge sio kula mayai kwa sababu ni kitu sijawahi na wewe ndio mtu wa kwanza nakusikia kwamba mayai ya khanga yanaliwa.
 
una pafahamu ubungo Riverside uku kwa mzee wa upako?
bas ukiweza kufika mpaka mitaa hii ya karibu na kanisa la Lusekelo uliza machinjio ya Mdudu yapo wapi bas utaelekezwa kua ume fika sehem husika nazan kg hua n 7000 tshs
Ahsante mkuu
 
Mkuu hii nyama ukiichemsha halafu uikaange hupati taste ya mdudu OG

ndio mana point za mdudu nyingi hawachemshi,ukiona wanachemsha basi

ujue anakaaangia mafuta ya korie,sunflower,nk maana mafuta hayo yanawahi

ivisha nyama na kuikausha haraka tofauti na anaekaanga nyama kwa mafuta halisi

ya mdudu mwenyewe,mafuta ya mdudu sio makali,hayababui nyama yanakaanga nyama

taratiiibuuuu hadi inaiva,na wengi wanaokaanga kwa mafuta haya huwa hawachemshi nyama

wanaidumbukiza mbichi hvyo hvyo,ila ukitumia mafuta ya dukani nyama muhimu kuchemsha la sivyo

utakula nyama ngumu isiyo na real taste na usi enjoy utamu halisi wa mnyama aliethibitishwa na TBS.
sawa kabisa kuchemsha muhimu ila usiweke maji,chemsha ilesupuyakeikikauka karanga kwamoto mdogo mpakamwisho utapata rangi safi na nyama laini,ukitaka kukaanga na mafuta mengine basi kuwa mpole mafuta moto wastani tu mpaka itapata rangi safi na laini.hapo ukitoa tu ni chumvi ndimu fasta na pilipili kula ya moto utapiga yowe.
 
hapa shambani kwangu msimu wa kilimo huwa tunachoma na kuchemsha ngiri
ni jamii hiyo hiyo
 
Back
Top Bottom