Je Pyramids zilikua na kazi gani ?

Je Pyramids zilikua na kazi gani ?

View attachment 3250113
View attachment 3250115
the great pyramid of Giza


tutumie great pyramid ( Piramidi kuu )

hii pyramidi imejengwa zaidi ya miaka 4700 iliyopita lakini inaacha maswali mengi zaidi kuliko majibu, maana kila unapojaribu kupata jibu unakutana na maswali zaidi kuhusiana na jibu lako,

inavyoaminika hadi sasa ni kwamba, pyramids zilijengwa hasa kama sehemu au mahali pa maziko kwa mfalme.
watu a rcheology wanakadiria kua pyramid kuu imetumia miaka ishirini hadi kukamilika.

lakini je, lengo lao haswa likikua ni kwaajili ya kulitumia kama kaburi la farao kama inavyoaminika na wanasayansi wa sasa au ilikua na maana nyingine na matumizi mengine ambayo ni tofauti kabisa?

View attachment 3250118

★ Pyramid kuu imejengwa kwa mawe makubwa sana zaidi ya milioni 2.3
★ kila jiwe lina uzito wa kati ya tani mbili hadi tani 80 kwa jiwe moja
★ ilijengwa kwa urefu wa mita 146.66 kwenda juu
★ Chini ina upana wa mita 230.4 kila upande
★ juu kabisa ina upana wa mita 0 yaani ilikua na ncha kabisa
★ imenyooshwa kufuata true north ikiwa na error ya 0.05° tu
★ kona zake zimenyooshwa nyuzi 90 kabisa zikiwa na error ya 0.01° tu
★ ni moja kati ya maajabu saba ya dunia ya kale na ndio ya pekee inayoendelea kusalia hadi leo

Pyramid ina chambers mbali mbali zipatazo 6 zenye kazi tofauti ambapo mbili ni kwaajili ya mfalme na malkia pyramid kuu ilijengwa kwaajili ya Pharaoh Khufu

View attachment 3250119

ujenzi wa piramidi hasa ndio unaacha fumbo ambalo ni ngumu kuelewa wenzetu walifanyaje miaka 4700 iliyopita?
walikua na teknolojia gani iliyowawezesha kujenga jengo la namna hii ?

- jinsi gani waliyatengeneza matofali makubwa yenye uzito wa hadi kilo 80,000 kwa tofali moja ?

- hata baada ya kutengeneza matofali ya uzito huo je waliwezaje kuyahamisha kutoka walipoyatengeneza hadi kwenda kuyajengea pyramid ambalo lina urefu mkubwa tu kwenda juu ? zaidi ya matofali milioni mbili na laki tatu

- walichokifanya miaka 4700 iliyopita bado ni kigumu hata tukitaka kukifanya sasa,
mfano kufikia precission ya vipimo kama walivyofikia wao inabidi kutumia Laser Scaner na vifaa vingine vya kisasa


pande za pyramid zimejengwa zililinganishwa na True North ( yaani upande halisi wa kaskazini wa dunia )
huu upande halisi wanasayansi walianza kuujua baada ya kugundulika kwa dira.

miaka 4700 iliyopita wa misri wa zamani walijenga pyramid kufuata True north wakiwa na error ya 0.05 degree
je waliwezaje ?
nini ilikua lengo lao kufanya hivyo ?

kwa vifaa na mbinu ambazo tunaamini zilitumika kujenga pyramid, mfano kwa siku moja wangeweza kutengeneza tofali moja na lulisafirisha hadi kwenye pyramid na kuliweka kulingana na vipimo,
ingetumia zaidi ya miaka 6000 kukamilisha ujenzi wa piramidi moja, lakini piramidi kuu limejengwa ndani ya miaka 20 tu

theory nyingine zina sugest kwamba huenda tunavyowajua watu wa kale ni tofauti na maisha yao halisi yalivyokua,

huenda pia walikua na teknolojia kubwa tuu ambayo ilipotea kwa sababu fulani na hatujaweza kuipata, lakini baadhi ya mambo na alama walizo acha zinadhihirisha ujuzi waliokua nao,
pia huenda bado hatujui lengo halisi na matumizi halisi ya piramidi katika kipindi chao.
Wazungu wana tabia moja nayo ni kutambua ugunduzi pale wao wanapo gundua ni kama mlima Kilimanjaro wanakuambia mgunduzi ni mtu fulani wa kizungu ...hivyo zamani walikuwa na technology kubwa tu hasa kwenye ujenzi na vita ...usafiri majini nk hata ramani ya dunia walikuwa nayo kwa ufasaha hadi imewashangaza wanasayansi wa sasa


View: https://youtu.be/bPHcWeXrXOQ?si=yv52O-Yh8DZhpDLf
 
Waz

Ungu wana tabia moja nayo ni kutambua ugunduzi pale wao wanapo gundua ni kama mlima Kilimanjaro wanakuambia mgunduzi ni mtu fulani wa kizungu ...hivyo zamani walikuwa na technology kubwa tu hasa kwenye ujenzi na vita ...usafiri majini nk hata ramani ya dunia walikuwa nayo kwa ufasaha hadi imewashangaza wanasayansi wa sasa


View: https://youtu.be/bPHcWeXrXOQ?si=yv52O-Yh8DZhpDLf

hao watu walikua hatari
 
mkuu, kuhusu lengo la ujenzi wa mnara wa babeli nakushauri ukasome tena historia hasa biblia utaelewa, nakupa mfano tena, umemkaribisha mtu katika shamba lako,ana tamaduni zake tofauti na wewe, akaishi humo,akajenga nyumba nzuri kukuzidi wewe, je utamuacha aje akujengee na wewe ya kufanana naye? ndivyo ilivyokuwa,na ukae ukijua miaka 400 ni zaidi ya vizazi vinne, waisrael waliongezeka na kuwazidi wenyeji hivyo baadhi ya wenyeji walifuata tamaduni za kiisrael kama vile mummification,na ustaarabu mwingine. piramid ya kwanza ilijengwa na waisrael kama sehemu ya kuwahifadhi(sio kuzika) na waegpt walipoona piramids hiyo wakabidi wawatumie hao waisrael kujenga piramid kwa ajiri yao.
Ukisoma vizuri Biblia utagundua
1. Misri ilikuwako kabla ya Israel
2. Misri kwa kipindi hicho ilikuwa na maendeleo na ustaarabu mwingi kuliko israel
 
mkuu, kuhusu lengo la ujenzi wa mnara wa babeli nakushauri ukasome tena historia hasa biblia utaelewa, nakupa mfano tena, umemkaribisha mtu katika shamba lako,ana tamaduni zake tofauti na wewe, akaishi humo,akajenga nyumba nzuri kukuzidi wewe, je utamuacha aje akujengee na wewe ya kufanana naye? ndivyo ilivyokuwa,na ukae ukijua miaka 400 ni zaidi ya vizazi vinne, waisrael waliongezeka na kuwazidi wenyeji hivyo baadhi ya wenyeji walifuata tamaduni za kiisrael kama vile mummification,na ustaarabu mwingine. piramid ya kwanza ilijengwa na waisrael kama sehemu ya kuwahifadhi(sio kuzika) na waegpt walipoona piramids hiyo wakabidi wawatumie hao waisrael kujenga piramid kwa ajiri yao.
Kama Waisrael waliweza kujenga pyramid hapo Misri mbona waliporudi kwao baada ya utumwa hawakuweza kuzijenga hizo pyramid?
 
Back
Top Bottom