Je, Rais Samia alikuwa haaminiki au ndiyo mfumo wa ulinzi na usalama ulivyo?

Na ndio asilimia 75 ya viongozi wote..
 
Mkuu, Inawezekana kwa sasa lakini hayati Nyerere alikuwa na huo utaratibu na ulikuwepo pia wakti wa Mwinyi, Kikwete na Mkapa.

Alipoingia hayati JPM palikuwepo vurugu na hivyohivyo alipoingia mama Samia.

Ila utaratibu wa SB umekuwepo siku zote.

Huanzia na magazeti muhimu ya siku hiyo kisha kuketi na DG au msaidizi.

Sasa hata haya magazeti yetu ya leo mengi si makini.

Zamani ukimsoma mtu kama Charles Kizigha au Lucas Liganga unafahamu utapata kitu muhimu.
 
Kama watu wa usalama wa taifa ndo kama akina sabaya na wengine wengi tu wenye madudu mengi basi kazi ipo nchi hii
 
Kama watu wa usalama wa taifa ndo kama akina sabaya na wengine wengi tu wenye madudu mengi basi kazi ipo nchi hii
Mkuu hii ni kwa taarifa yako tu ktk kila watu 10 unawajua ww 4 -5 ni UT(usalama wa taifa)..

Sabaya Wala Hana kesi ni vijimambo tu, mama alikosea kwa kukoseshwa ila soon he will be free.. stay tuned..
 
The Presidency is not shared.

Commander in Chief ni mmoja kwa wakati mmoja, hata Marekani pamoja ni briefings wanazopewa, bado wanachopata ni peanuts ukilinganisha na anachopewa CiC. Ndio changamoto za kazi, Marais wote huwa wanaanza na blunder za hapa na pale.
 
Nasubiri kuona...

Sabaya atatoka auatafungwa?!

Tutaanzia hapo..
 
Nadhan hz brief anapewa mgombea wa ccm km zp baadhi
 
Bro una hoja nzuri sana ila naona hutaki kukosolewa. naomba nikuulize kwa mazingira gani tuseme basi Sabaya yupo gerezani/ mahabusu kaenda kumhoji nani ambaye yupo kwenye top list ya ma files ya TISS

Nadhani Mkuu unapaswa kutulia na usome na kuelewa mantiki nzima ya bandiko la mtoa Mada.
 
Af mdau inaonekana hataki kukosolewa yaani

Tatizo siyo kukosolewa,nachokiona hapa wewe binafsi ndiyo hujaelewa mantiki nzima ya bandiko lake.Ukielewa unaweza kuja na hoja za msingi pia za kumkosoa,wewe hapa unakwenda kushoto wakati mada inakwenda kulia.Hapo ndipo tatizo la “ukosoaji” wako linapoanzia.
 
kamati ya maadili? Maadili gani ya kimaku ya kuwateuwa majangili kuwa maDC ?Nani anafanya vetting? Anyway time I'll tell.
 
Ulevi wa Madaraka hauendani kabisa na mambo ya kiusalama.
Jamaa alikua mlevi wa Madaraka na asiingizwe/asiusishwe kabisa kwenye mfumo maana atachafua taswira nzima ya mfumo Bora na msafi wa kiusalama wa Nchi yetu Tanzania.
 
Na tumkumbushe tu kuna mmiliki wa mabasi fulani hadi leo ni mwizi wa simu kwenye ma grocery
 
Kwa Marekani hata raisi aliyestaafu ana aceess ya kupewa intelligence briefing. kwa hapa TZ bado sana
 
Kwamba Sabaya anaenda kuiba simu aina ya Techno kwa kutumia silaha! Nchi hii kuna sanaa na maigizo ya aina yake!
Hata mimi nashangaa jambo hilo lilivyovurugwa kitaalamu!

Uzushi tuliosadikishwa raia na namna mashitaka yalivyoandaliwa na wanaojiita wanasheria wabobezi ni mambo mawili tofauti na ni ya kustaajabisha sana.

Hivi kiongozi kutenda makosa katika kutekeleza majukumu yake kisheria(kuchukua na kuomba rushwa), waweza kumuandika mashitaka ya ujambazi wa kutumia silaha?

Ninadhani hapa kuna namna ya kulimaliza suala hili bila hatua yoyote kuchukuliwa!

Ni yale yale ya Zombe na genge lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nini unataka kusema?
Kwamba Sabaya ni afisa wa usalama wa taifa? Kama ni ndio kuna kipindi alishawahi kushtakiwa kwa kujifanya usalama wa taifa?
Taifa hili usalama wa taifa ni watu wa hovyo tu isipokuwa wachache sana wanaoijua vyema kazi yao.
Tunaweza kuamini hivyo kwamba ni 'Tiss', sababu kwenye kesi hiyo ya kitambulisho ambacho alikamatwa nacho red handed, mwisho wa siku serikali ilinywea!

Eti haioni faida ya kuendelea na kesi ya mtu aliyefoji nyaraka muhimu za serikali!

Vichekesho sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kama ni hivyo kwa nini wanasubiri mpaka chama kikuteue mgombea ndio wakupe briefings?

kwani siku unapopanda jukwaani na kutangaza nagombea huwezi kuanza kuropoka mambo yasiyo na maslahi ya Taifa ?

Acha kutuongopea hapa wewe bana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…