Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndiyo mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo?

......vinapoteua wagombea Urais ambapo huanza kupewa intelligence briefings ili wakati wa kampeni wajue ni mambo gani wanatakiwa wayaseme kwenye mikutano ya hadhara ili kulinda maslahi ya taifa.
Nawaza wagombea wetu wote mfano hii ya 2020....wapewe intel briefing ili waweke sawa kampeni zao!. Hii kitu mkuu hakiwezi kunakiliwa kama kilivyo kisha kukitupa huku kwetu. Nina imani umejua ninachokimaaanisha.
 
Ninakubali kuna taarifa zingine anapaswa Rais pekee azijue lakini anayofanya Rais Samia yanaonyesha hata yale aliyokuwa anapaswa kuyajua alikuwa hayajui! Hii sio sawa kama taifa endelevu!
 
Ninasikitika kuwa maandishi yako hayaeleweki!

Kama kuandika maneno/sentesi sahihi ni tatizo, sidhani kama utaweza kujenga hoja yenye nguvu za hoja!

Samahani kama nitakukwaza!
 
Hili ni jukwaa la kujenga hoja na kuzijibu kwa nguvu za hoja!

Kusema tu ''nalazimisha hoja'' bila kunyambulisha kivipi unakuwa kama mtu anayepiga kelele bila kueleza sababu yake!
Kwa nini huwa unamtetea huyo kibaka mwenye tuhuma za kijingajinga? Halafu unataka kutueleza kwamba "Ole Mungiki" mwenye tabia sugu za uhalifu(rejea alivyojifanya TISS halafu akakwama) kwamba hawezi kuiba simu?Ulitaka aibe,apore nini weye ndiyo ingekuingia akilini kwamba amefuzu ukibaka?
Unajua kwamba kuna watu wazima,kwa sababu wana tabia za udokozi,hawajaacha kudokoa mboga hadi wanafika late 50's?
 
Nini unataka kusema?
Kwamba Sabaya ni afisa wa usalama wa taifa? Kama ni ndio kuna kipindi alishawahi kushtakiwa kwa kujifanya usalama wa taifa?
Taifa hili usalama wa taifa ni watu wa hovyo tu isipokuwa wachache sana wanaoijua vyema kazi yao.
Ni wapi nimesema Sabaya ni Usalama wa Taifa?

Kama Sabaya alishitakiwa kwa kujifanya Usalama wa Taifa, kesi yake iliishaje? Mkuu, think bigger!
 
"System ya utawala"?
Aliyokuwa akifanya Sabaya iwe ni 'system ya utawala', kweli? 'System hiyo itakuwa na kasoro kubwa sana!

Niseme tu kwamba makala yako ni nzuri kuisoma, hata kama baadhi ya yaliyomo yanaonyesha kwamba tuna mfumo mbaya.

BTW: "TO DARE IS TO DO, WHO DARES WINS" - Says who? Ain't necessarily so!
 
Mkuu nashukuru kwa angalizo lako! Tuendelee kuelimishana kwa manufaa ya taifa letu!
Si kwamba anakusifu.Amekueleza jinsi hadithi zako "zinafikirisha" na ni za kutunga hewani!Halafu huyo unayetaka utuaminishe ni "mtu fulani" asingekuwa anafanya Makosa ya kipuuzi namna hiyo!Angeshafifishwa au kuwa "ghosted" siku nyiiiingiii!Muache tu apokee "ujira" wake kwa kujitwisha koti lisilomtosha.
 
Tatizo unajenga hoja huku umetanguliza emotional reasoning! Tumia logical thinking ili ufikie hitimisho sahihi!
 
Yaani lisu mlopokaji ateuliwe na CHADEMA hiihii ya vilaza aanze kupeww inteljensia reports za kitaifa .

Hoja yako ulianza vema Aya ya mwisho umeharibu


USSR
 
Mkuu Zanzibar-ASP ,Kongole sana. Umemaliza kila kitu kwa maandishi machache.
CC ya CCM ndio kila ujinga unaanzia huko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…