Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndiyo mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo?

Kesi ya Sabaya ipo mahakamani acha mahakama iamue.
Kama unajua tabia za Sabaya hii ni mara yake ya pili kusimama mbele ya Pilato kwa makosa haya haya.
Mara ya kwanza alibebwa ila sasa hivi kisu kimegusa mfupa.
 
Kwa hiyo viongozi/wafanyakazi wa usalama wana haki ya kuiba ama kufanya uhalifu wowote kwa kadiri wanavyojisikia?
Neno ''wanavyojisia'' halipo kwenye majukumu ya ofisa wa Usalama wa Taifa!

Hoja ya msingi ni kuwa utajuaje kama alichofanya amekifanya kama ''anavyojisikia'' na sio kama ''alivyotumwa''.

Wenye historia ya nchi hii tunajua kuwa wakati wa vita vya uhujumu uchumi vilivyoongozwa na Marehemu Sokoine wakati wa utawala wa Nyerere, kuna watu wa usalama wa taifa ilibidi waonekane kama wamekamatwa na kupelekwa gerezani kama wahujumu uchumi lakini kiuhalisia walikuwa kazini kwenda kuwapeleleza mahabusu wengine waliokamatwa kwa kesi hizo.
 
Nimekusoma nimekuelewa vizuri kusema kweli, na zaidi hapo kwa Samia nikikazia kidogo ni kwamba hakujua hata kama Magufuli amefariki, wakati wenzake wanajipanga watoke vipi, yeye akapangiwa ziara akaenda Morogoro kama sijakosea.

Inasemekeana kina Mabeyo ndio waliokuja kumuokoa na kumrudisha kwenye chati, vinginevyo huyu aliekuwa makamu wa Rais alishakubali kutumwa na waliokuwa chini yake kimamlaka na akakubali kutumwa nao, ndio maana hata leo sishangai serikali yake kuwa na mambo ya kubahatisha tu, kama kuteua na kutengua within minutes.

- Hizi kesi za kina Sabaya nazo ni kama ulivyosema, kutuzuga tu, japo kupruv kosa la ubakaji ni vigumu mahakamani, lakini kuna makosa mengine kama kuvamia hoteli ya Mbowe usiku akiwa na silaha na ushahidi wa CCTV Camera upo yalitakiwa yafunguliwe dhidi yake, au kama ni Mbowe ndie anatakiwa kumshtaki na yupo kimya I don't know, ila sio wizi wa simu ya tecno.
 
Umeongea vitu makini sana...
 
Nlishangaa kusikia shahidi wa kwanza ambaye ni mmiliki wa duka anasema hakuwepo dukani wakati wa tukio Bali alisimuliwa, shahidi wa pili nae akasema alivamiwa na kundi,
Hivyo mpaka hapo, Sabaya kishashinda kesi.
Ni sawa, classified information kufichwa kwa baadhi ya viongozi.
Kuna aina ya taarifa, anapaswa awe nazo rais peke yake
 
Unalazimisha hoja.Subiri tunywe chai kwanza.
 
wapumbavu hao majambazi kina sabaya ndio unaleta huku hao ccm wanajuana tu hakuna briefing wala nn in short hata hao usalama wenyew ni wajinga hawezi kifanya nchi iwe tajiri wamebanza kuoendelea maccm akati akili kubwa ziko upinzani kwa maendeleo ya taifa
 
Kabla haujauliza swali ulitakiwa kwanza ujue kazi za watu wa Usalama wa Taifa!

Jibu la swali liko kwenye kazi za ofisa wa Usalama wa Taifa!
Nini unataka kusema?
Kwamba Sabaya ni afisa wa usalama wa taifa? Kama ni ndio kuna kipindi alishawahi kushtakiwa kwa kujifanya usalama wa taifa?
Taifa hili usalama wa taifa ni watu wa hovyo tu isipokuwa wachache sana wanaoijua vyema kazi yao.
 
Umewahi kujiuliza kama hao unaodai ni wapinzani wananunuliwa wakati kumbe hao pia ni sehemu ya ''system''!

Kama tunamjadili Makamu wa Rais asiyejua kinachoendelea nchini utawezaje wewe kujua wakati hata mlango wa Ikulu hujui umekaa upande gani?
 
Very well written. Urais ni taasisi, kwa sasa mama kakaa kitaasisi kweli kweli.
Mama alitakiwa akae kitaasisi wakati akiwa Makamu wa Rais! Ni kosa kubwa kwa Makamu wa Rais tena aliyekaa kwa miaka zaidi ya mitano lakini hajui kinachoendelea nchini!
 
Usiamini direct kuwa Magufuli alikosea kumtumbua Diwani na kumteua Mkurugenzi wa mkoa wa Kagera. Intelligence agencies hazifanyi kazi kwa mtiririko, muda wowote wanamfanyia demotion mwandamizi wao na kumpima uwezo wake kukaa nje ya system bila kuihujumu au kuwa na kinyongo.
Au wanampa likizo ya kumpunguzia kazi kwa kumteua nafasi isiyochosha hasa akiwa ametimiza jukumu kubwa aliloagizwa.
Au wanamuondoa sehemu ili kulinda identity yake kama inahisiwa ameanza kujulikana na hapa lazima aonekane amefukuzwa na demoted.

Mwisho ndio hiyo anakuwa demoted kiukweli kwa vile kakosea. So ni vigumu kujua sababu
 
Mkuu una point sana . Unachokiongea ni kweli kwa sababu huwezi niambia kuwa huo mfumo unachagua baadhi ya watu ambao in deep down hawana uwezo wa kujenga hoja bungeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…