Hivi unajua unemployment rate ya Marekani? Kama tunatolea mfano Marekani kwa ubora wa sera zao za ndani na za nje ,mbona ukweli ulio mchungu hausemwi kwamba bado tatizo la ajira ni sugu hata kwao.
Hili sio nililotaka kusema lakini ni katika kukazia hoja ya usugu ya tatizo la ajira.
Tanzania ni nchi ambayo vijana wanakimbia shule wakiamini katika kujiajiri na baadae wanalalamika wakiona umri unasogea na hakuna walichobahatika nacho kwenye kujiajiri. Kwa mfano mtaani kwetu, vijana wengi ambao hata kidato Cha nne hawajamaliza wameacha shule wanajiingiza kwenye bodaboda na kamari
Hili kundi halitiliwi maanani Sasa lakini miaka kumi ijayo watakuja kusema ajira ni tatizo na wataonekana wana hoja kwa Sababu hatujifunzi kutokana na historia ya zamani.
Matokeo yake linatengenezwa tatizo lisilotatulika la ajira kwa watu hao. Mtu kama huyo hata ukimpa pikipiki awe bodaboda hatofanya Kama msomi wa Elimu ya kati achilia Elimu ya juu.
Tukirudi kwenye hoja yako , nchi za wenzetu tatizo la ajira halina usugu Kama kwetu kwa Sababu vijana walisoma na wakaelimika na bado wanaweza kutumia Elimu zao kujikwamu na akishughulisha na boda anafanya kisomi, ujasirimali anafnaya kisomi