Je, Rais amevunja Katiba Kumuapisha PM na Mawaziri wengine kwa Pamoja?

Je, Rais amevunja Katiba Kumuapisha PM na Mawaziri wengine kwa Pamoja?

Katiba ya nchi ibara ya 55 inataja mchakato wa uteuzi wa mawaziri na manaibu waziri. Ibara ya 55(1) inasema Rais atateua mawaziri baada ya kushauriana na Waziri mkuu. Tasfiri ya kingerereza limetumika neno "shall" kuonesha kwamba ni lazima Rais ashauriane na Waziri mkuu kuwapata mawaziri. Sio hiyari...
JPM alishauriana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ileeeeeeeeeee baada tu ya ushindi wa kishindo, akingali bado PM, wakakubaliana wamchague Prof. Kabudi & Dr. Mpango. Case closed, Mr Trump. You fairly lost the election!
 
Wakati Matokeo yanatangazwa kua JPM kashinda hakukua na Waziri Mkuu
 
Katiba ya nchi ibara ya 55 inataja mchakato wa uteuzi wa mawaziri na manaibu waziri. Ibara ya 55(1) inasema Rais atateua mawaziri baada ya kushauriana na Waziri mkuu. Tasfiri ya kingerereza limetumika neno "shall" kuonesha kwamba ni lazima Rais ashauriane na Waziri mkuu kuwapata mawaziri. Sio hiyari...
Malisa na Zitto wamezidi na propaganda zao z kisiasa. Hawajawashinda kwa hoja yoyote!
 
mhe zzmk ni kama chizi baada ya ile ajali,akili yake haiko sawa tena yani hana tofauti na lissu wa risasi za kiuno😂😂😂😂😂
Jiulize huyo mwenye kitufe kwenye moyo anayeua watu kila kukicha kichwani chake kizima? Mzee wa watu analazimisha kuchekesha kwenye hotuba zake badala yake anajikuta anaongea mambo ya kutia aibu nchi! Siku yake yaja... amezoea kumdhihaki Mungu akifikiri Mungu anadhihakiwa!
 
Hivi nani ana uhakika na ushahidi kwamba Rais hushauriana na waziri Mkuu kwenye hizi teuzi za Mawaziri?
Kuna vitu vingine tunatakiwa tuwe tunavitafakari kwa kina. Huyo Waziri Mkuu anateuliwa na huyo huyo mtu mmoja, ni dhahiri hakuna ushauri makini sana anaoweza kutoa.

Haswa kama walivyokwishafanya pamoja awamu ya kwanza, anatakiwa kufuata mwelekeo na matakwa ya mwenye kuteua. Hizo ibara ni kiini macho tu cha siasa za utawala wa chama kimoja.
 
Katiba hiyo hiyo inampa Rais mamlaka yasiyohojika na halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote wala kubanwa na chochote anapotekeleza majukumu yake.

Hali hii ilianzia kwenye Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1962 wakati Nyerere aliporudi Madarakani kama Rais wa Jamhuri baada ya kuwa amejiuzuru nafasi ya Waziri Mkuu kwa shinikizo la Afrikanization.
 
Katiba ya nchi ibara ya 55 inataja mchakato wa uteuzi wa mawaziri na manaibu waziri. Ibara ya 55(1) inasema Rais atateua mawaziri baada ya kushauriana na Waziri mkuu. Tasfiri ya kingerereza limetumika neno "shall" kuonesha kwamba ni lazima Rais ashauriane na Waziri mkuu kuwapata mawaziri. Sio hiyari...
Umeandika vizuri sana, lakini mtu ambaye anaweza kutegua kitenda wili hicho ni Waziri mkuu.

Yeye waziri Mkuu ndiye awezae kuthibitisha kama alishauliwa ama vipi? Rusha hili swali kwa PM amalize mchezo.
 
Kwani Magufuli anaheshimu katiba?

Alimteua marehemu Dr. Mahiga ubunge. Kabla Dr. Mahiga hajaapishwa ubunge, maana yake kabla hajawa mbunge kisheria, Magufuli akamuapisha Dr. Mahiga uwaziri.

Kitu ambacho ni kinyume na katiba. Kwa sababu Waziri anatakiwa awe mbunge. Na mbunge wa kuteuliwa na rais hawezi kutimiza ubunge mpaka aapishwe na Spika.

Kwa hiyo, Dr. Mahiga aliapishwa kuwa waziri bila ya kuwa mbunge.

Magufuli hajali.
 
Umeandika vizuri sana, lakini mtu ambaye anaweza kutegua kitenda wili hicho ni Waziri mkuu.

Yeye waziri Mkuu ndiye awezae kuthibitisha kama alishauliwa ama vipi? Rusha hili swali kwa PM amalize mchezo.
We unafikiri akiulizwa atasemaje??
 
Usisahahu KABLA matokeo kutangazwa, JMT ilikuwa na Rais na PM halali kabisa! Hao ndio walioteua majina hayo mawili ya mawaziri.
 
Umezungumzia kiapo, hiki kiapo cha kuandikiwa... huwa wanasoma tu ilivyoandikwa na kisha kutupa ile karatasi.

Kiapo ni utopolo ulioandikwa vizuri!
 
Back
Top Bottom