Je, Rais Samia anayo haki na misingi ya kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) kwa mambo yasiyo ya Muungano?

Hoja yako ni mufilisi.
Eti hoja mufilisi... hoja mufilisi au HUELEWI!!
Huwezi kutenganisha Urais alioupata Samia bila kuweka Uzanzibari wake.
Kwahiyo kama angekuwa amegombea, ndo angeweza kuongoza mambo ya bara yasiyo ya muungano?!

REMEMBER, kama angegombea usingeangaliwa u-ZNZ wake bali Utanzania wake!!

Na kwa mawazo yako, kwavile hakugombea basi mamlaka yake yanakuwa tofauti kulinganisha kama angegombea wakati anatumia katiba ile ile na sheria zile zile?! Kwamba, kwavile ametokea kuwa VP, basi urais wake hauwezi kuwa kama yule ambae aligombea?!
Katiba imetamka, Rais akifariki, Makamu( ambaye ni lazima atoke Zanzibar) anarithi kiti. Sasa unatenganishaje haya mawili.
Sio kutenganisha... niliweka wazi mapema kwa sababu nilishashuku kwamba huenda unau-judge urais wake sio kama rais bali kama rais aliyekuja kuwa rais akitokea kuwa VP!

Unashindwa kufahamu kwamba, a moment alipoapishwa, huyu akawa rais na u-VP wake ukakoma hapo!

Na kwavile akaja kuwa rais, ana wajibu na mamlaka ya kuhudumu kama rais bila kuangalia kama alisimama majukwaani kuomba achaguliwe kuwa rais, au vinginevyo!

Muhimu ni kwamba, urais wake ni halali kwa mujibu wa katiba!
Lakini hoja yangu sio Samia kuwa Rais wa JMT. Hoja yangu ni Samia kuongoza mambo ambayo siyo ya muungano as per constitution. Over!!!!!
Na nimeshakuambia, sifa ya mtu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kwa mhusika kuwa raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano, PERIOD!

Na hakuna popote kwenye katiba panaposema rais aliyechaguliwa majukumu yake ni haya, na yule ambae ameingia akitokea kuwa VP, majukumu yake ni haya!

Na hakuna inaposema Rais wa Jamhuri anayetokea ZNZ majukumu yake ni haya na yule anayetokea bara, majukumu yake ni haya!

Na katiba haijasema kwa sababu hicho kingekuwa ni kiroja!!
 
Hatujaanza leo wala jana kulitumia zao la muungano kwa faida ya wote.

Makamu wa JK alikuwa Profesa Gharib, lolote lingempata JK Profesa angemalizia muda uliobaki.

Ndio aina ya muungano tulionao tuna haki sawa.
 
You could have raised that query by then, ila kwa sasa usinipangie cha kuuliza. Baki kwenye hoja yangu, ila usinipangie cha kuuliza sasa au kwa nini sikuiliza kabla.
Tuwe wapole tu huyu Mama ndio rais wetu kuelekea 2025 na Mpango makamu wake.

Nafasi ya urais haikubaliani na ombwe hata siku moja. JPM alipolala usingizi wa milele yule aliyetembea nae muda wote wakati wa kampeni ndio kavaa viatu vyake.

Ni takwa la kikatiba hayawi mapenzi ya mtu binafsi.
 
Wewe ni mfinyu kiakili na bado ni mtoto sababu kwanza inaonekana kabla hujaleta hii hoja hukusumbua kichwa chako kujiuliza maswali. Hoja yako kwa sasa haina mashiko kutokana na katiba tuliyonayo ambayo haiwezi kuondoa uhalali wa mama kuwa Rais. Aidha ninachokiona hapa kwenye hoja yako ni mama kuwa Rais, sivyo ungehoji kwa nini mzee Ruksa alipelekwa Ikulu 1985-1995 kwa katiba hii hii ambayo leo unaiona mbovu. Sasa mshachelewa Mama Samia kwa sasa ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa katiba hii unayoiona leo ni mbaya baada ya kifo cha Dikteta Magufuri. Nakushauri kakae na mkeo mjue maisha yataendaje
 
Mzee nilikuwa sijakuelewa kutokana heading ila nimesoma mara mbili mbili nimekuelewa. Kudos
 
Suluhisho ni tatu au moja basi
 
Kwani Magufuli alikuwa anawatawala hadi mambo yenu ambayo sio ya Muungano??.
Hapa issue ni kuwa hatutaki kutawaliwa na Mzanzibari hadi kwenye mambo ambayo sio ya Muungano.huyo Ali Hassan ana bahati watu wengi walikuwa hawana shule.
siyo kweli, G55 ilikuwa 1993 wakati wa utawala wa Mwinyi Ali Hassan
 

Acha uzwazwa, sasa umejibu hoja au umeleta historia?

Hivi ninyi kizazi cha 70 mnashida gani? Mbona mnaonekana wote ni mburulaz?

Changia hoja kama huna soma na pita kimya
 
Anavyoandika kuhusu wazanzibari utadhani hawana uhusiano kabisa na watu wa huku bara.

Hajui kuwa wajomba na baba wadogo wa huyo Rais wa sasa wana asili ya huku.

Hajui historia ya Karume kuwa asili yake ni huku bara.

Akiambiwa kuwa hii mada ina ubaguzi ndani yake analeta ubishi wakati kila kitu kipo bayana kabisa.
 
Baadae ataanza ya kanda, maeneo fulani weshatoa maraisi fulani ila bado maeneo fulani..


Alotupiga zongo keshafariki..... Sisi vijana na wazee wa nchi hii hatuna sera ya nchi , bali matakwa ya raisi wa zamu, ndo maana unakuta mijadala kama hii imejaa humu, isiyo na tija yoyote kwa umma na maendeleo ya Tanzania.
 
Nimeielewa concern yako. Ninachosema ni kuwa hakuna kipya utakacholeta hapa JF kuhusu mapungufu ya muungano ambacho hakikuwahi kujadiliwa.
Fikiria, hata Rais wa kwanza wa Zanzibar naye alihoji kuhusu baadhi ya mambo ambayo aliona yanaminya uhuru (autonomy) wa Zanzibar. Hakuwahi kupewa jibu muafaka hadi anafariki.
Mwanzoni ilikuwa ni Rais wa kwanza wa JMT aliyekuwa na “stranglehold” kwenye suala la muungano; hakuna aliyeweza kuhoji muungano mbele ya Nyerere.
Baadaye ni CCM kama chama kimegundua kuwa muungano ni kete yake muhimu kujihakikishia madaraka ya kisiasa na ki-dola katika pande zote mbili za muungano. Pia kuituliza Zanzibar. Wabunge wa Zanzibar wanajaza viti na kuongeza ruzuku.
Halafu, imagine Zanzibar ingekuwa nchi huru, chama tawala cha enzi zile, ASP, kingeshang’olewa madarakani siku nyingi bila msaada wa dola ya “Tanganyika”. Na kuna uwezekano mkubwa kuwa bila usimamizi wa Tanganyika, Zanzibar ingekuwa kisiwa cha vurugu mechi kila wakati.
 
Yaani pesa za Tanganyika au za muungano?
 

Wazalendo gani hao unaowakusudia? Mana Muungano ulikua ni wa Karume na Nyerere hakuna mwengne aliyeshirikishwa, Karume hakushauriana na hata baraza lake la mawaziri.
Hawa majamaa nchi walizifanya milki yao na ndio matunda yake haya. Kuendelea kuwatukuza wapuuzi kama hawa ni kujizidishia laana tu
 
Siasa za machoni huwa tofauti na zile za mbali na macho.

Mtu akitazama taratibu za kisheria zinazoandikwa vitabuni anaweza akadhani maisha halisi yapo hivyo hivyo.

Muungano wetu tangu mwanzo ulikuwa na mazingira yenye kujitofautisha na miungano mingine. Na pande zote mbili zimekuwa zikielewa ni kwanini hali ipo kama ilivyo.
 
Waulize wakubwa kiumri waliokuwepo wakati huo ili uweze kupata kuyajua mengi yenye manufaa.

Tulikuwa na dunia mbili ndani ya moja, ile ya kibepari na kijamaa na zote zilikuwa na mivutano mingi.

Walipoamua kuungana walitazama masuala kama hayo. Haikuwa dunia kama hii ya sasa ya simu za viganjani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…