Salaam, Shalom!!
Kuna mkanganyiko unaendelea katika majukwaa ya kisiasa juu ya kuchapisha fomu Moja ya mgombea Urais 2025.
Kwa wakati tofauti Mh Kinana na Mh Majaliwa wanarudia rudia kuwa 2025 itakuwa Awamu ya pili ya Mh Samia hivyo Utaratibu wa CCM uendelee wa kuchapisha fomu Moja tu.
Nijuavyo, Awamu ya kwanza ni ya kupigiwa kura na wananchi kama mgombea Urais na kushinda uchaguzi, Si vinginevyo.
Swali linakuja,
Ikiwa 2025 itakuwa Awamu ya pili Kwa Mh Samia, je mgombea mwenza wa Rais Samia katika Awamu ya kwanza alikuwa nani?
Karibuni Kwa ufafanuzi. 🙏