Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndiyo mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo?

Uko right. Kwa mfumo huu hata aingie nani hawezi ku-perform vizuri. Kitu cha kwanza ni kuwa mfumo unamfanya rais achanganyikiwe kwa sababu anakutana na vitu vingi sana vya kufanya. Akishachanganyikiwa ndiyo anaanza kulainika na wapambe ndiyo wanaingia kufanya yao. Kumbuka kuna watu huu mfumo ndiyo kula yao na hawatakubali hata siku moja ubadilike.
 
Sabaya anaweza akawa huru mwakani tarehe kama ya leo
 
Kwani ukiwa usalama wa taifa ukiwa mwizi haushugulikiwi?

Acha upumbavu basi

Hakuna usalama yeyote anawezafanya kosa la jinai na akaachwa labda kwenye mfumo kama wetu uliasisiwa na ccm na magenge yake.

Acha ushamba.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Kwamba Sabaya anaenda kuiba simu aina ya Techno kwa kutumia silaha! Nchi hii kuna sanaa na maigizo ya aina yake!
Hilo gazeti refuuu uliooandika hapo juu kumbe lengo ilikuwa kumtetea jambazi mwenzio Sabaya?

Sijui classified intelligence briefing,sijui kitu gani..... Usalama wa taifa wanaruhusiwa kuwa wahalifu...unajaribu kutuaminisha nini?

Kama ni kweli unayosema basi nchi hii inatawaliwa na genge la wahuni. Bahati nzuri unayosema siyo ya kweli!
 
Bandiko lako hili limenifikirisha tukio la intel wa UK kuacha nyaraka za siri stendi kuhusu ile meli ya kupita karibu na Crimea!!! Je. Press ilikuwa inatudharau sisi wasomaji ama UK intel iliteleza kweli!?
 
..Je, WIZI huo ulitokea?

..SABAYA alikuwepo ENEO la tukio?

..kama alikuwepo, alikuwa na SILAHA YA MOTO?
Hivi kama watu wanatangaza wana uwezo wa kumnyoa ng'ombe dume; ndama jeuri ataipata wapi? Nadhani wana namna nyingi ya unyoaji huu waweza kuwa mmojawapo.

Sijui nasomeka, kweli?
 
Kwa hiyo viongozi/wafanyakazi wa usalama wana haki ya kuiba ama kufanya uhalifu wowote kwa kadiri wanavyojisikia?
Huyo ni boya ajui uchunguzi na ukaguzi anao fanya mama ni bosheni tu kwa sababu ya kivuli cha magufuli
 
Kuwa usalama wa taifa sio kinga ya kufanya uhalifu.
 
Umeandika utumbo mtupu. Usalama wa taifa sio tiketi ya kufanya maovu. Huyo mumeo Sabaya unayemtetea kafanya maovu yasiyohitaji maelezo mengi zaidi ya kumfikisha mahakamani. Kamati ya maadili ya CCM ndo kila kitu nchi hii. Muulize Lowassa atakupa jibu sahihi kuhusu hiyo kamati.
 
Nini unataka kusema?
Kwamba Sabaya ni afisa wa usalama wa taifa? Kama ni ndio kuna kipindi alishawahi kushtakiwa kwa kujifanya usalama wa taifa?
Taifa hili usalama wa taifa ni watu wa hovyo tu isipokuwa wachache sana wanaoijua vyema kazi yao.
Jamaa ni bora ndo maana tuko salama hata leo...tusifie vyetu, tutasifia cia mpaka lini !? Ajionavyo mtu ....
 
Na wengine walipotoka huko wakaoata na U DC U RDD na ukadhalika
 
Mkuu wa wilaya anasimamia miradi ya mabilioni ya shilingi na dola ndo akaibe shi 3milioni na simu ya tecno kweli haiingii akilini kabisa
Mwizi ni mwizi tu, hata ufagio ataiba !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…