Je, Rais Samia anayo haki na misingi ya kuongoza Tanzania Bara (Tanganyika) kwa mambo yasiyo ya Muungano?

Haya Mambo ya Muungano yamekuwa na kelele miezi hii 2 toka Jiwe afariki.

Kitu nimegundua Watanganyika wengi sio kwamba hawampendi Mama Samia ila hawapendi kuongozwa na MTU kutoka Zanzibar.
 
Kwani Magufuli alikuwa anawatawala hadi mambo yenu ambayo sio ya Muungano??.
Hapa issue ni kuwa hatutaki kutawaliwa na Mzanzibari hadi kwenye mambo ambayo sio ya Muungano.huyo Ali Hassan ana bahati watu wengi walikuwa hawana shule.
 
Usije ukawa unaongea kumbe nawe ni wa unguja ambao ni wabara tu,wazanzibar ni hao kutoka Pemba akina Samia na Maalimu self.
 
Watu wanongea ongea tu Mara tumpe support,haya mambo CCM inayachukulia kilaini lakini tu kila Mtawala anaogopa ku ya solve lakini haya isipokuwa kizazi chetu hiki kuna siku CCM itakuja kuanguka na kutatokea vyama tofauti katika hizo Nchi ndipo kimbembe kitanzia hapo.
 
mh nipo Tanzania ila sikufahamu kabisa mambo hayo,kikubwa tusameheane hayo ni mapungufu ya kibinadamu
 
Kwani Mzanzibari si Mtanzania? Mbona Mwinyi na Jumbe waliongoza Zanzíbar ilhali si Wazanzibari?
Je katiba inasemaje kuhusu Zanzíbar kutoa raisi au inasema MTANZANIA tu ?
 
M
Mjadala huu ni mpana sana ila elewa kuwa suala la mapato-TRA ni la kimuungano isipokuwa kwa makubaliano baadhi ya mapato ie uhamiaji yanabaki zanzibar. Hivyo wao kupata mgao wa fedha ni haki yao kama walivyopewa juzi fedha za muungano
 
M

Muundo wa United Kingdom ?, United Arab Emirates? United States of America?.....
 
N
Ndiyo maana it is high time kupitia Katiba yetu ya 1977 kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
 
Kwani Magufuli alikuwa anawatawala hadi mambo yenu ambayo sio ya Muungano??.
Hapa issue ni kuwa hatutaki kutawaliwa na Mzanzibari hadi kwenye mambo ambayo sio ya Muungano.huyo Ali Hassan ana bahati watu wengi walikuwa hawana shule.
G55 ya nini kwa sasa. Lets give time kwa mama atulie kwenye kiti kisha haya Muungano tutayazungumza baadaye na yeye kuyafanyia kazi kwa mujibu wa Katiba na atakavyoona inafaa. Kwa sasa yupo kwenye nafasi hiyo kwa mujibu wa katiba iliyopo. Fullstop.
 
Yani kweli inaonesha kuna watu hawajapenda kabisa mama kushika uongozi..inamaana hawakujua toka alipokua makamu wa rais kuwa likitokea la kutokea yeye ndo rais ?
Ukiona wazazi wako wanaanza kuandika wosia lazima uogope japo unajua kabsa kifo kipo.
 
Yani kweli inaonesha kuna watu hawajapenda kabisa mama kushika uongozi..inamaana hawakujua toka alipokua makamu wa rais kuwa likitokea la kutokea yeye ndo rais ?
Kuna watu mpaka leo hawaelewi kwamba hakuna raia wa Zanzibar, kuna raia wa Tanzania tu.

Na sifa moja qualifier ya kikatiba kuwa rais wa Tanzania ni suala la uraia, si suala la ukabila wala umetoka upande upi wa Muungano.
 
Mleta hoja Tuorodheshea mambo ambayo siyo ya Muungano, natuambie km Rais SSH hajateua mawaziri wakusimamia hayo mambo na pia tuambie kuwa Aliyekuwa Rais awamu ya pili kama hakuyasimamia hayo mambo kwa maslahi ya Tanzania Bara.



Je, Mzanzibari akiwa Rais wa Muungano

-hateuwi mawaziri wakuongoza hizo wizara?

-hateuwi watendaji?

-hapeleki fedha za maendeleo huko?

-anafuta hizo wizara?



Nyerere alishawahi kusema Muungano wa serikali mbili ni sera ya CCM ila Watanzania wakitaka Serikali tatu CCM ijiandae kisaikolojia. Wakati wa mapendekezo ya katiba mpya Watanzania walijibu hayo maswali yako walitaka serikali tatu, kwasababu ujengaji hoja wa CCM nikuangalia maslahi binafsi basi mkajitoa akili, sasa mkachukue mnakowekaga akili zenu then turudi kwenye maswala ya katiba. Kwasasa acha kazi iendelee siyo mara ya kwanza Rais wa Muungano kutokea Zanzibar.
 
N

Pia kwenye bunge letu kuna wabunge wanaochaguliwa toka Zanzibar kama wabunge wa Bunge la muungano, lakini wanakaa katika bunge hilo hata kwa mambo yasiyo ya muungano. Kuna mbunge mmoja aliwahi kusema wazi hilo bungeni. Nani anawalipa posho zao ni serikali ya Tanganyika (Tanzania). Huko Zanzibar wana tayari wawakilishi wao, sijui kuna maeneo wana wabunge wawili sijui. Na pia wanapata pesa za ubunge za jimbo, inalipa Tanganyika. Jamani huu muundo si sawa kabisa. Hakuna anayekataa muungano, tunachoakataa ni muundo ufanyiwe marekebisho. Ili muungano uwe muungano ni muhimu kutofautisha kati ya Tanganyika na Tanzania, ili rais atawale Tanzania na katiba ya Tanzania na awepo kiongozi wa Tangayika na katiba ya Tanganyika. Kama ilivyo Zanzibar wana katiba yao, bendera yao na Rais wao.
Nafikiri pendekezo la katiba ya Warioba ingefaa liwekwe tena, kwa sababu jambo hili haitakwisha kulalamikiwa.
Makamu wa Rais amesema hatavumilia ye yote anayevuruga muungano. Ukweli ni kwamba hakuna anayekataa muungano kinachopingwa ni mfumo au muundo wa Muungano. Mbona nchi nyingi zina muungano wa kila nchi zilizouungana inajulikana kwa kuwa na uongozi wake.
Kitu kimoja nilichowahi kukusikia wanasiasa wanajisifu kuwa Muungano wetu ni wa kipekee duniani. Kwahiyo lazima tuudumishe. Sielewe tuudumishe kwa maslahi ya nani. Tumekaa miaka yote hii, ila naona kuna mabavu yanatumika kulinda muungano huu. Watu wanafukuzwa kila mmoja anapouliza juu ya jambo hili. Na sisi Watanganyika ni waoga mno hatuna ujasiri wa kudai nafasi ya Tangayika katika muungano huu.
Kama Zanzibar ni nchi iliyoungana na Tanganyika kwanini isitoe cho chote kwenye Muungano kwa uwiano wa ukubwa wake. Ukweli tumekamatwa na tunaendelea kuchezewa huu mchezo na siasa za nchi hii.
Mungu asaidie uongozi wa Chama tawala hivi wana masilahi gani katika mfumo huu ambao umeweza kupingwa miaka na miaka. Lakini wenye mabavu wachache wameshikilia usukani.
 
Wanajifanya wehu hawa.

Yaani mara moja hii wanajifanya wamesahau yooote haya
 
Hoja yako inakosa mashiko unapoongelea suala la serikali ya Tanganyika. Hakuna serikali ya Tanganyika duniani, labda ndotoni.
 

Muungano wa JMT (wa “Tanzania bara” na Zanzibar) ni muungano wa kipekee duniani. NA kwa msimamo wa Serikali na chama tawala, ni tunu muhimu ya taifa la Tanzania. Watanzania “wazalendo” hawapaswi kuhoji tunu hii.

Mkuu uliyoandika hapa yanaeleweka vizuri sana tangu enzi na enzi. Wako wengi waliojaribu kuhoji mikingamo ya muungano huu kama wewe. Tafuta walihitimishaje hizo juhudi zao na wao waliishia wapi. Juzi hapa VP katoa angalizo kwa wanaotaka “kuchezea” muungano.

Kwa kifupi, hakuna mjadala wenye tija unaoweza kufanyika kuhusu mambo ya muungano wa JMT. Hivyo, FACT ni kuwa STATUS QUO inabakia kama ilivyo. SSH ndiye Rais wa JMT hadi (hatujui lini) na ana madaraka yote (absolute power) juu ya mambo yote ya Tanzania isipokuwa yale exclusive kwa Zanzibar pekee. Hakuna nchi inayoitwa “Tanganyika” duniani.
 
Ila mbona Zanzibar inaongozwa kwenye mambo yasiyo ya Muungano na Rais mwenye asili ya Tanganyika (Hussein Mwinyi).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…