Je, Rais anao mpango wowote kuhusu ajira kwa vijana au anasubiri kampeni?

Je, Rais anao mpango wowote kuhusu ajira kwa vijana au anasubiri kampeni?

Duniani Kote kuna ajira za aina 2.
1. Za Serikali - hizo ajira za uwalimu, Udaktari etc.
2. Za Binafsi
Serikali inatakiwa kuwa na mipango endelevu ya kuwezesha Graduates kujiajiri. Kwa Tanzania haya Mazingira yamejaa Bra bra nyingi mno kuliko uhalisia.Tatizo lipo hapo
Pia ishu ya upatikanaji wa mitaji naona linasahaulika.
 
Watu wanaropoka sana juu ya kujiajiri. Ila hawazungumzii mtaji. Labda uwe unatumia ndumba/uchawi kwenye biashara. Na watu sikuhizi pesa hawana ya kununua vitu. Na biashara zimekuwa nyingi mno kuliko wateja.


Jamaa yangu ametangaza biashara kila sehemu mpaka Instagram wanamdai, ila biashara haikui, na wateja ni changamoto.



Inatakiwa papatikane suluhisho. Hizi siasa zitaleta majanga.
Mabeyo alisema ukweli hajui kazi ingine zaidi ya jeshi, kupewa kazi ya kulinda faru ngorongoro
 
Mabeyo alisema ukweli hajui kazi ingine zaidi ya jeshi, kupewa kazi ya kulinda faru ngorongoro
Kujiajiri sio jambo rahisi kama watu wanavyodhania. Ukiona unabiashara yako inaenda mshukuru Mungu. Ila pia usiombe waje washindani yaani hutaamini macho yako 😂. Huuzi hata kidogo.
 
Hili janga la ukosefu wa ajira naona kama linazimwa hivi.

Je, kuna mpango wowote wa kutatua?

Au tusubirie saundi za kwenye kampeni.
Vijana kwenye hili taifa tumeshatolewa kafara. Hili la ajira wameshashindwa tena vibaya. Idadi ya unemployment inakuwa na ni kubwa sana kwa sasa. Katika vijana kumi ni vijana kumi hawana ajira.
 
Vijana kwenye hili taifa tumeshatolewa kafara. Hili la ajira wameshashindwa tena vibaya. Idadi ya unemployment inakuwa na ni kubwa sana kwa sasa. Katika vijana kumi ni vijana kumi hawana ajira.
Yaani mkuu huo ndio ukweli. Yaani majobless wameongezeka na wanazidi kuongezeka. Na wazee wamegoma kustaafu ni mwendo wa Teuzi tu. Yaani hapo Mungu mweyewe ndio atawastaafisha.


Nahisi kipengele cha hali ya ajira kingewekwa kwenye sensa ya mwaka huu.


Na huo utafiti wa kati ya vijana 10 ni 10 hawana ajira. Nahisi umepunguza makali. Naona kati ya vijana 10 ni vijana 15 hadi 20 hawana ajira, maana watoto/vijana walio bado kwenye elimu sioni kama watapata ajira huko mbele. Labda wapate ajira kwenye makampuni ya wazazi wao au nje ya nchi.



Halafu wajasiriamali/wafanyabiashara wamekuwa wengi kuliko wateja. Labda watanzania tuanze kuexport.
 
Ukweli ni kuwa serikali kuajiri wanaograduate wote huo uwezo haupo si Tanzania tu ila hata mbali huko kwa wenzetu ila sasa zipo njia nyingi za kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira kama ÷
Serikali kupunguza miaka ya kustaafu ili walio mtaani pia wapate muda wa kulitumikia taifa

Serikali kupunguza au kuacha kudaili wanafunzi katika kozi ambazo hazina uhitaji nchini.

Serikali kuweka mkazo tena katika elimu na kutoa elimu iliyo bora kama ya zamani sio leo kila mtoto kupata division one ni jambo la kawaida kitu ambacho kwa akili za kawaida sio sawa lakini pia mitaala ijielekeze kwenye kumpa mtu uwezo wa kujitegemea na sio kutegemea ajira.

Serikali itoe mikopo yenye mashariti nafuu na ziwepo njia madhubuti za kuwasaidia wananchi kupitia mikopo hiyo Sio leo mikopo nimpaka uhonge ili upate mkopo No.

Ni haya ambayo ukiyageuza ndiyo chanzo cha ukosefu wa ajira kwa walio wengi .

Ni ndoto Tanzania yangu kuyafanya ila naamini kizazi ubadilika hivyo wakati waja tuusubiri.

TEKERI
 
Back
Top Bottom