Je Pyramids zilikua na kazi gani ?

Je Pyramids zilikua na kazi gani ?

Ni kweli mkuu, hii inaleta maswali kadha wa kadha... Usikute duniani kulikua na maisha fulani ambayo yalifikia katika level za juu sana za technology ila kwa sababu fulani yake maisha yaliharibiwa kisha tukaja sisi kuanza maisha mengine upya kabisa.
Kabisa kumbuka mwanzo 11 katka Bibilia mnara wa babeli ujenzi wake hata Mungu akasema natushuke tuwavurugie mipango na lugha Yao vinginevyo tukiwaacha wamedhamiri kufikisha mnara hadi huku tulipo
 
Kabisa kumbuka mwanzo 6 katka Bibilia mnara wa babeli ujenzi wake hata Mungu akasema natushuke tuwavurugie mipango na lugha Yao vinginevyo tukiwaacha wamedhamiri kufikisha mnara hadi huku tulipo
Hii puzzle inachanganya sana akili, ila hilo andiko ni uthibitisho mwingine wa kutuambia kwamba Dunia ilishawahi kuwa na ustaarabu wa hali ya juu hapo awali... Kuna michoro niliwahi kuiona ya kale ilikua inaonesha helicopter.
 
nacho maanisha ni kwamba mchina atatumia teknolojia ya kisasa ndo utofauti huo, hizo wamisri walijenga miaka hiyo kwa vifaa wanavyojua wao
usiseme walijenga wamisri sema piramids zilizopo misri ukisema walijenga wamisri utakuwa unapotosha na kuudanganya umma.
 
Hii puzzle inachanganya sana akili, ila hilo andiko ni uthibitisho mwingine wa kutuambia kwamba Dunia ilishawahi kuwa na ustaarabu wa hali ya juu hapo awali... Kuna michoro niliwahi kuiona ya kale ilikua inaonesha helicopter.
Ndomaana tunasema hakunajipya chini ya jua
 
Hii puzzle inachanganya sana akili, ila hilo andiko ni uthibitisho mwingine wa kutuambia kwamba Dunia ilishawahi kuwa na ustaarabu wa hali ya juu hapo awali... Kuna michoro niliwahi kuiona ya kale ilikua inaonesha helicopter.
Well said
 
Nimeisoma hiyo historia vizuri. Waisrael wangapi walienda Misri na wangapi waliondoka baada ya miaka 400?

Walioingia unaweza kuwaita Taifa watu chini ya mia moja? Kila kitu walijifunza Misri, wakachukua vitu kadhaa na wakabadilisha vitu kadhaa wakatengeneza dini yao tofauti.
ni mtu asiyekuwa na maarifa na asiyejua historia na vitabu vya dini ndiye atakayesema waisrael waliotoka misri idadi yao walikuwa hawafiki mia, ngoja nikufundishe na nikupe somo kidogo, waisrael walioingia egypt idadi yao inaweza kuwa watu 50,lakini ndani ya miaka hiyo 400 walizaliana na kuongezeka hadi kuwazidi wenyeji wa eneo husika,ilifikia hatua watawala wa egypt wakawa wanaua watoto wadogo wasije wakaendeleza kizazi hicho na kuwapindua. Ila hao mafarao walikuwa wanafaidika na waisrael hasa ktk ujenzi wa piramids. Mkuu naongea haya nikiwa kama mbobezi wa history na nimetembea nchi nyingi za kihistoria kukuletea haya.
 
Hiyo michoro ilichorwa kama miaka mingapi iliyopita
Inakadiriwa kuwa na takriban miaka 3,000 hadi 3,200 kwa kuwa inahusiana na enzi ya Farao Seti I, aliyewahi kutawala Misri kati ya 1290 na 1279 KK.
 
View attachment 3250113
View attachment 3250115
the great pyramid of Giza

tutumie great pyramid ( Piramidi kuu )

hii pyramidi imejengwa zaidi ya miaka 4700 iliyopita lakini inaacha maswali mengi zaidi kuliko majibu, maana kila unapojaribu kupata jibu unakutana na maswali zaidi kuhusiana na jibu lako,

inavyoaminika hadi sasa ni kwamba, pyramids zilijengwa hasa kama sehemu au mahali pa maziko kwa mfalme.
watu a rcheology wanakadiria kua pyramid kuu imetumia miaka ishirini hadi kukamilika.

lakini je, lengo lao haswa likikua ni kwaajili ya kulitumia kama kaburi la farao kama inavyoaminika na wanasayansi wa sasa au ilikua na maana nyingine na matumizi mengine ambayo ni tofauti kabisa?

View attachment 3250118

★ Pyramid kuu imejengwa kwa mawe makubwa sana zaidi ya milioni 2.3
★ kila jiwe lina uzito wa kati ya tani mbili hadi tani 80 kwa jiwe moja
★ ilijengwa kwa urefu wa mita 146.66 kwenda juu
★ Chini ina upana wa mita 230.4 kila upande
★ juu kabisa ina upana wa mita 0 yaani ilikua na ncha kabisa
★ imenyooshwa kufuata true north ikiwa na error ya 0.05° tu
★ kona zake zimenyooshwa nyuzi 90 kabisa zikiwa na error ya 0.01° tu
★ ni moja kati ya maajabu saba ya dunia ya kale na ndio ya pekee inayoendelea kusalia hadi leo

Pyramid ina chambers mbali mbali zipatazo 6 zenye kazi tofauti ambapo mbili ni kwaajili ya mfalme na malkia pyramid kuu ilijengwa kwaajili ya Pharaoh Khufu

View attachment 3250119

ujenzi wa piramidi hasa ndio unaacha fumbo ambalo ni ngumu kuelewa wenzetu walifanyaje miaka 4700 iliyopita?
walikua na teknolojia gani iliyowawezesha kujenga jengo la namna hii ?

- jinsi gani waliyatengeneza matofali makubwa yenye uzito wa hadi kilo 80,000 kwa tofali moja ?

- hata baada ya kutengeneza matofali ya uzito huo je waliwezaje kuyahamisha kutoka walipoyatengeneza hadi kwenda kuyajengea pyramid ambalo lina urefu mkubwa tu kwenda juu ? zaidi ya matofali milioni mbili na laki tatu

- walichokifanya miaka 4700 iliyopita bado ni kigumu hata tukitaka kukifanya sasa,
mfano kufikia precission ya vipimo kama walivyofikia wao inabidi kutumia Laser Scaner na vifaa vingine vya kisasa

pande za pyramid zimejengwa zililinganishwa na True North ( yaani upande halisi wa kaskazini wa dunia )
huu upande halisi wanasayansi walianza kuujua baada ya kugundulika kwa dira.

miaka 4700 iliyopita wa misri wa zamani walijenga pyramid kufuata True north wakiwa na error ya 0.05 degree
je waliwezaje ?
nini ilikua lengo lao kufanya hivyo ?

kwa vifaa na mbinu ambazo tunaamini zilitumika kujenga pyramid, mfano kwa siku moja wangeweza kutengeneza tofali moja na lulisafirisha hadi kwenye pyramid na kuliweka kulingana na vipimo,
ingetumia zaidi ya miaka 6000 kukamilisha ujenzi wa piramidi moja, lakini piramidi kuu limejengwa ndani ya miaka 20 tu

theory nyingine zina sugest kwamba huenda tunavyowajua watu wa kale ni tofauti na maisha yao halisi yalivyokua,

huenda pia walikua na teknolojia kubwa tuu ambayo ilipotea kwa sababu fulani na hatujaweza kuipata, lakini baadhi ya mambo na alama walizo acha zinadhihirisha ujuzi waliokua nao,
pia huenda bado hatujui lengo halisi na matumizi halisi ya piramidi katika kipindi chao.
Siku zinavyozidi kwenda uwezo wa mwanadamu unazudi kupungua kutokana na sababu mbalimbali zakimazingira, na ndio maana mambo kama haya tunaona mambo makubwa..

Dunia ya sasa kuna AI ambayo tunaona sisi ni msaidizi kwetu lakini anatufanya tushindwe hata kufikiri kwa jambo dogo ambalo tungeweza kulifanya, lakini twaona aaaah! Nisijichoshe ngoja nitumie AI.
 
Na helicopter ziligunduliwa kama miaka mingapi iliyopita
Mwanzoni mwa karne ya 20 ndio helicopter zilianza kufanya kazi, ingawa wazo la tekinolojia ya ndege kwa ujumla lilianzia karne za nyuma zaidi ya hapo.
 
ni mtu asiyekuwa na maarifa na asiyejua historia na vitabu vya dini ndiye atakayesema waisrael waliotoka misri idadi yao walikuwa hawafiki mia, ngoja nikufundishe na nikupe somo kidogo, waisrael walioingia egypt idadi yao inaweza kuwa watu 50,lakini ndani ya miaka hiyo 400 walizaliana na kuongezeka hadi kuwazidi wenyeji wa eneo husika,ilifikia hatua watawala wa egypt wakawa wanaua watoto wadogo wasije wakaendeleza kizazi hicho na kuwapindua. Ila hao mafarao walikuwa wanafaidika na waisrael hasa ktk ujenzi wa piramids. Mkuu naongea haya nikiwa kama mbobezi wa history na nimetembea nchi nyingi za kihistoria kukuletea haya.
Uwezo wa kusoma vizuri ukaelewa unakushinda, hayo mengine utaweza kweli kuyaelewa.

Umeambiwa waliongia hawakufika 100 walipotoka baada ya miaka 400 walikuwa zaidi ya 600,000 hata hiki kidogo kinakushinda kuelewa. Uwe unajaribu kuelewa kilichoandikwa kwanza kabla ya kujibu.

Walikuja kama wakimbizi wakikimbia njaa. Walipofika Egypt walikuta nchi iliyostaarabika na iliyoendelea kwenye kila sekta kama kilimo, afya,elimu,miundombinu, lugha, philosophy na sophisticated culture na mifumo thabiti ya kiutawala. Ndipo hapo walijifunza mambo mengi baada ya miaka 400 walikuwa wameiga mengi na kuyafanya sehemu ya utamaduni wao pia.

Walikaribishwa vizuri, ili baadaye namba zao zikipoongezeka sana ndio wakafanywa kuwa watumwa, sababu mazingira mazuri, chakula cha kutosha walizaliana sana kabla ya hapo kufika Misri walikuwa karibu wafe kwa njaa. Ukiwa na njaa, maskini huwezi kufikiria hata kujenga majengo ya kifahari kama pyramids.
 
mnara wa babeli according to bible haikujengea ili kimfikia Mungu, ulijengwa ili watu wasitawanyike yaani wasiende mbali nao uwekama sehemu ya kupatambua hapo ila moango wa Mungu ulikua ni wat
mkuu, kuhusu lengo la ujenzi wa mnara wa babeli nakushauri ukasome tena historia hasa biblia utaelewa, nakupa mfano tena, umemkaribisha mtu katika shamba lako,ana tamaduni zake tofauti na wewe, akaishi humo,akajenga nyumba nzuri kukuzidi wewe, je utamuacha aje akujengee na wewe ya kufanana naye? ndivyo ilivyokuwa,na ukae ukijua miaka 400 ni zaidi ya vizazi vinne, waisrael waliongezeka na kuwazidi wenyeji hivyo baadhi ya wenyeji walifuata tamaduni za kiisrael kama vile mummification,na ustaarabu mwingine. piramid ya kwanza ilijengwa na waisrael kama sehemu ya kuwahifadhi(sio kuzika) na waegpt walipoona piramids hiyo wakabidi wawatumie hao waisrael kujenga piramid kwa ajiri yao.
 
Mwanzoni mwa karne ya 20 ndio helicopter zilianza kufanya kazi, ingawa wazo la tekinolojia ya ndege kwa ujumla lilianzia karne za nyuma zaidi ya hapo.
Kwa hiyo hao waliozichora hizo helicopter walikuwa na helicopter zao kabla
 
Mkuu hao waisrael unawapigia chapuo si lolote wala chochote kwa Wa misri ndo maana walikua utumwani…kiasili na kikawaida jamii yenye nguvu ndo hutawala jamii Legevu. Mfano ni jamii legevu ya africans kutawqalia na jamii yenye nguvu Whites,ki uchumi na ki technology
wewe utakuwa hujui lolote mkuu, fuatilia chanzo cha utumwa wa waisrael misri halafu urudi hapa, usaidizi soma Bible, kuanzia GENESIS 37 ndipo utajua hawa waisrael ilikuwaje wakajikuta watumwa,ukiweza sana endelea hadi kitabu cha kutoka uone walikuwa wanafanya nini,harakati zao za ukombozi na ikikupendeza uendelee kusoma biblia uone hali ilikuwaje wakiwa njiani mpaka wakafika CAANAN ni hayo tu.
 
Kwa hiyo hao waliozichora hizo helicopter walikuwa na helicopter zao kabla
Hilo ndio halijulikani ila mtu hawezi kuchora kitu ambacho hajawahi kukiona, so kuna possibility kubwa ya kwamba tekinolojia ya hayo mambo ilikuwepo nyakati hizo.
 
wewe utakuwa hujui lolote mkuu, fuatilia chanzo cha utumwa wa waisrael misri halafu urudi hapa, usaidizi soma Bible, kuanzia GENESIS 37 ndipo utajua hawa waisrael ilikuwaje wakajikuta watumwa,ukiweza sana endelea hadi kitabu cha kutoka uone walikuwa wanafanya nini,harakati zao za ukombozi na ikikupendeza uendelee kusoma biblia uone hali ilikuwaje wakiwa njiani mpaka wakafika CAANAN ni hayo tu.
Walkuwa watumwa sababu ya njaa,walipigwa njaa huko na wakakimbilia misri kwa ndgu yao Yusuph then ndo wakaanza zaliana huko had kizaz cha Mussa.! Sa jamii yenye nguvu na maarifa itapigwa njaa na ikimbie ishndwe tatua hilo tatzo?!
 
vizuri,umeanza kuja katika maana yangu, kwa hiyo mkuu unamaanisha jamii isiyo na nguvu haiwezi kujiimalisha na kuwa jamii yenye nguvu?
 
vizuri,umeanza kuja katika maana yangu, kwa hiyo mkuu unamaanisha jamii isiyo na nguvu haiwezi kujiimalisha na kuwa jamii yenye nguvu?
case ya wa israel ni tofauti,kwa maana huko misri walikua watumwa na wasindikizaji tu sababu hawakuweza kufanya lolote la maana na ilkua ni jamii iliyoparanganyika….obviously hawawezi kuleta positive impact kwamba wao ndo wajenge hayo mapyramid!..Walkula na kulala kwa shida hua mda wa kua hzo akili hawakuw nazo.
 
Back
Top Bottom