Je, Rais Samia anayo haki na misingi ya kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) kwa mambo yasiyo ya Muungano?



Hakutakiwa,. hata hivyo katiba ya Warioba ingerekebisha hii kitu .
 
Si mambo ya kuhitaji kuumiza kichwa chako haya, miaka yote tumeimba, tumetisha, tumesingizia watu kuwa WANAHATARISHA MUUNGANO,
kwamba MUUNGANO ULINDWE KWA GHARAMA ZOZOTE.
Acha mambo yaende hivyo hivyo; ndiyo gharama yenyewe
 
Mtapiga kelele sana ..Rais ni Samia S Hassan..
Niliwahi kufikiria kuwa ni mmoja wa watu tafakari Jadidifu lakini kumbe sivyo kabisa. Umeshindwa kuona kuwa Mleta Mada ana hoja nzit? Huoni kuwa Katiba yetu ina tatizo kubwa? Ni hivi hakuna Serikali ya Muungano bila Tanzania Bara na Zanzibar!
Kama Katiba inasema kuna mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano mama anapata wapi nguvu za kisheria za kununua Meli za Biashara na kuzigawa huko ZNZ? Nani kasema biashara ni issue ya Muungano?
 

Kwa sheria zetu zilizopo, hakuna hata sheria moja inayomnyima Mzanzibari haki ya kushika nafasi ya uongozi wa umma Tanzania Bara. Ndiyo maana aliyekuwa mgombea mwenza wa Lissu amewahi kugombea ubunge, kama sikosei, wa Jimbo la Kinondoni akashindwa tu. Kwa ujumla, Mzanzibari yeyote aliyepo Tanzania Bara anahitaji political capital tu kuchaguliwa kuongoza kipande chochote cha Tanzania Bara!
 
Tofauti na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania isemayo Zanzibar ni sehemu ya JMT, Wazanzibar wengi huona Zanzibar ni nchi, ni taifa na ni dola. Katiba yao ya 2010 nayo inaitaja Zanzibar kuwa ni nchi, si sehemu ya JMT!

Ieleweke kuwa muungano haupaswi kuwa jumuiko la viongozi la kupeana vyeo na kuwatisha wanaohoji utata na kero za muungano zisizoisha.

Muungano mzuri huunganisha mioyo ya watu kwa kushirikiana na kuhusiana kwa hiari, kwa usawa na kwa faida ya pande zote mbili. Sivyo ilivyo kwa Tanganyika na Zanzibar na watu wao. Hakuna urari wowote ule!

Wazanzibari wengi hujiona wana nchi yao na taifa lao, na hujitambulisha hivyo kimataifa. Hawajitambulishi kama Watanzania toka Tanzania! Soma shairi hili la Mohammed K. Ghassani katika diwani yake ya N'na Kwetu (Sauti ya Mgeni Ugenini):

"Mapenzi nikupendayo, nchi yangu Zinjibari
Sitampenda mwenzio, na wala siko tayari

Mapenzi nikupendayo, nchi yangu ya uzawa
Kwa mwengine siwi nayo, na wala haitakuwa

Mapenzi nikupendayo, ewe taifa tukufu
Hatazuka mfanowo, wala sitakukhalifu

Mapenzi nikupendayo, dola yangu Zanzibar
Yang'ara kama kioo, wala hayatachakaa

Mapendo nikupendayo, watwani wangu watwani (nchi)
Twaa yote nilonayo, na wala sitakukhini (sitakufanyia khiyana)

Mapenzi nikupendayo, biladi yangu biladi (mji)
Takupenda kila leo, na daima yatazidi"

Je, hapo kuna muungano wa kweli toka katika mioyo ya Wazanzibari wengi? Hakuna! Je, Watanganyika tuna mapenzi kama hayo kwa Tanganyika??!!
 
Mambo yote ya Tanganyika yaligeuzwa kuwa ya muungano isipokuwa Zanzibar imebakia na yake yasiyokuwa ya muungano. Ila ni utata mtupu, maana Tanganyika imejificha kwenye Tanzania.

Suluhisho ni serikali moja na nchi moja au nchi mbili tofauti zenye ujirani mwema na mahusiano mema.
 
Muungano ni muhimu sana kuna mambo machache ikiwemo usafirishaji bidhaa kutoka Zanzibar kuja bara kuna leta shida sana hasa kwenye suala la ushuru hii ni nchi moja Tanzania,pia ndugu zetu wao ni watanzania wapo free kwenda sehemu yoyote ndani ya Tanzania na kuishi popote akitaka kuishi Kigoma,Tanga ,Arusha atajenga na kufurahia nchi yake waache kujitenga.
 
UMENIFIKIRISHA KITU
 
1. Rais ni Mtanzania.
2. Rais ni Kiongozi wa Serikali ya Muungano wa Tanzania.
3. Ana haki ya msingi ya kuongoza Tanzania yote, bara na visiwani.

Kinacho matter hapa si asili yake ni wapi, kama ulivyosema, Tanzania ni nchi moja, hivyo ukweli kwamba asili yake ni Zanzibar si muhimu.

Kinacho matter hapa, ni, je ana cheo gani na yupo katika serikali gani?

Mtu kama Waziri Kiongozi wa Zanzibar hastahili kuongoza mambo ya bara, si kwa sababu yeye ni Mzanzibari, bali kwa sababu ni mtumishi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, si serikali ya Muungano.Tumeona Dr. Omar Ali Juma alikuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, halafu akaja kuongoza Tanzania nzima kama makamu wa rais.

Rais wa Tanzania ana haki ya kuongoza Tanzania bara na visiwani, kwani ni kiongozi wa Tanzania nzima.

Ila, Rais wa Jamhuri ya Muungano, hatakiwi kujiingiza kwenye mambo ya Zanzibar ambayo hayapo katika Muungano.

Zaidi, ukileta habari za Uzanzibari na Utanganyika katika nchi ambayo ni Muungano, hapo unaleta ukabila.

Una m define vipi nani Mtanganyika na nani Mzanzibari katika nchi ambayo kuna watu wengi wametoka bara kwenda kuishi visiwani na wametoka visiwani kuja kuishi bara?

Utam define kwa kuzaliwa? Kwa miaka ya kukaa sehemu? Au kwa vipi?

Wazanzibari wenyewe karibu wote ni mchanganyiko wa Wazaramo, Wamakonde, Wanyamwezi na kadhalika, sasa ukisema uwabague utarudi mpaka lini?

Huyo Ali Hassan Mwinyi kawa rais wa Zanzibar na Tanzania, na kazaliwa Kisarawe. Huyu ni mtu wa wapi?
 
Wewe unataka Rais wetu atoke wapi? Nimemuuliza mtoa hoja kwa nini hakuleta hoja kuwa tulikosea kumpeleka Mzee Ruksa Ikulu na hakujibu, Hii ni hoja ya kibaguzi sababu mzanzibar na mtanganyika hawa wote ni waTz na wana haki sawa. Acheni kuleta hoja za kijinga kama hizi! Wewe huwezi kupindua katiba iliyopo hata kama ina mapungufu ambayo leo unayaona baada ya kifo cha Dikteta. Acheni mama afanye kazi, huyu ndiye Rais wetu kwa mujibu wa katiba yetu ambayo ninyi mliiona nzuri wakati Dikteta Magufuri alipokuwa madarakani.
 
UMENIFIKIRISHA KITU

HONGERA KWA MAELEZO ..
 
Kwa upande wangu siwezi kukataa kwamba hii hoja haina uzito, ili zanzibar iweze kuwa na semi-autonomous status inatakiwa Tanganyika (tuseme Tanzania) iwe ni dola kamili ambapo rais wa Tanganyika (Tanzania) anatakiwa awe na mamlaka ya uamiri jeshi mkuu, mambo ya nje na mambo mengine ya kidola huku akiachia maswala mengi ya ndani ya kiuendeshaji kwa rais wa zanzibar, mfano wa hili tunaliona kwa nchi kama China na Hongkong ambapo China ni nchi kamili lakini ina mamlaka ya kidola kwa Hongkong ambayo inajiendesha kwa mambo yake.....kwa muktadha huu urais utahusu dola la Tanganyika (Tanzania), na mzanzibar mwenye sifa ataweza kugombea urais kwa sababu ya kuwa raia wa dola zima la Tanzania na siyo kwa sababu yeye ni mzanzibar, hivyo bado atakuwa na mamlaka kamili kwenye dola zima la Tanganyika (Tanzania) na vile vile atakuwa na limited jurisdiction kwa upande wa zanzibar kwa sababu ile ni semi-autonomous state.......kwa hiyo katika kugombea urais wa Tanzania mzenji na mtanganyika wanatakiwa wawe na nafasi sawa, na sharti la kwamba rais akitoka upande huu makamu wake atoke upande mwingine halitakuwa relevant........
 
Hiyo mwenzake ni Tanzania visiwani siyo Zanzibar bwashee!
Bwashee ni hivi,

Kumbuka

NCHi inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (JMT), hii inatambuliwa rasmi na UN, AU, EAC, SADC etc.

SERIKALI ya JMT imegawanywa ktk sehemu kuu mbili kiutawala, kama ifuatavyo:

Utawala wa JMT - Mambo yote yaliyo ktk hati za Muungano ikiwemo URAIA wa JMT na hii inahusu Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.

Utawala wa Tanzania Bara - Mambo yote yaliyo ktk hati ya Muungano na yasiyo ktkt hati Muungano lakini yanayohusu Tanzania Bara pekee.

Kuhusu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) - Hii inasimamia mambo yote kiutawala yaliyo nje ya hati ya Muungano na yanayogusa Tanzania Zanzibar .

Issue ya Rais wa JMT kutoka Tanzania Visiwani:

Hili linawezeshwa na mambo yaliyo ktk hati ya Muungano hususan kwenye kipengele cha URAIA wa JMT ambapo mwananchi wa kutoka Tanzania Zanzibar ni Raia wa JMT kama alivyo mwananchi wa kutoka Tanzania Bara na hivyo basi ana haki ya kugombea nafasi yeyote ya uongozi ktk JMT ikiwemo ya kiti cha U Rais.

Tatizo ninaloliona ni suala la kuzuia wananchi wa kutoka Tanzania Bara ktk kugombea nafasi za uongozi ktk SMZ huko Tanzania Zanzibar pamoja na kuwasumbua kwenye suala la kumiliki ardhi.
 
Bwashee Zanzibar ni nchi kamili

Hakuna nchi inaitwa Tanzania bara duniani kote

Nchi inayojulikana ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mzanzibar anaweza kufanya kazi popote katika JMT

Wewe siyo mzanzibari hivyo huwezi kufanya kazi kule wala kupewa ardhi, ni sawa tu na umeenda Kenya au Uganda!
 
Hahaha, bwashee unatafuta Visa wewe, angalia kauli zako, hapa tunazungumzia TUNU za JMT🙂
 
Hahaha, bwashee unatafuta Visa wewe, angalia kauli zako, hapa tunazungumzia TUNU za JMT🙂
Zanzibar walikuwa makini sana wakati wanaingia kwenye huu Muungano vinginevyo wangemezwa kama Afro shiraz ilivyomezwa na Tanu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…