Je, Rais amevunja Katiba Kumuapisha PM na Mawaziri wengine kwa Pamoja?

Je, Rais amevunja Katiba Kumuapisha PM na Mawaziri wengine kwa Pamoja?

Nafikili ndiomaana huyo jamaa anamua kufanya anavyotaka.
Kuna kitu kimoja mkuu. Katiba hata iwe nzuri namna gani bila utashi wa viongozi wa kuifuata na umoja wa wananchi wa kuitetea pale viongozi wanapokwenda kinyume, hamna faida yoyote. Mtu kama Nyerere alikuwa na busara na nidhamu ya uongozi ndiyo maana wakati ule japo kilikuwa ni chama kimoja kushika hatamu lakini kulikuwa na viongozi makini waliopatikana kwa njia halali na za ushindani. Ameingia huyu mungu mtu hali imebadilika.
 
Katiba hiyo hiyo inampa Rais mamlaka yasiyohojika na halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote wala kubanwa na chochote anapotekeleza majukumu yake.

Hali hii ilianzia kwenye Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1962 wakati Nyerere aliporudi Madarakani kama Rais wa Jamhuri baada ya kuwa amejiuzuru nafasi ya Waziri Mkuu kwa shinikizo la Afrikanization.
Weka kabisa kifungu cha katiba kuhusu haya uliyoandika
 
Katiba ya nchi ibara ya 55 inataja mchakato wa uteuzi wa mawaziri na manaibu waziri. Ibara ya 55(1) inasema Rais atateua mawaziri baada ya kushauriana na Waziri mkuu. Tasfiri ya kingerereza limetumika neno "shall" kuonesha kwamba ni lazima Rais ashauriane na Waziri mkuu kuwapata mawaziri. Sio hiyari.

Ibara ya 55(2) inasema Rais aweza kushauriana na Waziri Mkuu kuteua Manaibu Waziri. Tafsiri ya kiingereza imetumia neno "may" yani si lazima. Maana yake ni kwamba kuteua mawaziri Katiba inamlazimisha Rais kushauriana na Waziri Mkuu, lakini kuteua Manaibu Waziri Katiba haimlazimishi.
Ibara ya 51(1) inasema Waziri Mkuu ataanza kazi baada ya kuapa. Kwahiyo Rais anapaswa kumteua kwanza Waziri mkuu, amuapishe kisha ndio ashauriane nae kuteua Mawaziri. Haya ni masharti ya katiba, sio masharti ya ZZK wala Hashimu Rungwe.

Lakini Rais alimteua Waziri mkuu na Mawaziri wawili (Kabudi na Mipango) na akawaapisha kwa pamoja. Je alishauriana na nani kuteua mawaziri hao wakati Waziri mkuu alikua bado hajapatikana? Je uteuzi wa Kabudi na Mipango ni batili? Je Rais amevunja Katiba?
Hii ndio hoja ya ZZK. Hoja hii inatakiwa kujibiwa kwa weledi kwa sababu ni KOSA KUBWA Rais kuvunja Katiba aliyoapa kuilinda. Moja ya mambo yanayoweza kumuondoa Rais madarakani ni kuvunja Katiba.

Lakini Mwigulu amejibu kwa mihemko na matusi. Mara ZZK ameshindwa uchaguzi, mara anatafuta kuwaridhisha mabwana zake na ujinga ujinga mwingine.
Nilitegemea Mwigulu ajibu hoja za ZZK kwa kujustify kwanini Rais hajavunja Katiba. Lakini yeye ameacha hoja akaanza kumshambulia mtoa hoja. What a shame for a PhD holder?

Lakini hii si mara ya kwanza Mwigulu kufanya utoto kama huu. Alipofurushwa uwaziri alikua anashinda mitandaoni kupiga X post za wapinzani. Hata bungeni alianzisha utaratibu wa kumsifia sana mkuu. Hatimaye akarudishwa kundini.
Pengine ameshajua udhaifu wa "boss" wake kwahiyo ameanza tena kupiga "X" post za wapinzani ili akumbukwe.
[emoji1787]
[emoji1787]
Anajua uteuzi haupo mbali hivyo anaanza kutukana wapinzani, kuwashambulia watoa hoja badala ya kujibu hoja zao, sambamba na kumsifia "boss" kwa nguvu zote. Hii ndio aina ya viongozi tulio nao Afrika. Mwigulu et al. Poor Africa.!!
Mimi nafikiri lazima uende mbali zaidi na kujua ni wakati gani Waziri Mkuu anakuwa mteule na wakati gani anakuwa Waziri Mkuu kamili na je uapishwaji wake unasemwa je? Ni lazima mara anapopitishwa na Bunge au wakati mwingine wowote Rais anapoamua hayo ni mambo mihimu kuyajua kabla hujahitimisha. Kwa namna ninvyoona Waziri Mkuu mteule anakuwa Waziri Mkuu immediately anapothibitishwa na Bunge suala la kuapa ni subject. Hivyo kipindi hicho mara baada ya kupitishwa na Bunge anaweza kushauriana na Rais katika kuwapata mawaziri wengine. ANZIA HAPO NDUGU YANGU
 
Hahaha kwanza ni ujinga kwa mtu aliyejuu ya sheria kuapa au kuapishwa.

Unamuapisha ili iweje na kwanini?!

Nini maana ya kiapo?!

Wamepitisha sheria kwamba wao hawashitakiwi leo na hata kesho. Yani wakiwa madarakani na hata wakitoka madarakani.

Sasa kiapo cha nini wanaapishana ili iweje?!

Wanavunja shera zipi wakati wako juu ya sheria?!, hata wakizivunja hakuna madhara yoyote kwao?!

Hawaadhibiwi Sasa yanini hata kuleta uzi huu?!

Ni sawa na kusema Mimi na wewe na malaika tumuapishe Mungu, wakati hata akikosea hatuwezi kumuadhibu.

Sasa nini faida ya viapo vyao, wanaapa nini, kwa nani, kwanini, ili iweje?!

Wakivunja sheria then what?!
I salute you for your comments
 
Hivi nani ana uhakika na ushahidi kwamba Rais hushauriana kweli na waziri Mkuu kwenye hizi teuzi za Mawaziri?

Hiyo sheria yenyewe ina makengeza.

Rais akisema alijadiliana na PM tarehe 4 November 2020 hiyo sheria inambana vipi?

Maana Majaliwa alikuwa bado PM.
Haya ndio makande ya Lumumba...hvi unaelewa kweli au uzombie umetawala kichwani.....ebu jaribu kuficha kdg huu ujuha wako
 
Kuna kitu kimoja mkuu. Katiba hata iwe nzuri namna gani bila utashi wa viongozi wa kuifuata na umoja wa wananchi wa kuitetea pale viongozi wanapokwenda kinyume, hamna faida yoyote. Mtu kama Nyerere alikuwa na busara na nidhamu ya uongozi ndiyo maana wakati ule japo kilikuwa ni chama kimoja kushika hatamu lakini kulikuwa na viongozi makini waliopatikana kwa njia halali na za ushindani. Ameingia huyu mungu mtu hali imebadilika.
Hahahahahahahahaahaha.........
Umenikumbusha baba yetu nyerere.
Nakumbuka kwenye hotuba zake alishasema kwa katiba hii ya sasa akitoke mtu asiekua na busara atafanya anavyotaka.
Na hio yaha sasa tunayaona.
Kiukweli hali inatisha ila tatizo hawa vijana wanaojiita wasomi waliokalibu nae wamekaatu kama mashemale.
Ni tatizo.
Yaan wakiambia kaueni,katesen wao ndio.wanaona sawa ila wakiambiwa wapiganie fulani kwa faida ya vizazi hakuna.
 
Anaijua hata hiyo katiba? Viilevile si amekiri hadharani hajua diplomasia ni nini? Dark ages in Tanzania .
 
Kuna kitu kimoja mkuu. Katiba hata iwe nzuri namna gani bila utashi wa viongozi wa kuifuata na umoja wa wananchi wa kuitetea pale viongozi wanapokwenda kinyume, hamna faida yoyote. Mtu kama Nyerere alikuwa na busara na nidhamu ya uongozi ndiyo maana wakati ule japo kilikuwa ni chama kimoja kushika hatamu lakini kulikuwa na viongozi makini waliopatikana kwa njia halali na za ushindani. Ameingia huyu mungu mtu hali imebadilika.
Unaona kabisa hata nyerere na uzee wake aliona katiba hii inatatizo ila aliamua kuwaacha vijana lakini ametutahadharisha.
Kikwete kaja kabaliki kabisa kama mnataka kubadili ndio wakati wenu huu.
Lakini wanatoke.wajinga wachache wamevuruga.

Sizani kama atatokea tena wa kuweza au kutamani kufanya mabadiliko ten kwa miaka hii a kalibuni.
 
Mimi nafikiri lazima uende mbali zaidi na kujua ni wakati gani Waziri Mkuu anakuwa mteule na wakati gani anakuwa Waziri Mkuu kamili na je uapishwaji wake unasemwa je? Ni lazima mara anapopitishwa na Bunge au wakati mwingine wowote Rais anapoamua hayo ni mambo mihimu kuyajua kabla hujahitimisha. Kwa namna ninvyoona Waziri Mkuu mteule anakuwa Waziri Mkuu immediately anapothibitishwa na Bunge suala la kuapa ni subject. Hivyo kipindi hicho mara baada ya kupitishwa na Bunge anaweza kushauriana na Rais katika kuwapata mawaziri wengine. ANZIA HAPO NDUGU YANGU
So anaweza tu kupiga kazi hata kabla hajaapishwa?
 
Malisa umekosa ubunge kupitia Chadema hasira zako unataka kuzimalizia kwa Magufuli pole
You are off the point...!!

Inashangaza na wewe badala ujikite kwenye hoja, umetoka nje kabisa na kuanzisha "personal attack" kwa mleta hoja kama alivyofanya Mwigulu..

Hebu jikite kwenye hoja sasa..

Je, Rais Magufuli kavunja Katiba ya JMT kama inavyoelezwa au HAPANA hajavunja?

Maelezo ya mtoa mada yanaenda na vielelezo vya ibara za katiba. Wewe unasemaje?

Kama ndiyo tufanyeje kwa Rais wako kuisigina ama kutoijali katiba ya nchi?
 
Imeandikwa na Malisa Godlisten

Katiba ya nchi ibara ya 55 inataja mchakato wa uteuzi wa mawaziri na manaibu waziri. Ibara ya 55(1) inasema Rais atateua mawaziri baada ya kushauriana na Waziri mkuu. Tasfiri ya kingerereza limetumika neno "shall" kuonesha kwamba ni lazima Rais ashauriane na Waziri mkuu kuwapata mawaziri. Sio hiyari...
Law interpretation imekupiga chenga.
 
Back
Top Bottom