Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndiyo mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo?

Sabaya anakesi mbili kwa mahakimu tofauti hiyo ya ujambazi upelelezi umekamilika ile ya utakatishaji fedha bado
Zile za ngono zembe zake zinamsubiri Moshi
Source----Raia mwema na Millard Ayo on line tv
 
Bro una hoja nzuri sana ila naona hutaki kukosolewa. naomba nikuulize kwa mazingira gani tuseme basi Sabaya yupo gerezani/ mahabusu kaenda kumhoji nani ambaye yupo kwenye top list ya ma files ya TISS
Bro kama umenisoma vizuri nimesema Rais Samia anaonekana alikuwa hajui kinachoendelea nchini ndiyo maana alipoingia madarakani akaanza kutoa maagizo ya kufanya chunguzi mbali mbali ambazo chanzo chake ni kwenye mitandao ya kijamii kwa watu ambao pia hawajui kinachoendelea nchini!

Kwa sasa baada ya kuanza kuujua ''ukweli'' ameanza kubadilika! Kwa hiyo kuna uwezekano hata kina Sabaya tukawaona wako nje!

Nimetoa mfano wa wakati wa utawala wa Nyerere sio kwamba ndicho kinachoendelea kwa sasa kwa sababu mazingira ya sasa ni tofauti!
 
Rejea kuondolewa kwa Gen Kombe...waliomwondoa Mzee Mkapa aliwapa msamaha kwa sababu ni state task
 

Mkuu umetoa sifa za kijinga mpaka umeonekana kama mtoto wa kidato cha pili. Rais sasa ndio amepewa sifa za ulinzi wa nchi wakati ameshindwa hata kuwakamata waliojiunganishia bomba la mafuta hapa mjini?!.Ukiona wazungu wanatuita manyani ujue hawajakosea.
 
Sometime is better to blame the system, na sio kiongozi, maana inaonesha kiongoz akishika madaraka, zile siku za mwanzo anakuwa na nia njema ya kuwatumikia wananchi, lkn baada ya muda mfupi anarudishwa ktk factory reset ya system iliyomuweka madarakan kwa kufanya na kufuata agenda nzma za system bila kuvunja mashart, ndio kama muonavyo kwa samia, mwanzo inawezekana hakujua hali ikoje ktk utawala.lkn baada ya kuingia ndyo anaanza kuwekwa sawa na wenyenchi yao...ccm ni ilee ilee
 
Nawaza wagombea wetu wote mfano hii ya 2020....wapewe intel briefing ili waweke sawa kampeni zao!. Hii kitu mkuu hakiwezi kunakiliwa kama kilivyo kisha kukitupa huku kwetu. Nina imani umejua ninachokimaaanisha.
Ndio maana sikutaka kujikita zaidi kwenye wagombea Urais kupata intel briefing kwa sababu siasa zetu bado ni changa sana!

Nimejikita kwa Makamu wa Rais kwa sababu kiuhalisia anakuwa ni Rais wa nchi wakati wowote kama la kutokea litatokea!

Sio unakuwa na Makamu wa Rais halafu la kutokea likitokea nchi inakuwa kama ndio imemaliza Uchaguzi Mkuu na inakuwa kwenye transition period!
 

..kwamba upo uwezekano Sabaya alitumwa na "system" kuvamia hoteli ya Mbowe?

..pia upo uwezekano "system" ilimuelekeza atumie gari yenye namba feki za UN?

..Na "system" haikuhakikisha kwamba Sabaya hataonekana ktk CCTV camera?

..nadhani umeidharau sana "system" kiasi cha kufikiria inaweza kushiriki jambo la kipumbavu namna ile.

..kwa upande mwingine "system" inaundwa na binadamu kama mimi na wewe, na kila binadamu ana mapungufu.
 
Watu wa system ya utawala kwa ivo watawala wafanye makosa yote wasiwajibishwe.

Acha kuandika conspiracy zisizo na maana na kuwajaza wafu misinformation ambazo hazina misingi yeyote. When a President is A President. Bahati mbaya sana Tanzania tuna Vice President na si Deputy President

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Utawala wa Magufuli ulikuwa ni utawala wa aina yake. Samia alikuwa ni kama mtu wa pembeni na hakuaminiwa na Magufuli kwa siri nyingi, hivyo hata kama kungekuwa na briefying kwa vice president bado tu angebaniwa. Samia alikuwa anaonekana kama ni informer wa kambi ya Msoga ambayo nayo haikuwa ''inaiva'' sana na marehemu. Mpaka Magufuli kuugua Samia alikuwa hajui undani wa kinachoendelea na mpaka siku alipofariki hakupata habari mapema. Mwisho: nina uhakika wa 100% Magufuli angejua kuwa hatamaliza kipindi chake cha pili, uchaguzi wa 2020 angechagua makamu mwingine au angebadili katiba ili makamu wa mgombea wa urais wa jamhuri atoke bara pia!
 
Na watanzania wanapenda conspiracy kama hizi hakuna mfano.
 
Msingi wa hoja yangu alitakiwa aive wakati akiwa Makamu wa Rais!
Nani alikwambia hakuiva? Equivocal unamanisha pia JPM hakuwa ameiva alipokua Rais tayari?...manake umefanya judgement ya maamuzi yake alipokua rais kuwa hakujua mfumo blah blah, Once you're a President You Are The President acha kabisa kudanganya watu

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…