Je, Rais Magufuli amepuuza ushauri uliotolewa na viongozi wastaafu?

Je, Rais Magufuli amepuuza ushauri uliotolewa na viongozi wastaafu?

Kiukweli siwajui wateule wowote ambao wanaonyesha wazi hawataki kuendesha utawala wa sheria katika maeneo yao, ndio maana niuliza ututajie. Na kukusisitiza, ukiwataja, utaje na ni maeneo ya utawala wa sheria waliyoyakiuka.

Sio vibaya na ukatuwekea mifano angalau mmoja wa hayo matamko ya ajabu ajabu yanayotolewa na wateule hao wa Rais, kiasi cha kuona kama nchi haitawaliwi tena na sheria na badala yake tunatawaliwa na matamko ya kisiasa ya wateule hao wamayoyatoa majukwaani!.
P.
Pascal ni wazi kabisa kuanzia yeye mwenyewe hafuati sheria, nikuulize ni kwa sheria ipi kuzuia mikutano ya siasa nnchi nzima?. Huu ni mfano mmoja ambao yeye mwenyewe amehusika kwa kutamka na mara moja ikawa sheria. Sasa kwa wateule iko mingi. Juzi juzi nimemsikia Dc wa Arumeru akimaudit mbunge wa meru kwanini hafiki ofisini kweli ndio kazi aliomteua kufanya?. Kimsingi kila kiongozi kwenye awamu hii wanajiona wako juu ya sheria. Juzi tu issue ya makontena ni matokeo ya viongozi kutofuata sheria na kuongoza kufuata mipaka ya uongozi! Pascal haya mambo yashakuwa ya kawaida nnchi hii kwa sasa sikutarajia ungeuliza swali la aina hii.
 
Mkuu Pasco!
Nakusalim!
Tafadhari! Na kwa heshima na taadhima, naomba unitajie Ibara ya Katiba ya JMT inayosema rais wetu (sio Rais Magufuli) "halazimishwi kufuata USHAURI wa mtu YEYOTE" na "atafikia maamuzi...peke yake"
Na kama hivyo ulivyosema ndivyo ilivyo;

1. Kwanini tuwe na Bunge, Mahakama na Tume ya Haki za Binadamu nk, na Wizara ya Sheria na Sheria zenyewe per se? Vya Nini na vinamshauri nani? (soma Ibara: [ 35.-(1) ] ya Katiba ya Nchi).

2. Kwa mtazamo wako na kauli yako hii, na baadhi ya vitendo na kauli za 'Serikali' dhidi ya upinzani bungemi na nje ya Bunge, hazikinzani na misingi ya democracy, ikiwa ni PAMOJA na uhuru wa kujieleza, haki ya kuchagua na kuchaguliwa nk, kwa mujibu wa Katiba?

3. Je, kwa mujibu wa Katiba, Rais yuko juu ya Katiba na sheria?

Najiuliza mengi zaidi ya hayo kwasababu ukishataja Katiba ya Nchi siwezi kuacha kufanya marejesho ili nijiridhishe kama lisemwalo lipo au uzushi!

Tunaweza kukejeli, kuminya au kuzuia watu kusema, lakini hatuwezi kumzuia binadamu mwenye afya na akili timamu, hata awe mtumwa, KUFIKIRI.
Mkuu umeongea hoja ya msingi sana......

Pascal anatuambia kuwa Rais wa nchi hii HALAZIMISHWI kufuata ushauri wa mtu yeyote!

Umempa challenge akuonyeshe ibara inayosema hivyo

Akikujibu nitag
 
Back
Top Bottom