Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,988
- 30,183
Imeandikwa na Malisa Godlisten
Katiba ya nchi ibara ya 55 inataja mchakato wa uteuzi wa mawaziri na manaibu waziri. Ibara ya 55(1) inasema Rais atateua mawaziri baada ya kushauriana na Waziri mkuu. Tasfiri ya kingerereza limetumika neno "shall" kuonesha kwamba ni lazima Rais ashauriane na Waziri mkuu kuwapata mawaziri. Sio hiyari.
Ibara ya 55(2) inasema Rais aweza kushauriana na Waziri Mkuu kuteua Manaibu Waziri. Tafsiri ya kiingereza imetumia neno "may" yani si lazima. Maana yake ni kwamba kuteua mawaziri Katiba inamlazimisha Rais kushauriana na Waziri Mkuu, lakini kuteua Manaibu Waziri Katiba haimlazimishi.
Ibara ya 51(1) inasema Waziri Mkuu ataanza kazi baada ya kuapa. Kwahiyo Rais anapaswa kumteua kwanza Waziri mkuu, amuapishe kisha ndio ashauriane nae kuteua Mawaziri. Haya ni masharti ya katiba, sio masharti ya ZZK wala Hashimu Rungwe.
Lakini Rais alimteua Waziri mkuu na Mawaziri wawili (Kabudi na Mipango) na akawaapisha kwa pamoja. Je, alishauriana na nani kuteua Mawaziri hao wakati Waziri mkuu alikua bado hajapatikana? Je uteuzi wa Kabudi na Mipango ni batili? Je Rais amevunja Katiba?
Hii ndio hoja ya ZZK. Hoja hii inatakiwa kujibiwa kwa weledi kwa sababu ni KOSA KUBWA Rais kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda. Moja ya mambo yanayoweza kumuondoa Rais madarakani ni kuvunja Katiba.
Lakini Mwigulu amejibu kwa mihemko na matusi. Mara ZZK ameshindwa uchaguzi, mara anatafuta kuwaridhisha mabwana zake na ujinga ujinga mwingine.
Nilitegemea Mwigulu ajibu hoja za ZZK kwa kujustify kwanini Rais hajavunja Katiba. Lakini yeye ameacha hoja akaanza kumshambulia mtoa hoja. What a shame for a PhD holder?
Lakini hii si mara ya kwanza Mwigulu kufanya utoto kama huu. Alipofurushwa uwaziri alikua anashinda mitandaoni kupiga X post za wapinzani. Hata bungeni alianzisha utaratibu wa kumsifia sana mkuu. Hatimaye akarudishwa kundini.
Pengine ameshajua udhaifu wa "boss" wake kwahiyo ameanza tena kupiga "X" post za wapinzani ili akumbukwe. Anajua uteuzi haupo mbali hivyo anaanza kutukana wapinzani, kuwashambulia watoa hoja badala ya kujibu hoja zao, sambamba na kumsifia "boss" kwa nguvu zote. Hii ndio aina ya viongozi tulio nao Afrika. Mwigulu et al. Poor Africa!