Je, Rais Samia Suluhu ndo Deng Xiaoping wa Tanzania?

Duniani ni wawili wawili! Wewe huamini ilo?
Wawili wawili ni mtu na mkewe. Sivyema MTU akifanya Jambo afrika mnatafuta wa huko nje wakumlinganishia, huo niutumwa wa kifikra...hatufanani nao kifikra,kitabia,kimazingira,kiimani,kihistoria,kijiografia hata kirangi.
 
K
Wawili wawili ni mtu na mkewe. Sivyema MTU akifanya Jambo afrika mnatafuta wa huko nje wakumlinganishia, huo niutumwa wa kifikra...hatufanani nao kifikra,kitabia,kimazingira,kiimani,kihistoria,kijiografia hata kirangi.
wa iyo kulinganisha watu ni utumwa? Huko shule ulisomea ujinga?
 
Of course kwenye uchumi mambo yatanoga ila kwenye siasa ataamua yeye afuate mambo ya kukandamiza upinzani au auende Katiba mpya.
 
Mungu atupe uzima. Kwa niliyoyasikia ikifika 2030 tutaufufua huu uzi.
Kwenye uchumi atafaulu Sana kwa sababu yeye pia ni mfanyabiashara kwa hiyo anaamini kwenye uchumi wa soko.

Unadhani alipisema tv yake inakula hasara alipenda? Uchumi ukichanganya vyombo vya habari vinanufaika kwa matangazo.

Nakumbuka kabla ya 2015 taa za mijini zilikuwa zinapambwa na matangazo ya biashara na ilikuwa dili saizi ziko tupu hakuna wa kugusa maana uchumi umeanguka Sana.
 
Mimi ukitaka nikuchukie uje na sera zako za kipumbavu za ujamaa na kutegemea serikali kila kitu ndio maana nilimchukia mwendazake nakuona ni mtu mjinga sana, Duniani kote ujamaa ulishafeli yeye akaanza kuleta uchumi ukaporomoka akaanza kupora pesa za watu.

Mama hana ule ujinga na ujuha,kwa mda mfupi wizara zote mama zimepata mafungu ya uhakika kilio cha Tarura kimepatiwa ufumbuzi,maji na sekta ya Elimu vyote ameviweza kwa mda mfupi.

Kitu kikubwa ambacho afanye mwaka ujao ni kupunguza VAT kutoka 18% hadi 10-12% hapa biashara nyingi zitafunguka,atapata kodi nyingi na demand itakuwa kubwa mwisho wa siku itastimulate uchumi Sana.
 
Msumari wa VAT ndo unaenda kumaliza kila kitu
 
Kuna wawekezaji wamekuja na wana mtaji wa pesa ndefu wameanza taratibu za kufanya uwekezaji wao hapa Tanzania.
Mama akiendelea kukaza shingo kuhusu katiba mpya hawa wawekezaji watakimbia ama watakimbizwa
 
Mie hali ilianza kunishtua mwaka 2018. Mjini kampuni nyingi zilianza kupunguza wafanyakazi. Nyingine zikaanza kubana matumizi. Posta nikaanza kuona inakufa, Quality Centre na Quality Plaza ndo hadi zilinitoa machozi maana pale ni maelfu ya watu walipoteza ajira.
 
Mama akiendelea kukaza shingo kuhusu katiba mpya hawa wawekezaji watakimbia ama watakimbizwa
Fuatilia siasa za Singapore alafu Njoo tena urudi humu. Kwenye ubabe wa kisiasa kunaweza kuwa na wawekezaji wengi tu ili mradi ubabe wenu wa kisiasa hauathili uwekezaji wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…